Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA: MPANGO WA CONGO.


SEHEMU YA 12



Alipofika nje hakutaka kutoka bila walau kupata maelezo kuhusu OCCID na alipokwisha kuyapata maelezo kuhusu makazi ya mtu huyo akaitisha usafiri wa bodaboda kuelekea kuitafuta Club D.

Tatizo hajui ilipo.

********

Remi baada ya kuona mnyukano wa wanaume wawili katikati ya milango ya Buzuruga Plaza; hakuwa na budi kufanya maamuzi alioona ni sahihi kwake.

Mwanzo alitamani kubaki ili aone hatima ya kijana waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku Contractors na pia kugeuka kuwa msaada wake wakati akiwa amekabwa na mtekaji.

Wazo hilo alilipinga haraka hasa baada ya kushindwa kuwa na imani na kijana anaemtetea.

“kama ni mbinu yao ya kunitia mikononi!” alijiwazia na kisha haraka akawatazama akaona bado wamewekeana mchoro wa mapambano na pembeni aliona umati wa watu ukizidi kujongea huku kila mmoja akijaribu kuwa wa kwanza kuwa shuhuda wa mtanange ule wa kibabe.

Kisha akarudi tena kuwatazama mafahali wale na hapo akakutanisha macho yake na mtekaji na akaona jinsi macho ya mtekaji yalivyomakini nae.

Akangoja nafasi itokee.

Mungu alijibu maombi yake.

Ni wakati mtekaji alipojaribu kumnasa kwa kumpita hasimu wake na kuangushwa kwa mtama safi aliopigwa na hasimu wake.

Wakati mtekaji anamgeukia hasimu wake,ni wakati huo alipoona nafasi ya yeye kutokomea.

Akapenya katikati ya watu na kisha akakimbia kama mwizi aliekoswa na jiwe.

Mbio zake zilimfikisha njia panda ya mataa Buzuruga. Hapo akatulia huku akitizama huku na huko na alipohakikisha Hakuna anaemfuatilia; akaamua kuvuka na kuingia ndani ya kituo cha mabasi Buzuruga.

Alipokwisha kuingia tu tayari wahudumu na wapiga debe wa mabasi yaendayo Musoma na maeneo mengine walianza kumzonga huku wakinadi ubora wa mwendo na huduma za mabasi yao.

Hakuwajali!.

Akazidi kuwakwepa huku akionekana kupagawa kwa kuvutwa vutwa na baadhi ya wapiga debe wasio na staha.

Walipoona sio msafiri wakaamua kumuacha ajiendee zake.

Alipokwwisha kuachwa na wasumbufu hao ambao baadhi waliishia kumtusi,nae hakuwajali akaendelea na hamsini zake.

Miguu yake ilikoma akiwa katikati ya soko la Buzuruga.

Tumbo lilikosa ushirikiano lakini pia alihitaji kutuliza akili na kuamua jambo la kufanya wakati huo.

Alijongea katika mgahawa mmoja uliokuwa sokoni humo kisha kwa pesa kidogo aliokuwa nayo akaagiza chai ya moto na wali mweupe.

Alikula taratibu huku mawazo lukuki yakikizonga kichwa chake.

Licha ya akili yake kuuona ugumu wa kumpata Mwasu kwa siku hiyo,ila bado aliona mtu sahihi zaidi wa kumfikia ni Mwasu ili walau apate ushauri kutoka kwake na namna ataweza kuepuka masaibu yanayomzonga.

Lakini jambo moja lilimchanganya; ni vipi watu wale wamefika haraka Mwanza na pia wamewezaje kufuatilia nyendo zake kirahisi vile!?

Alijipa utulivu wa akili.

Jibu halikukawia japo hakujua kama ndilo litakuwa sahihi ama la.

Alidhani ya kwamba, watu wale wabaya walijua akifika Mwanza; Mtu wa kwanza kumtafuta atakuwa ni Mwasu na ndio mana alikuta wamemtangulia.

Alitoa kimkoba kidogo chenye ukubwa Sawa na pochi za akina dada ila hiki kilikuwa ni cha ngozi na pia kilikuwa na mikanda mirefu myembamba sana. Tofauti nyingine ni kuwa kimkoba hiki kingekuwa kinamilikiwa na wadada wa mjini basi ungekuta kimejaa vipodozi; kioo na taulo moja ya kike. Ila mkoba huu wenyewe ulikuwa na karatasi nne tu.

Karatasi hizi zilikuwa zinatokana na zao la miti hivyo hazikuwa nyeupe bali zilikuwa ni kaki.

Alitazama mazingira aliokuwapo na alipohakikisha hakuna anaejali anachokifanya,akazitoa zote.

Zilikuwa zimekunjwa kwa kuzungushwa kisha kwa juu zikabanwa na kamba nyembamba sana.

Alipokwisha kuziweka pembani karatasi zile akarudisha tena mkono kwenye mkoba ule na alipoutoa alikuwa na kadi ndogo ya kuhifadhi kumbukumbu.

Akakitazama kikadi kile kisha akayakumbuka maneno ya mtu aliempa vitu vile.

Kabla hajapewa alisisitiziwa sana kuhifadhi kadi ile kuliko karatasi, yani bora karatasi zipotee ila si kadi ile.

Lakini pia alikumbuka kuonywa ya kuwa kama anataka aendelee kuishi ni lazima awe na vitu vile huku akiambiwa kama atapokonywa basi ndipo uhai wake utakapoishia.

Akazishusha pumzi kwa mkupuo kisha akawaza kuifanyia kitu kadi ile ili awe na hakika nayo katika usalama wake na kadi ile.

Lakini wakati akikumbuka kurudia chakula mezani, wazo moja likapita kichwani mwake.

Polisi!!

Yesi aliwaza kwenda kuutua mzigo wa mateso ule kituo cha polisi. Japo aliamini anaweza kuzungushwa sana hadi kushugulikiwa,lakini aliamini ni lazima watalishugulikia kulingana na uzito wa suala lenyewe.

Akapitisha wazo la kwenda kituo cha polisi.

Alipogeukia chakula chake alikuta kimepoa na chai imegeuka kuwa maji ya baridi.

Akakimalizia kisha akalipa na kuinuka kisha akatafuta njia yenye watu wengi na kujichanganya akatoka nje ya kituo cha mabasi.
*****

Dakika ishirini badae alikuwa anatazamana na kituo cha polisi Nyakato Neshino.

Aliingia hadi mapokezi kisha akaomba kuonana na mkuu wa kituo kile.

Aliruhusiwa kumuona bila kuulizwa maswali mengi kama alivyotarajia.

“Unaitwa nani binti” aliuliza mkuu wa kituo.

“Remi” alijibu binti.

“Ndio Remi; unaishi wapi na utokea wapi” aliuliza tena mkuu wa kituo.

“Natokea Kigoma” alijibu binti.

Mkuu wa kituo akamtazama binti kwa makini sana kisha akatikisa kichwa kwa alichokiona kutoka kwa binti yule.

Mkuu wa kituo alihisi binti atakuwa na matatizo kiakili kwa sababu ya muonekano wake kuwa mchafu na anaonekana hajaoga siku kadhaa.

Hiyo huwa si kawaida ya wadada wenye urembo kama wa yule binti japo hakuwa akiuthamini urembo wake.

Mkuu wa kituo pia aliyajumlisha majibu ya binti yalivyo ya mkato kuzikamilisha hisia zake.

“Shida yako tafadhali” alisema mkuu wa kituo.

“nimepoteza wadogo zangu” alijibu binti.

“wamepoteje?”

“sijui walivyopotea ila wamepotea”

Mkuu wa kituo akaingiwa na gadhabu kwa sababu alijua kabisa binti yule hayuko sawa kiakili na pale anampotezea tu muda wake.

“Ok!!, unahisi ni nani aliefanya hivyo?” akauliza mkuu wa kituo huku akijaribu kuzizuia gadhabu zake.

“ninao ushahidi wa mwanzo huu hapa” alijibu binti huku akimpa Mkuu wa kituo karatasi nne ambazo zilionekana kabisa zimetolewa nakala kwa kirudufu muda si mrefu.

Mkuu wa kituo akazichukua karatasi zile na kuzifunua.

Akajikuta akicheka sana huku gadhabu zikimuisha na kuamini kweli binti alieyeko mbele yake ni mgonjwa wa akili.

“Dada nadhani unahitaji msaada wa haraka sana” alisema mkuu.

Remi akatabasamu kwa mara ya kwanza tangu aingie ndani ya jiji la Mwanza.

Lakini hakujua kauli ya Mkuu wa kituo haikumaanisha alivyodhani yeye.

Furaha na matarajio yake yakakoma gafla.

“sio msaada unaodhani wewe binti,msaada ninao kupa inabidi twende hospitalli ukapime akili yaezekana umekuja hapa ukiwa hujui”

E bana eeh!

Mshangao ukatamaradi usoni pa Remi huku akiona kabisa alivyodhaniwa na ukichaa tena mbele ya serikali.

Amah!!

“Afande kwanini…?” Alijikuta anakwama kuuliza.

“Remi huoni unaumwa wewe?,hivi unakujaje hapa ukiwa na karatasi zilizoandikwa kwa lugha ya kifaransa afu useme zinahusiana na upotevu wa wadogo zako?”

Jama!!

Akapagawa na hapo ndo akajua lugha iliotumika pale ni kifaransa mana tangu mwanzo alishindwa kusoma kilichopo kwa sababu hakuwa na uelewa wa lugha ile sasa hakujua ya kuwa hata hapo kituoni wapo wasiojua kifaransa kama yeye japo alishukuru walau tu kuambiwa ni kifaransa kimetumika kuziandika karatasi zile.

“anyway, nenda ofisi namba kumi ueleze shida yako vizuri kisha uwape hizi karatasi,sasa ikibainika unacheza ujinga utajuta kucheza na serikali” alisema kwa mkwara mkuu wa kituo huku akimpa Remi karatasi zake.

Remi alijua hajacheza vizuri karata yake ili aeleweke. Lakini nafsini mwake alijiambia yupo sahihi kuanza vile mana hajui ni nani yupo nyuma ya sakata lile na alijua kabisa hata serikalini wamo.

Remi hakutaka kufunguka lolote zaidi pale na ni baada ya kuhisi tangu mwanzo mazungumzo yake na mkuu yule yatakavyokuwa kwa sababu alionekana mjivuni sana bwana yule

Lakini pia hakutaka kuongea sana mana angejulikana si Mtanzania kwa lafudhi yake na hiyo ingemletea shida zaidi mana angekufa na ushahidi wake ndani ya gereza kwa kuwa mhamiaji haramu wala hakuna ambae angejua ni Mkimbizi alietoroka kwenye kambi ya wakimbizi huko Kigoma.

Ofisi namba kumi ndani ya jengo lile la kituo cha polisi ilikuwa inakaliwa na ofisa mkuu wa upelelezi katika kitengo cha makosa ya jinai na pia kilishugulika na ujasusi wa ndani.

OCCID alikuwa anatazamana na Remi na baada ya kumsikiliza maelezo yake ambayo yalikuwa sawa na aliyotoa kwa mkuu wa kituo,akazichukua karatasi zile kisha hakuzipitia akaziweka pembeni huku akimwahidi kulishugulikia swala lile kikamilifu.

Remi akaaga na kuondoka ndani ya ofisi zile na alipotoka nje alilakiwa na macho ya watu wawili tofauti.

Mmoja alikuwa ni Mtega nyoka na mwingine alikuwa ni askari wa usalama barabarani aliekuwa anaripoti kwa ajili ya kurudi nyumbani kupumzika.

Alimtizama kwa jicho lisilo la wema ila si yeyote aliejua isipokuwa ofisa yule wa usalama barabarani.

Tofauti na siku Zote ambazo ofisa yule huripoti kisha kuondoka,ila siku hiyo akabaki pale kituoni kwa dakika kadhaa, lengo ni kujua njia alizopita Remi na alifuata nini pale kituoni.

Hilo alifanikiwa mnoko yule.

*****

OCCID hakutaka kupuuzia lalamiko la Remi lakini pia hakutaka kuzipotezea karatasi zile hivyo haraka akamuita kijana mmoja kutoka kitengo cha upelelezi cha polisi (Intelligence Police) ambae anaijua lugha iliotumika pale ili ampe kazi hiyo ya kushugulikia kesi iliohusisha lugha ya kigeni.

Mwanzo hakujua kama lile ni suala kubwa sana na ndio mana alipomwita Intelligence Ofisa au maarufu ‘IO' hakuhitaji kutafsiriwa pale mana alijua itakuja kwenye ripoti atakayopewa badae.

Waswahili walisema; ‘mazoea mabaya' hilo lilidhihirika ndani ya ofisi zile za upelelezi mana hata IO alipopewa maelezo kidogo ya kesi ile na karatasi hakujihangaisha kusoma mbele ya mkubwa wake, akatoka na kwenda ofisini kwake kushugulikia baadhi ya viporo na kisha usiku akitulia aanze kupitia karatasi zile na ahsubuh aamkie kesi hiyo endapo ingekuwa na tija sana.

Hakujua yajayo!!

Hakujuwa kesho anaijua mungu pekee na hakuna binadamu aliewahi kuifikia kesho isipokuwa mauti pekee ndio hukufikisha katika ukomo wa kesho ila si mwanadamu aliehai mana kila siku ni kesho ijayo.

Hakujua! Hakujua!
 
Ivi hizi simulizi mbona zinaishiaga kitonga
 
Rip IQ
Sent using Jamii Forums mobile app
 
shemejiiiiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…