desertambush
Senior Member
- Feb 16, 2016
- 107
- 63
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
'Usilolijua ni sawa na usiku wa giza'Naona kuna kidudu mtu kinasikilizia mazungumzo ya wakuu atajuta baadae,, ahsante Sana mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
RIWAYA : MPANGO WA CONGO.
SEHEMU YA 15
Sajini kebu akageuza macho yake kushoto kwake akakutana na jicho la Kojo ambae waliunganishwa pamoja baada ya vijana wa Kebu kuadhibiwa na Honda; hivyo sasa alikuwa ameungana na kundi la Kizibo na Kojo.
Aliona jinsi uso wa Kojo ulivyopasuka bila mpangilio.
“Umesema hii kazi ya yule bwege sio!!” aliuliza Sajini Kebu.
Swali lile lilionekana kumkera Kojo ila hakujibu akabaki kutazama pembeni.
“Bwana yule ananitesea rafiki yangu aisee” alidakia Kizibo aliekuwa amekaa kwenye kiti cha dereva.
“Hebu nipelekeni nikapumzike kwa mrembo wangu nikitoka huko risasi za kichwa zitammaliza Honda!!” alisema Sajini Kebu huku akiegemea kiti cha abiria alichokuwa amekalia.
Gari ikawashwa na kuondoka kuelekea viunga vya mji wa Gombe pembeni kidogo ya mji wa Kinshasa.
Ni kwa kuwa hawakujua lijalo halijawahi kujulikana kamwe.
Na kama walidhani wanaenda kupumzika walikosea sana.
****
Simbi Musinza alikuwa ni mshindi wa mashindano ya ulimbwende katika mji wa Kishansa kisha akaenda kushiriki mashindano ya urembo yaliokutanisha warembo kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Congo.
Bahati mbaya kwake, hakufanikiwa kufanya vizuri sana hasa baada ya wandaaji kugundua Simbi alikuwa akitumia zaidi mwili wake kushawishi wandaaji wamchague.
Ukizungumizia warembo waliotikisa katika mashindano hayo basi huwezi kumsahau Simbi ila tabia yake ya kupenda rushwa kwa kutumia mwili wake ilisababisha aangukie pua.
Licha ya kushindwa katika mashindano hayo,lakini bado jina lake na uzuri wake uliendelea kutikisa kurasa za magazeti jijini Kinshasa.
Simbi alikuwa na maisha ya kupenda anasa, kila siku lazima avinjari viwanja kadhaa waliokuwa wanapapatika na uzuri wake na umaarufu wake.
Hakuna sehemu yoyote ya anasa ambayo Simbi hakufahamika.
Katika sehemu moja ya chumba cha watu maalumu(VIP) kulikuwa kuna watu wawili wamekaa huku wakisikiliza muziki uliokuwa utoka kwenye sipika zilizokuwa zimefungwa kila kona ya chumba kile.
Mwanaume mmoja wa kizungu alikuwa amekaa huku amenyoosha miguu yake na usawa wa tumbo lake kulikuwa kuna kichwa cha mwanamke kilichokuwa kimejaa nywele bandia za gharama kubwa.
Mwanamke yule alikuwa akiperuzi mtandaoni huku mara kwa mara akicheka peke yake na mara zingine alicheka huku akimtizama usoni mwanaume wake wa kizungu.
Alikuwa ni Simbi!!
Mzungu aliendelea kumpapasa Simbi kuanzia kifuani hadi kichwani.
Ni kama Simbi hakusikia mguso wowote kutoka kwa mtu wake huyo, yeye alikuwa bize tu na kuperuzi kwenye mtandao.
Kama si upofu wa mapenzi basi Mzungu yule angekasirika kwa kutokupewa muda na Simbi.
Ila hakujali!!
Simbi akiwa bado anaperuzi, mara akaona ujumbe kwenye simu yake.
“Uko wapi!!” ulisomeka hivyo huo ujumbe kutoka kwa mtu aliekuwa amehifadhi jina lake kwa SAJINI.
Akanyanyuka gafla kisha akamtazama mzungu ambae wala hakujali yeye aliendelea kuvuta shisha tu.
Simbi alibaki ameganda bila kufanya lolote huku akijua kabisa ni nadra sana kuona lile jina linamtafuta.
Na likimtafuta basi siku hiyo anajua lazima avuliwe chupi.
Kilichomfikirisha sio kuvuliwa chupi na mmiliki wa jina lile.
la hasha!
Yeye aliwaza dau la pesa ambalo angeachiwa ahsubuhi na bwana huyo.
Dau la bwana yule huwa ni kubwa kuliko analoachiwa na mzungu.
Akawaza jibu.
“Nipo njiani naenda home” alijibu kisha akamsogelea mzungu.
“Leo unatoa ngapi kwani!!” aliuliza kwa sauti kavu huku mkono akiwa ameshika kiunoni.
Mzungu alishangaa mabadiliko ya mwenzi wake huyo.
“Kama kawaida dola mia!!” alisema Mzungu.
“Ooh ok!!” alisema Simbi.
“Kwani vipi!!” Mzungu alionesha mashaka yake.
“Hapana mpenzi, ila nimeingia kwenye mzunguko wa hedhi sasa hivi!!”
Mzungu alinywea kama kapigwa denda na kichaa.
Wakati bado Simbi anangojea kauli nyingine kutoka kwa Mzungu; mara akasikia ujumbe mwingine ukiingia kwenye simu yake.
Akaufungua!!
Aisee!
Alitamani kuivunja simu wakati huohuo na asipatikane kabisa.
Akaurudia kuusoma ujumbe ule na kuhakikisha jina la mtumaji.
Halikubadilika lilikuwa ni lile lile na ujumbe ni ule ule na ulisomeka vile vile.
“Nipo nakuja kwako Chimamy” ulisomeka hivyo na mtumaji mtu aliekuwa amemhifadhi kwa jina la CHIBABY.
Simbi alihisi kubanwa na tumbo la kuhara,haraka akakimbilia chooni.
Huko wala alichotarajia kitoke hakikutoka, isipokuwa aliongeza joto mwilini kwa mbio zilizomfikisha huko maliwatoni.
Mapigo yake ya moyo yalitaka kuzidi kipimo cha kawaida cha udundaji wake.
Akatoka maliwatoni bila kufanya lolote huko na alipomtazama mzungu wake akamwona alivyosawajika na midomo kumuanguka kama rasi alienyolewa usingizini.
Hakumjali!!
Yeye alikuwa anawaza tu namna ya kutatua fumanizi huko kwake na ukizingatia wanaume wote aliwahitaji mana mmoja alikuwa anamhonga vizuri na mwingine ndie mwanaume aliempenda sana.
Nani alisema wapenda pesa hawana moyo wa kupenda!!
Simbi hakutaka kumpoteza kabisa chibaby wake, mwanaume wa kitanzania alietokea kumgusa kila kona ya mwili wake nae akagusika,mwanaume aliejua kumwacha hoi kila walipokutana,mwanaume aliejaliwa mwili mzuri wa kiume.
Hata!!
Wote aliwahitaji.
Mwanaume mwenye pesa na mwanaume wa moyo wake.
Lazima aue fumanizi hilo kivyovyote.
Haraka akakimbilia mkoba wake na kutoka nje ya chumba kile kilichokuwa kwenye jumba kubwa la anasa ndani ya mji wa Gombe.
****
Nje ya nyumba ya Simbi kulikuwa kuna gari moja jeupe limesimama huku ndani yake kukiwa na watu watatu.
Sajini Kebu;Kizibo na Kojo.
“Komredi mi naingia kupiga pumzi kidogo,nitakaa saa tatu!!”
Alisema Sajini Kebu huku akifanya jitihada za kushuka ndani ya gari.
“Kwa hiyo sisi tunabaki kuwa walinzi wako? Aliuliza Kizibo.
“Hapana! Kama kuna anaetaka kuingia nae akapumzike kidogo twenzetuni jama” Sajini aliwaelekeza wenzie.
Kizibo na Kojo walitazamana, kisha Kizibo akazima gari na kushuka huku akimwacha Kojo akijilaza kwenye viti kumaanisha yeye atapumzika ndani ya gari.
“Unalala tena kwenye gari yule bwege atakuotea tena aisee!!” alitahadharisha Kizibo na Kojo akanyoosha bastola juu kumaanisha akitokea tu anamlipua kwa risasi kadhaa.
Kizibo na Sajini Kebu wakatasamu huku wakiliendea geti.
Kitu ambacho hawakujua ni kuwa Simbi alikuwa ndani na mwanaume mwingine na mwanaume aliekuwa ndani nae hakujua kuna mwanaume mwingine nae anakuja hapo ndani.
Wao walikuwa hawajui ila Simbi alijua na alipanga kucheza nao wote usiku mmoja.
Tatizo hakuwahi kujua wanaume wanaonenda kukutana ndani ni wanaumeume wa aina gani!!
Patamu
******
Ni fupi leo, ila heri kidogo kuliko kukosa kabisa
Tuvumiliane kwa leo
tuko pamoja shemelaUtajua tu!! Endelea kushikilia hapa hapa shemeji
Yawezekana aisee,Wasiwasi wangu ni kuwa CHIBABY ndo Honda mwenyewe...yajayo yanafurahisha tuyangoje kutoka kwa Kudo
Na hapo ndo kitimtim kitakuwa kitam zaidi. Natamani mzee baba leo atutegulie hiki kitendawili. Pia nahisi Solomon hakufa, alifanikiwa kuokolewa ili ngoma ya Mwanza nayo inogile
Halafu sitaki Solomon afe, wambea tunataka kujua kilichoandikwa kwenye karats zile ni yeye tu anajua.Na hapo ndo kitimtim kitakuwa kitam zaidi. Natamani mzee baba leo atutegulie hiki kitendawili. Pia nahisi Solomon hakufa, alifanikiwa kuokolewa ili ngoma ya Mwanza nayo inogile
Hicho ndo kinanifanya niamini hajafa, maana amebeba siri nzito ambayo kujulikana kwake kutachochea moto Tz.Halafu sitaki Solomon afe, wambea tunataka kujua kilichoandikwa kwenye karats zile ni yeye tu anajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Solomon sijui ataponea wapi, naona mtwanga mbele atakumbana na kesi hii maana anamfuatilia Remi hata hivyo inaonekana Remmy anakop zingine maana zile karatasi zilikuwa zimetolewa kopiHalafu sitaki Solomon afe, wambea tunataka kujua kilichoandikwa kwenye karats zile ni yeye tu anajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa watampataje Remy ,na Remy anavyowindwa hayuko salama kabisaSolomon sijui ataponea wapi, naona mtwanga mbele atakumbana na kesi hii maana anamfuatilia Remi hata hivyo inaonekana Remmy anakop zingine maana zile karatasi zilikuwa zimetolewa kopi