Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Riwaya :Mpango WA kongo

Sehemu ya nane

Lakini mbali na hivyo alikuwa na mtego wake kwa yule mhudumu mana kama mhudumu akisimama kutoa chenji asimkute, basi lazima atatoka nje kumtafuta na ndio mana alikuwa anaelekea kwenye nyumba za kanisa ili atizame vizuri harakati za kuingia na kutoka ndani ya mgahawa ule wa Tunde.

Haikuwa dakika nyingi alichokitarajia alikiona!!

****

Mhudumu alipigwa na butwaa bada ya kuinuka na kumkosa mteja wake.

Akapagawa!!.

Alipagawa kwa sababu hakudhani, sekunde chache vile mtu ampotee kirahisi tu.
Akajaribu kungojea dakika moja au zaidi, lakini tofauti na matarajio yake hakumuona Honda.

Akaamua kutoka nje lau aone uelekeo aliopitia ili tarifa yake ikamilike kwa wakubwa wake.

Mhudumu yule alitoka hadi nje, akaangaza kushoto na kulia hakuona mtu wala kivuli chake.

Shiiit!!” mhudumu akamaka huku mikono ikiwa imeshika kiuno asijue afuate lipi.

Akiwa hajui lipi afanye mara gari ikasimama karibu na miguu yake na hakujiuliza mara mbili akasogea kwenye kioo cha upande wa dereva,akasikiliza kidogo kisha akarudi akandoka kurudi mgahawani.

Kutokea pale alipokuwa ametulia; Honda aliyaona yote yaliofanywa na mhudumu yule nje ya mlango wa mgahawa wa Tunde.

Hata wakati gari inakuja na kusimama na kisha kuzungumza na walioko ndani ya gari, yote Honda aliyaona na sasa alitaka kuona watu wale waliokuwa ndani ya gari wangelifanya nini, lakini pia hakujua wapo wangapi japo aliamini ni zaidi ya mtu mmoja.

Aliendelea kusubiri hadi aone hatima ya watu wale.

Baada ya dakika kadhaa milango ya nyuma ya ile gari ikafunguliwa na kutoka kila upande wakashuka wanaume wawili waliojazia kimazoezi hasa. Wanaume wale wakaangaza huku na huko kisha wakaingia ndani ya mgahawa ule wa Tunde.

Katika hesabu za Honda aliamini ndani ya gari kutakuwa bado na watu wawili,mmoja dereva na mwingine yupo upande wa pili wa dereva.

Kwa kasi aliambaa na kuta za nyumba kadhaa kisha bila kuonesha tashwititi yoyote akavuka barabara huku hesabu zake zikiwa ni namna ataweza kuifikia ile gari bila kutiliwa shaka.

Alipovuka barabara tu akainamisha uso chini kisha akaanza kutembea kama mlemavu mwenye mguu mmoja mfupi na mwingine mfupi huku mkoba ukiwa unaning’inia mgongoni.

Hila za Honda zikazaa matunda, hadi analifikia lile gari hakuna aliekuwa amemtilia shaka na kwa kasi ya hewa akafungua mlango wa nyuma na bila kujiuliza akakaa kwenye kiti huku akiwa amewaelekezea bastola wale watu wawili waliokuwa wamekaa viti vya mbele wakiwa na mzubao usio semekana huku dhahiri hofu ikiwa juu yao.

“ondoeni gari hapa!” alisema Honda huku akiwa makini ili asifanyiwe fitina.

Hakuna aliemjibu wala kutekeleza amri yake nae akajua jamaa wanapoteza muda ili wale mabaunsa watokee na wakitokea hatari ipo kwake tu.
Hilo kamwe hakutaka litokee.

Bastola yake iliokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti ikatema jiwe la moto na kupenya katikati ya uti wa mgogo wa mtu aliekuwa upande wa kushoto wa dereva na wala mtu yule hakuomba hata maji akawa hana mawasiliano huku damu ikimwagika kama bomba bovu.

Dereva hakuwa na namna, akaiondoa gari bila kujua ni wapi anapaswa kuelekea.

“endesha hadi nitakapokupa maelekezo mengine.” Sauti kavu ya Honda ikaunguruma bila chembe ya mzaha.

****
Safari ya Honda ilikuwa imegubikwa na ukimya wa kutisha na baada ya kitambo kidogo Honda akamwelekeza pahali alipopswa kugesha gari.

Mateka aliegesha gari kando kidogo ya nyumba ya marehemu Bulembo na
Baada Yakuhakikisha mateka wake amezima gari, kwa kasi ya radi akampiga kwa kitako cha bastola chini kidogo ya kisogo na mateka wake akapoteza fahamu hivyo ndani ya gari akawa na watu wawili, mmoja hana fahamu na mwingine bila uhai.

Haraka akashuka na kulekea lango la kuingilia ndani ya nyumba ya Bulembo na alitegemea kukuta utepe wa polisi wa kuzuia aisehusika kuingia pale na ndivyo ilikuwa.

Licha ya kuwapo utepe, pia kuliwa kimya sana kuashiria hakuna askari anaelinda pale na kuhakikisha zaidi akaingia hadi ndani ya utepe na kujaribu kuita ila hakuitikiwa zaidi alisikia sauti yake tu ikitengeneza mwangwi kwenye eneo pweke.

Haraka akarudi kwenye gari na kumchukua mateka wake ambae bado alikuwa amepoteza fahamu, akaingia nae moja kwa moja ndani na huko akamfunga vizuri kwenye kiti kisha akarudi ndani ya gari na kuliondoa kurudi walikotokea ambapo kwa kitambo fulani akaingia njia za vichochoro kulitelekeza gari ile na maiti yake. Huku akichukua baadhi ya vitu alivyodhani vinaweza kumsaidia.

Alikodi usafiri binafsi na kurudishwa hadi karibu na nyumba ya Bulembo, akalipa pesa kisha akaelekea kwenye kichochoro fulani lengo likiwa ni kumchanganya dereva endapo akibanwa huko ili atoe taarifa zake.

Huko huko alikopitia akajikuta yupo ndani ya mitaa yenye nyumba anayoihitaji.

Alipokwisha kuingia ndani, moja kwa moja akaanza upekuzi wake huku akiwa amemweka mateka wake kama kiporo.

Licha ya kukuta ukaguzi wa hali ya juu lakini bado aliamini kuna kitu kitakuwa mle ndani chenye kuweza kumsaidia hasa katika mambo matatu makubwa.

La kwanza ni kujua mhusika wa mauaji ya Bulembo na balozi Aly Sapi, lakini kubwa zaidi ni kuhusu tetesi za kuwapo mtu ambae historia hailezi wazi kuhusu kifo chake, na sasa tarifa za mwanzo za marehemu Bulembo zinasema yupo hai na anampango wake mahususi juu ya nchi ya Tanzania.

Mpango gani;?

Ndilo lilihatajika kufumbuliwa na mpelelezi Honda.

Honda alikuwa ametumia zaidi ya dakika kumi na tano bila kupata hata dalili ya maelezo yenye kumsaidia.
Alijishika kiuno huku akitembeza macho kila kona ya chumba kilichotumiwa na Bulembo kulala huku kichwani akifikiria kuacha kufuatilia njia aliotumia Bulembo mana inazidi kumwacha njia panda na muda unazidi kwenda.
Alitamani sasa kuingia kivingine na kwa njia zake ili apate ukweli wa sakata lile.

Wakati akili ikitafakari maamuzi; macho yakanasa kitu ukutani juu kidogo ya mto na mto huo ulionekana ndio ulikuwa unatumiwa na marehemu Bulembo kwa kuwa ulikuwa unaonekana kuwa na mafuta ya nywele yaliotengeneza weusi kidogo kwa kulaliwa mara kwa mara.
Juu kidogo ya tendegu la kitanda aliona mikwaruzo, akasogea kwa hatua za aste aste na alipofikia karibu aliona maandishi ila yalikuwa ni maandishi yale yale alioyaona kwenye kikaratasi alichokitafuna wakati akiwa mikononi mwa Sajini Kebu.

Na yalikuwa yamepangiliwa vile vile kama yalivyokuwa kwenye karatasi alioitafuna.

“142BOULEVARD DU JUIN
B. P. 1612
KINSHASA CONGO (81)”

Aliyatazama tena maandishi yale, bado hakuwa amepata walau wazo la kujua Bulembo alitaka kumaanisha nini japo alijua hii ilikuwa ni anuani ya ubalozi wa Tanzania Lakini kilichomchangaya zaidi ni ile alama ya mabano kisha zikafuatia namba (81) ilimaanisha nini hii namba! Hakujua wala kufikiria mbali zaidi ya kuzidi kuchanganyikiwa na asijue afuate lipi katika anuani ile

***
Angalizo ; Mnaosoma na kupita kimya kimya hamtendi haki kabisa, kama haivutii sema, umependa sema pia huo ndio ujira wangu wala sihitaj pesa yako ili niendelee kuweka hapa mtaji Pekee ni koment yako ambapo itasaidia watu wengi kuisoma.

Au mnataka na kusibiri isitishwe ndo muibuke na kutoa mitusi? Wakati inapopostiwa hatuwaoni?
Karibuni kwa maoni
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA: MPANGO WA CONGO.

SEHEMU YA 12

Alipofika nje hakutaka kutoka bila walau kupata maelezo kuhusu OCCID na alipokwisha kuyapata maelezo kuhusu makazi ya mtu huyo akaitisha usafiri wa bodaboda kuelekea kuitafuta Club D.

Tatizo hajui ilipo.

********

Remi baada ya kuona mnyukano wa wanaume wawili katikati ya milango ya Buzuruga Plaza; hakuwa na budi kufanya maamuzi alioona ni sahihi kwake.

Mwanzo alitamani kubaki ili aone hatima ya kijana waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku Contractors na pia kugeuka kuwa msaada wake wakati akiwa amekabwa na mtekaji.

Wazo hilo alilipinga haraka hasa baada ya kushindwa kuwa na imani na kijana anaemtetea.

“kama ni mbinu yao ya kunitia mikononi!” alijiwazia na kisha haraka akawatazama akaona bado wamewekeana mchoro wa mapambano na pembeni aliona umati wa watu ukizidi kujongea huku kila mmoja akijaribu kuwa wa kwanza kuwa shuhuda wa mtanange ule wa kibabe.

Kisha akarudi tena kuwatazama mafahali wale na hapo akakutanisha macho yake na mtekaji na akaona jinsi macho ya mtekaji yalivyomakini nae.

Akangoja nafasi itokee.

Mungu alijibu maombi yake.

Ni wakati mtekaji alipojaribu kumnasa kwa kumpita hasimu wake na kuangushwa kwa mtama safi aliopigwa na hasimu wake.

Wakati mtekaji anamgeukia hasimu wake,ni wakati huo alipoona nafasi ya yeye kutokomea.

Akapenya katikati ya watu na kisha akakimbia kama mwizi aliekoswa na jiwe.

Mbio zake zilimfikisha njia panda ya mataa Buzuruga. Hapo akatulia huku akitizama huku na huko na alipohakikisha Hakuna anaemfuatilia; akaamua kuvuka na kuingia ndani ya kituo cha mabasi Buzuruga.

Alipokwisha kuingia tu tayari wahudumu na wapiga debe wa mabasi yaendayo Musoma na maeneo mengine walianza kumzonga huku wakinadi ubora wa mwendo na huduma za mabasi yao.

Hakuwajali!.

Akazidi kuwakwepa huku akionekana kupagawa kwa kuvutwa vutwa na baadhi ya wapiga debe wasio na staha.

Walipoona sio msafiri wakaamua kumuacha ajiendee zake.

Alipokwwisha kuachwa na wasumbufu hao ambao baadhi waliishia kumtusi,nae hakuwajali akaendelea na hamsini zake.

Miguu yake ilikoma akiwa katikati ya soko la Buzuruga.

Tumbo lilikosa ushirikiano lakini pia alihitaji kutuliza akili na kuamua jambo la kufanya wakati huo.

Alijongea katika mgahawa mmoja uliokuwa sokoni humo kisha kwa pesa kidogo aliokuwa nayo akaagiza chai ya moto na wali mweupe.

Alikula taratibu huku mawazo lukuki yakikizonga kichwa chake.

Licha ya akili yake kuuona ugumu wa kumpata Mwasu kwa siku hiyo,ila bado aliona mtu sahihi zaidi wa kumfikia ni Mwasu ili walau apate ushauri kutoka kwake na namna ataweza kuepuka masaibu yanayomzonga.

Lakini jambo moja lilimchanganya; ni vipi watu wale wamefika haraka Mwanza na pia wamewezaje kufuatilia nyendo zake kirahisi vile!?

Alijipa utulivu wa akili.

Jibu halikukawia japo hakujua kama ndilo litakuwa sahihi ama la.

Alidhani ya kwamba, watu wale wabaya walijua akifika Mwanza; Mtu wa kwanza kumtafuta atakuwa ni Mwasu na ndio mana alikuta wamemtangulia.

Alitoa kimkoba kidogo chenye ukubwa Sawa na pochi za akina dada ila hiki kilikuwa ni cha ngozi na pia kilikuwa na mikanda mirefu myembamba sana. Tofauti nyingine ni kuwa kimkoba hiki kingekuwa kinamilikiwa na wadada wa mjini basi ungekuta kimejaa vipodozi; kioo na taulo moja ya kike. Ila mkoba huu wenyewe ulikuwa na karatasi nne tu.

Karatasi hizi zilikuwa zinatokana na zao la miti hivyo hazikuwa nyeupe bali zilikuwa ni kaki.

Alitazama mazingira aliokuwapo na alipohakikisha hakuna anaejali anachokifanya,akazitoa zote.

Zilikuwa zimekunjwa kwa kuzungushwa kisha kwa juu zikabanwa na kamba nyembamba sana.

Alipokwisha kuziweka pembani karatasi zile akarudisha tena mkono kwenye mkoba ule na alipoutoa alikuwa na kadi ndogo ya kuhifadhi kumbukumbu.

Akakitazama kikadi kile kisha akayakumbuka maneno ya mtu aliempa vitu vile.

Kabla hajapewa alisisitiziwa sana kuhifadhi kadi ile kuliko karatasi, yani bora karatasi zipotee ila si kadi ile.

Lakini pia alikumbuka kuonywa ya kuwa kama anataka aendelee kuishi ni lazima awe na vitu vile huku akiambiwa kama atapokonywa basi ndipo uhai wake utakapoishia.

Akazishusha pumzi kwa mkupuo kisha akawaza kuifanyia kitu kadi ile ili awe na hakika nayo katika usalama wake na kadi ile.

Lakini wakati akikumbuka kurudia chakula mezani, wazo moja likapita kichwani mwake.

Polisi!!

Yesi aliwaza kwenda kuutua mzigo wa mateso ule kituo cha polisi. Japo aliamini anaweza kuzungushwa sana hadi kushugulikiwa,lakini aliamini ni lazima watalishugulikia kulingana na uzito wa suala lenyewe.

Akapitisha wazo la kwenda kituo cha polisi.

Alipogeukia chakula chake alikuta kimepoa na chai imegeuka kuwa maji ya baridi.

Akakimalizia kisha akalipa na kuinuka kisha akatafuta njia yenye watu wengi na kujichanganya akatoka nje ya kituo cha mabasi.
*****

Dakika ishirini badae alikuwa anatazamana na kituo cha polisi Nyakato Neshino.

Aliingia hadi mapokezi kisha akaomba kuonana na mkuu wa kituo kile.

Aliruhusiwa kumuona bila kuulizwa maswali mengi kama alivyotarajia.

“Unaitwa nani binti” aliuliza mkuu wa kituo.

“Remi” alijibu binti.

“Ndio Remi; unaishi wapi na utokea wapi” aliuliza tena mkuu wa kituo.

“Natokea Kigoma” alijibu binti.

Mkuu wa kituo akamtazama binti kwa makini sana kisha akatikisa kichwa kwa alichokiona kutoka kwa binti yule.

Mkuu wa kituo alihisi binti atakuwa na matatizo kiakili kwa sababu ya muonekano wake kuwa mchafu na anaonekana hajaoga siku kadhaa.

Hiyo huwa si kawaida ya wadada wenye urembo kama wa yule binti japo hakuwa akiuthamini urembo wake.

Mkuu wa kituo pia aliyajumlisha majibu ya binti yalivyo ya mkato kuzikamilisha hisia zake.

“Shida yako tafadhali” alisema mkuu wa kituo.

“nimepoteza wadogo zangu” alijibu binti.

“wamepoteje?”

“sijui walivyopotea ila wamepotea”

Mkuu wa kituo akaingiwa na gadhabu kwa sababu alijua kabisa binti yule hayuko sawa kiakili na pale anampotezea tu muda wake.

“Ok!!, unahisi ni nani aliefanya hivyo?” akauliza mkuu wa kituo huku akijaribu kuzizuia gadhabu zake.

“ninao ushahidi wa mwanzo huu hapa” alijibu binti huku akimpa Mkuu wa kituo karatasi nne ambazo zilionekana kabisa zimetolewa nakala kwa kirudufu muda si mrefu.

Mkuu wa kituo akazichukua karatasi zile na kuzifunua.

Akajikuta akicheka sana huku gadhabu zikimuisha na kuamini kweli binti alieyeko mbele yake ni mgonjwa wa akili.

“Dada nadhani unahitaji msaada wa haraka sana” alisema mkuu.

Remi akatabasamu kwa mara ya kwanza tangu aingie ndani ya jiji la Mwanza.

Lakini hakujua kauli ya Mkuu wa kituo haikumaanisha alivyodhani yeye.

Furaha na matarajio yake yakakoma gafla.

“sio msaada unaodhani wewe binti,msaada ninao kupa inabidi twende hospitalli ukapime akili yaezekana umekuja hapa ukiwa hujui”

E bana eeh!

Mshangao ukatamaradi usoni pa Remi huku akiona kabisa alivyodhaniwa na ukichaa tena mbele ya serikali.

Amah!!

“Afande kwanini…?” Alijikuta anakwama kuuliza.

“Remi huoni unaumwa wewe?,hivi unakujaje hapa ukiwa na karatasi zilizoandikwa kwa lugha ya kifaransa afu useme zinahusiana na upotevu wa wadogo zako?”

Jama!!

Akapagawa na hapo ndo akajua lugha iliotumika pale ni kifaransa mana tangu mwanzo alishindwa kusoma kilichopo kwa sababu hakuwa na uelewa wa lugha ile sasa hakujua ya kuwa hata hapo kituoni wapo wasiojua kifaransa kama yeye japo alishukuru walau tu kuambiwa ni kifaransa kimetumika kuziandika karatasi zile.

“anyway, nenda ofisi namba kumi ueleze shida yako vizuri kisha uwape hizi karatasi,sasa ikibainika unacheza ujinga utajuta kucheza na serikali” alisema kwa mkwara mkuu wa kituo huku akimpa Remi karatasi zake.

Remi alijua hajacheza vizuri karata yake ili aeleweke. Lakini nafsini mwake alijiambia yupo sahihi kuanza vile mana hajui ni nani yupo nyuma ya sakata lile na alijua kabisa hata serikalini wamo.

Remi hakutaka kufunguka lolote zaidi pale na ni baada ya kuhisi tangu mwanzo mazungumzo yake na mkuu yule yatakavyokuwa kwa sababu alionekana mjivuni sana bwana yule

Lakini pia hakutaka kuongea sana mana angejulikana si Mtanzania kwa lafudhi yake na hiyo ingemletea shida zaidi mana angekufa na ushahidi wake ndani ya gereza kwa kuwa mhamiaji haramu wala hakuna ambae angejua ni Mkimbizi alietoroka kwenye kambi ya wakimbizi huko Kigoma.

Ofisi namba kumi ndani ya jengo lile la kituo cha polisi ilikuwa inakaliwa na ofisa mkuu wa upelelezi katika kitengo cha makosa ya jinai na pia kilishugulika na ujasusi wa ndani.

OCCID alikuwa anatazamana na Remi na baada ya kumsikiliza maelezo yake ambayo yalikuwa sawa na aliyotoa kwa mkuu wa kituo,akazichukua karatasi zile kisha hakuzipitia akaziweka pembeni huku akimwahidi kulishugulikia swala lile kikamilifu.

Remi akaaga na kuondoka ndani ya ofisi zile na alipotoka nje alilakiwa na macho ya watu wawili tofauti.

Mmoja alikuwa ni Mtega nyoka na mwingine alikuwa ni askari wa usalama barabarani aliekuwa anaripoti kwa ajili ya kurudi nyumbani kupumzika.

Alimtizama kwa jicho lisilo la wema ila si yeyote aliejua isipokuwa ofisa yule wa usalama barabarani.

Tofauti na siku Zote ambazo ofisa yule huripoti kisha kuondoka,ila siku hiyo akabaki pale kituoni kwa dakika kadhaa, lengo ni kujua njia alizopita Remi na alifuata nini pale kituoni.

Hilo alifanikiwa mnoko yule.

*****

OCCID hakutaka kupuuzia lalamiko la Remi lakini pia hakutaka kuzipotezea karatasi zile hivyo haraka akamuita kijana mmoja kutoka kitengo cha upelelezi cha polisi (Intelligence Police) ambae anaijua lugha iliotumika pale ili ampe kazi hiyo ya kushugulikia kesi iliohusisha lugha ya kigeni.

Mwanzo hakujua kama lile ni suala kubwa sana na ndio mana alipomwita Intelligence Ofisa au maarufu ‘IO' hakuhitaji kutafsiriwa pale mana alijua itakuja kwenye ripoti atakayopewa badae.

Waswahili walisema; ‘mazoea mabaya' hilo lilidhihirika ndani ya ofisi zile za upelelezi mana hata IO alipopewa maelezo kidogo ya kesi ile na karatasi hakujihangaisha kusoma mbele ya mkubwa wake, akatoka na kwenda ofisini kwake kushugulikia baadhi ya viporo na kisha usiku akitulia aanze kupitia karatasi zile na ahsubuh aamkie kesi hiyo endapo ingekuwa na tija sana.

Hakujua yajayo!!

Hakujuwa kesho anaijua mungu pekee na hakuna binadamu aliewahi kuifikia kesho isipokuwa mauti pekee ndio hukufikisha katika ukomo wa kesho ila si mwanadamu aliehai mana kila siku ni kesho ijayo.

Hakujua! Hakujua!
 
Ivi hizi simulizi mbona zinaishiaga kitonga
 
Rip IQ

Riwaya : Mpango wa Congo

Na Bahati Mwamba

Simu: 0758573660

Hii ni sehemu ya tisa

Wakati akili ikitafakari maamuzi; macho yakanasa kitu ukutani juu kidogo ya mto na mto huo ulionekana ndio ulikuwa unatumiwa na marehemu Bulembo kwa kuwa ulikuwa unaonekana kuwa na mafuta ya nywele yaliotengeneza weusi kidogo kwa kulaliwa mara kwa mara.
Juu kidogo ya tendegu la kitanda aliona mikwaruzo, akasogea kwa hatua za aste aste na alipofikia karibu aliona maandishi ila yalikuwa ni maandishi yale yale alioyaona kwenye kikaratasi alichokitafuna wakati akiwa mikononi mwa Sajini Kebu.

Na yalikuwa yamepangiliwa vile vile kama yalivyokuwa kwenye karatasi alioitafuna.

“142BOULEVARD DU JUIN
B. P. 1612
KINSHASA CONGO (81)”

Aliyatazama tena maandishi yale, bado hakuwa amepata walau wazo la kujua Bulembo alitaka kumaanisha nini japo alijua hii ilikuwa ni anuani ya ubalozi wa Tanzania Lakini kilichomchangaya zaidi ni ile alama ya mabano kisha zikafuatia namba (81) ilimaanisha nini hii namba! Hakujua wala kufikiria mbali zaidi ya kuzidi kuchanganyikiwa na asijue afuate lipi katika anuani ile.

Honda alitoka pale kitandani, kisha akataka kutoka nje ya chumba kile lakini akasita.

Kuna sehemu alikuwa hajafikia mle ndani.

Godoro!!!

Hakuwa ameligusa kabisa lile godoro juu ya kitanda, akarudi na kulitoa shuka yake.
Macho yake yakaambulia patupu, akaamua kulitoa lote.

Aliona!

Macho yake yalikutana na karatasi nyeupe ikiwa imepachikwa kwenye kingo ya chaga,wala haikuonekana kuwekwa siku nyingi mana ilikuwa bado inamwonekano wa kuridhisha machoni.

“Ina maana alijua atakufa?” Alijiuliza Honda kisha akakichukua kikaratasi kile ambacho kilikuwa kimekatwa upande hivyo kupunguza ukubwa wake.

Akakifunua!

Kilikuwa kimeandikwa kwa mafumbo au kwa lugha ya kijasusi ‘code' lakini fumbo lilikuwa katika lugha rahisi ila ngumu kutafsirika.

Iliandikwa katika muundo wa mduara ila katika kila neno kulikuwa kuna mduara mwingine mdogo kumaanisha kila neno lilikuwa linajitegemea ila katika muunganiko mmoja.

Honda alirudia maneno yale.

“MTANZANIA X” kisha yakazungushiwa duara na ukafuata msitari ambapo ulikutana na mduara uliokuwa na neno lingine lililosomeka

“MAKANISA MATATU”

Kisha ukafuatia msitari mwingine ambapo nao ulienda kukutana na kiduara kilichokuwa na maneno

‘CLUB X'

Kisha ukafuatia mstari mwingine ulienda kuungana ni kiduara cha maneno ya kwanza.

Lakini kulikuwa na duara kubwa lililozunguka kiduara chenye muunganiko wa viduara vitatu na juu ya mduara ule kulikuwa na maneno makubwa yaliokuwa yameandikwa kwa kukolezwa.

“MPANGO WA CONGO”

Yote hayo aliyasoma kwa umakini wa hali ya juu huku akili yake ikijaribu kupambanua nini kilimanishwa kwenye mchoro ule.

hakika alipagawa!

Lakini alikumbuka pale ndani anamateka, haraka akatoka kule chumbani na kwenda chumba kingine alikokuwa amemfunga mateka wake.

Alipoingia akakuta mateka akiwa amesharejewa na fahamu.

Akamtazama kwanza!

Kisha akavuta kiti na kukaa mbele ya mateka wake.

“Mlifuata nini pale Tunde” aliuliza Honda.

“Tulikufuata wewe” alijibu mateka.

“Nani aliwatuma” Honda aliendelea kusaili.

“Mr X” alijibu mateka

Jibu la mateka lilimuinua kwenye kiti Honda,na hii ni kwa kuwa dakika chache tu katoka kuliona hilo jina X kwenye karatasi ilioachwa na Bulembo tena likiwa limesomeka mara mbili.

Mwanzo ilitanguliwa na Mtanzania kisha Club na sasa Mr.

Je X inatumika kote huko na X ndie mhusika mkuu? Sasa kama X ni mtu na ndie kiongozi, kwa nini awe mtanzania ikiwa mpango upo chini ya mtu aliewahi kusemekana kufa ila hakuwa mtanzania!?” alijiuliza Honda huku akimtizama mateka wake bila kusema lolote.

Pagumu!!!.

*****

.MWANZA TANZANIA.

Remi alibaki akiwa mgongoni mwa Mtega nyoka, mtu waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku contractors.

Hakutaka kuamini kuwa mtu mgeni yule alieingilia ugonvi wake na mtekaji angeliweza kumdhibiti mtekaji ambae yeye alijua uwezo na ukatili wake kuliko mtu yoyote aliekuwa eneo lile.

Remi aliona ni kama mtetezi wake ameingilia jambo gumu asilojua uzito wake.

Akajisogeza nyuma zaidi huku akiomba watu wazidi kuongezeka eneo lile apate wepesi wa kuchomoka pale.

Mtekaji ni kama alikuwa anazihesabu karata za Remi kichwani pake.
Hivyo wakati Remi anapiga hatua moja nyuma, tayari mtekaji alikuwa anatarajia hilo na kwa kuwa mbele yake kulikuwa na mtu tata alietokea kutibua mpango wake, hakutaka akwamishwe nae na hatimae kumkosa Remi kwa mara nyingine.

Alimchukulia poa Mtega nyoka.

Kwa kasi ya aina yake, mtu yule mrefu na mwembamba akatisha kama anataka kushambulia,ila akagairi gafla na tayari hila zake zilikuwa zimezaa matunda kwa kumtikisa kidogo Mtega nyoka.

Mtu yule akampita kwa kasi ile ile Mtega nyoka; lengo likiwa ni kumfikia Remi kabla hajatokomea tena.

Ila hakufika mbali akajikuta akipaa na kudondokea tumbo na hii ni bada ya kupigwa mtama safi na Mtega nyoka.

Mtega nyoka hakutaka kumfuata pale chini akamngoja asimame.

Mtekaji akasimama kwa mbwembwe kisha akamgeukia Mtega nyoka kwa gadhabu na kwa kuokoa muda akaenda mzimamzima
Kwa kushambulia kwa mtindo wa haraka haraka, lakini mapigo yote; Honda aliyaona vyema na kuyapangua kisha akaachia konde safi lilitua kifuani mwa mtekaji na kumyumbisha kidogo lakini halikutoa madhara makubwa.

Watu walizidi kushangilia na wengine kupiga picha za video bila kujua kitu gani hasa kinaendelea zaidi ya kuona mapigano kama muvi za Jet Lee.

Makelele na simu za watu zilizidi kumchanganya mtekaji mana hakutaka kabisa hilo litokee ila kukua kwa techonolijia na eneo walipokuwa lilirahisisha asichokitaka kitokee.

Akanesa kidogo kisha akawa kama anapeleka teke la kulia na alipoona Mtega nyoka ameingia kwenye mtego wake akaachia konde zito lililotua sawia kwenye paji la uso la Mtega nyoka.

Mtega nyoka alijikuta akiona nyota nyota na alipojaribu kufumba macho alijikuta anaambulia kuona mashilingi mengi na alipofumbua macho akaona ni kama umati wa watu unaiba shilingi alizoona.

Akagwaya!

Mtekaji alitaka kutumia nafasi ile kummaliza Mtega nyoka, lakini kabla hajatimiza lengo lake mara ukasikika mlipuko wa risasi na kuzua taharuki kwa watu waliokua pale huku kila mmoja akijaribu kuokoa uhai wake.
Mtekaji alibabaika kidogo lakini punde akasikia mvumo wa pikipiki anayoijua haraka akapiga tambo kubwa huku akikwepa konde lililotupwa na Mtega nyoka na tambo la pili lilimfikisha juu ya pikipiki huku nyuma zikisikika tena risasi kadhaa.

Mtega nyoka alishuhudia pikipiki isio kuwa na namba za usajili ikitokomea kuelekea katikati ya mji.

Jicho la Mtega nyoka likabaki likiangaza alipo binti asie jua kusoma wala asimuone.

Akah!!

“yuko wapi tena?” alijiuliza huku akianza kupiga hatua huku macho yake yakiwa yanaangaza huku na huko miongoni mwa watu waliokuwa wanakimbia milio ya risasi.

“Tulia na nyoosha mikono juu!” ilisikika sauti ya kimamlaka ikamuamuru Mtega nyoka.

Mtega nyoka aligeuka taratibu huku aking’ata meno kwa gadhabu.

Alipotulia macho yake yakakutana na mitutu miwili ya bunduki kutoka kwa askari wawili ambao aliwatambua ni waliokuwa wanalinda benki ya NMB.

“Amani afande” alisema Mtega nyoka huku akiingiza mkono mfukoni na alipotoa alikuwa na kitambulisho rasimi cha kazi yake.

Kilichofuata ni saluti kutoka kwa askari wale. Mtega nyoka hakujali saluti zao aligeuka na kujichanganya kwenye umati wa watu ulioanza kujikusanya tena huku kwa mbali akisikia king’ora cha gari la polisi kilisikika kikija eneo lile hivyo akajua askari wale watakuwa waliomba usaidizi makao makuu kwa kudhani wao ni wezi wakiwa wanapanga kuiba benki.

Itaendelea..

Nb: Nashukuru sana kwa sapoti mliooonesha leo na jana lakini pia kwa maoni yenu nami nawaahidi sitawaangusha nitafanya kadri ya uwezo wangu ili nanyi mridhike, vipande viwili kuanzia kesho vitakuwa vikiwekwa hapa...

Ambao bado mnapita kimya, tafadhalini toeni sapoti nami nipate moyo wa kuwaburudisheni..

Karibuni
shemejiiiiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom