Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Haya maoni yanawakilisha mawazo na maprndekezo ya wengi sana. Mkuu Kudo tunaomba utusaidie kwa hili
 
@kudo nitag mkuu ukidondosha kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuja mbio mbio nikujua kuna kitu kumbe hola
 
uko vizuri sana ndugu muandishi endelea kutushushia vitu kama hivi kila upatapo nafasi
 
Riwaya : Mpango wa Congo

Na Bahati Mwamba

Simu: 0758573660


Hii ni sehemu ya tisa


Wakati akili ikitafakari maamuzi; macho yakanasa kitu ukutani juu kidogo ya mto na mto huo ulionekana ndio ulikuwa unatumiwa na marehemu Bulembo kwa kuwa ulikuwa unaonekana kuwa na mafuta ya nywele yaliotengeneza weusi kidogo kwa kulaliwa mara kwa mara.
Juu kidogo ya tendegu la kitanda aliona mikwaruzo, akasogea kwa hatua za aste aste na alipofikia karibu aliona maandishi ila yalikuwa ni maandishi yale yale alioyaona kwenye kikaratasi alichokitafuna wakati akiwa mikononi mwa Sajini Kebu.

Na yalikuwa yamepangiliwa vile vile kama yalivyokuwa kwenye karatasi alioitafuna.

“142BOULEVARD DU JUIN
B. P. 1612
KINSHASA CONGO (81)”

Aliyatazama tena maandishi yale, bado hakuwa amepata walau wazo la kujua Bulembo alitaka kumaanisha nini japo alijua hii ilikuwa ni anuani ya ubalozi wa Tanzania Lakini kilichomchangaya zaidi ni ile alama ya mabano kisha zikafuatia namba (81) ilimaanisha nini hii namba! Hakujua wala kufikiria mbali zaidi ya kuzidi kuchanganyikiwa na asijue afuate lipi katika anuani ile.

Honda alitoka pale kitandani, kisha akataka kutoka nje ya chumba kile lakini akasita.

Kuna sehemu alikuwa hajafikia mle ndani.

Godoro!!!

Hakuwa ameligusa kabisa lile godoro juu ya kitanda, akarudi na kulitoa shuka yake.
Macho yake yakaambulia patupu, akaamua kulitoa lote.

Aliona!

Macho yake yalikutana na karatasi nyeupe ikiwa imepachikwa kwenye kingo ya chaga,wala haikuonekana kuwekwa siku nyingi mana ilikuwa bado inamwonekano wa kuridhisha machoni.

“Ina maana alijua atakufa?” Alijiuliza Honda kisha akakichukua kikaratasi kile ambacho kilikuwa kimekatwa upande hivyo kupunguza ukubwa wake.

Akakifunua!

Kilikuwa kimeandikwa kwa mafumbo au kwa lugha ya kijasusi ‘code' lakini fumbo lilikuwa katika lugha rahisi ila ngumu kutafsirika.

Iliandikwa katika muundo wa mduara ila katika kila neno kulikuwa kuna mduara mwingine mdogo kumaanisha kila neno lilikuwa linajitegemea ila katika muunganiko mmoja.

Honda alirudia maneno yale.

“MTANZANIA X” kisha yakazungushiwa duara na ukafuata msitari ambapo ulikutana na mduara uliokuwa na neno lingine lililosomeka

“MAKANISA MATATU”

Kisha ukafuatia msitari mwingine ambapo nao ulienda kukutana na kiduara kilichokuwa na maneno

‘CLUB X'

Kisha ukafuatia mstari mwingine ulienda kuungana ni kiduara cha maneno ya kwanza.

Lakini kulikuwa na duara kubwa lililozunguka kiduara chenye muunganiko wa viduara vitatu na juu ya mduara ule kulikuwa na maneno makubwa yaliokuwa yameandikwa kwa kukolezwa.

“MPANGO WA CONGO”

Yote hayo aliyasoma kwa umakini wa hali ya juu huku akili yake ikijaribu kupambanua nini kilimanishwa kwenye mchoro ule.

hakika alipagawa!

Lakini alikumbuka pale ndani anamateka, haraka akatoka kule chumbani na kwenda chumba kingine alikokuwa amemfunga mateka wake.

Alipoingia akakuta mateka akiwa amesharejewa na fahamu.

Akamtazama kwanza!

Kisha akavuta kiti na kukaa mbele ya mateka wake.

“Mlifuata nini pale Tunde” aliuliza Honda.

“Tulikufuata wewe” alijibu mateka.

“Nani aliwatuma” Honda aliendelea kusaili.

“Mr X” alijibu mateka

Jibu la mateka lilimuinua kwenye kiti Honda,na hii ni kwa kuwa dakika chache tu katoka kuliona hilo jina X kwenye karatasi ilioachwa na Bulembo tena likiwa limesomeka mara mbili.

Mwanzo ilitanguliwa na Mtanzania kisha Club na sasa Mr.

Je X inatumika kote huko na X ndie mhusika mkuu? Sasa kama X ni mtu na ndie kiongozi, kwa nini awe mtanzania ikiwa mpango upo chini ya mtu aliewahi kusemekana kufa ila hakuwa mtanzania!?” alijiuliza Honda huku akimtizama mateka wake bila kusema lolote.

Pagumu!!!.

*****

.MWANZA TANZANIA.

Remi alibaki akiwa mgongoni mwa Mtega nyoka, mtu waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku contractors.

Hakutaka kuamini kuwa mtu mgeni yule alieingilia ugonvi wake na mtekaji angeliweza kumdhibiti mtekaji ambae yeye alijua uwezo na ukatili wake kuliko mtu yoyote aliekuwa eneo lile.

Remi aliona ni kama mtetezi wake ameingilia jambo gumu asilojua uzito wake.

Akajisogeza nyuma zaidi huku akiomba watu wazidi kuongezeka eneo lile apate wepesi wa kuchomoka pale.

Mtekaji ni kama alikuwa anazihesabu karata za Remi kichwani pake.
Hivyo wakati Remi anapiga hatua moja nyuma, tayari mtekaji alikuwa anatarajia hilo na kwa kuwa mbele yake kulikuwa na mtu tata alietokea kutibua mpango wake, hakutaka akwamishwe nae na hatimae kumkosa Remi kwa mara nyingine.

Alimchukulia poa Mtega nyoka.

Kwa kasi ya aina yake, mtu yule mrefu na mwembamba akatisha kama anataka kushambulia,ila akagairi gafla na tayari hila zake zilikuwa zimezaa matunda kwa kumtikisa kidogo Mtega nyoka.

Mtu yule akampita kwa kasi ile ile Mtega nyoka; lengo likiwa ni kumfikia Remi kabla hajatokomea tena.

Ila hakufika mbali akajikuta akipaa na kudondokea tumbo na hii ni bada ya kupigwa mtama safi na Mtega nyoka.

Mtega nyoka hakutaka kumfuata pale chini akamngoja asimame.

Mtekaji akasimama kwa mbwembwe kisha akamgeukia Mtega nyoka kwa gadhabu na kwa kuokoa muda akaenda mzimamzima
Kwa kushambulia kwa mtindo wa haraka haraka, lakini mapigo yote; Honda aliyaona vyema na kuyapangua kisha akaachia konde safi lilitua kifuani mwa mtekaji na kumyumbisha kidogo lakini halikutoa madhara makubwa.

Watu walizidi kushangilia na wengine kupiga picha za video bila kujua kitu gani hasa kinaendelea zaidi ya kuona mapigano kama muvi za Jet Lee.

Makelele na simu za watu zilizidi kumchanganya mtekaji mana hakutaka kabisa hilo litokee ila kukua kwa techonolijia na eneo walipokuwa lilirahisisha asichokitaka kitokee.

Akanesa kidogo kisha akawa kama anapeleka teke la kulia na alipoona Mtega nyoka ameingia kwenye mtego wake akaachia konde zito lililotua sawia kwenye paji la uso la Mtega nyoka.

Mtega nyoka alijikuta akiona nyota nyota na alipojaribu kufumba macho alijikuta anaambulia kuona mashilingi mengi na alipofumbua macho akaona ni kama umati wa watu unaiba shilingi alizoona.

Akagwaya!

Mtekaji alitaka kutumia nafasi ile kummaliza Mtega nyoka, lakini kabla hajatimiza lengo lake mara ukasikika mlipuko wa risasi na kuzua taharuki kwa watu waliokua pale huku kila mmoja akijaribu kuokoa uhai wake.
Mtekaji alibabaika kidogo lakini punde akasikia mvumo wa pikipiki anayoijua haraka akapiga tambo kubwa huku akikwepa konde lililotupwa na Mtega nyoka na tambo la pili lilimfikisha juu ya pikipiki huku nyuma zikisikika tena risasi kadhaa.

Mtega nyoka alishuhudia pikipiki isio kuwa na namba za usajili ikitokomea kuelekea katikati ya mji.

Jicho la Mtega nyoka likabaki likiangaza alipo binti asie jua kusoma wala asimuone.

Akah!!

“yuko wapi tena?” alijiuliza huku akianza kupiga hatua huku macho yake yakiwa yanaangaza huku na huko miongoni mwa watu waliokuwa wanakimbia milio ya risasi.

“Tulia na nyoosha mikono juu!” ilisikika sauti ya kimamlaka ikamuamuru Mtega nyoka.

Mtega nyoka aligeuka taratibu huku aking’ata meno kwa gadhabu.

Alipotulia macho yake yakakutana na mitutu miwili ya bunduki kutoka kwa askari wawili ambao aliwatambua ni waliokuwa wanalinda benki ya NMB.

“Amani afande” alisema Mtega nyoka huku akiingiza mkono mfukoni na alipotoa alikuwa na kitambulisho rasimi cha kazi yake.

Kilichofuata ni saluti kutoka kwa askari wale. Mtega nyoka hakujali saluti zao aligeuka na kujichanganya kwenye umati wa watu ulioanza kujikusanya tena huku kwa mbali akisikia king’ora cha gari la polisi kilisikika kikija eneo lile hivyo akajua askari wale watakuwa waliomba usaidizi makao makuu kwa kudhani wao ni wezi wakiwa wanapanga kuiba benki.




Itaendelea..



Nb: Nashukuru sana kwa sapoti mliooonesha leo na jana lakini pia kwa maoni yenu nami nawaahidi sitawaangusha nitafanya kadri ya uwezo wangu ili nanyi mridhike, vipande viwili kuanzia kesho vitakuwa vikiwekwa hapa...

Ambao bado mnapita kimya, tafadhalini toeni sapoti nami nipate moyo wa kuwaburudisheni..

Karibuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…