Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unikumbuke katika ufalme wakoKudo nahitaji kitabu aiseeee
Amina tuombe heri shaka toa MkuuUnikumbuke katika ufalme wako
Ukituma kwenye PDF kwa tshs 3000 inakuwa Riwaya yote?RIWAYA : MPANGO WA CONGO
SEHEMU YA 22
Kitu pekee alichokifanya usiku ule,ni kuikariri namba ya gari ile iliokuja kuwachukua makahaba ndani ya baa.
Alipenda sana kuonana na Zana ili ampashe habari za Dekuku; lakini aliamini Zana hawezi kumpa habari mana hakuonekana kujua mengi licha ya kuwa ndie alietumiwa kufuatilia watu waliohitajika nyakati walizohitaji.
Mtega nyoka alirudi D8 sehemu aliokuwa amepanga tangu aingie jijini Mwanza.
Hakupenda alale bila kuwasiliana na Mzee Kinyonga. Alihitaji msaada wa Mzee yule ili aokoe muda katika sakata lile lililojificha.
"Komredi!!" alisema Kinyonga baada ya kupokea simu.
"Bado nipo gizani,nahitaji msaada wako." Alisema Mtega nyoka.
Mzee kinyonga alinyamza kidogo.
"Sina muda,mambo mengi..Nitafutie mmliki wa hii namba T117DHJ" aliuvunja ukimya Mtega nyoka.
"Sasa au badae!!" aliuliza Kinyonga.
"Muda wowote!!" alijibu Mtega nyoka na kukata simu kisha akajitupa kitandani na kuutafuta usingizi.
****
Ahsubuhi Mtega nyoka aliamshwa na muito wa simu. Haraka akakurupuka na kwenda kuipokea.
"Mmiliki wa T117 ni Kasuku Contractors!!" ikasema sauti ya Kinyonga kisha ikakata simu bila kusubiri ama kutoa maelezo zaidi.
Mtega nyoka akabaki anashangaa mambo yale yalivyo.
"Kwanini sasa waliwaua wafanyakazi wake?" alijiuliza Mtega nyoka baada ya kukuta wafanyakazi wawili wa Kasuku Contractors wameuwawa usiku mmoja na pia Malima ambae ndie msanifu mkuu wa majengo wa kampuni ile aliwekewa mtu wa kumfuatilia na sasa gari linalotumika kusafirisha makahaba anaambiwa linamilikiwa na kampuni ya Kasuku.
"Yakoje mambo haya!!" alijiuliza tena bila kupata jibu.
"Malima!!" hilo jina likapita haraka kichwani mwake.
"Aisee yule dogo yupo hatarini!!" alijisemea Mtega nyoka huku akikimbilia makiwatoni kujiswafi haraka ili pilikapilika zianze.
Dakika kumi baadae alikuwa anamalizia kuweka silaha zake mahali alipona panafaa,lengo likiwa ni kumweka Malima kwenye himaya yake ili ajue mbivu na mbichi za kampuni anayofanyia kazi.
Lakini hakujua ya kuwa muda unaweza kukuacha njia panda kama fisi na mialiko ya sherehe mbili kwa wakati mmoja.
..
Pahali fulani ndani ya jiji la Mwanza kulikuwa na kikao cha watu watatu huku wote wakiwa hawajakaa kwenye viti licha ya kuizunguka Meza moja ambayo juu yake kulikuwa kuna karatasi nne zenye mchoro wa jengo fulani.
Watu hawa walikuwa ni Amokachi;Sukuna na Elchapo.
Wote walikuwa ni warefu na wenye miili iliojaa kimazoezi. Na kila mmoja alikuwa na bastola kiuononi, sura zao hazikuwa na furaha kabisa.
"Kwa nini mliwachoma wale mabinti?" aliuliza Elchapo ambae alionekana ndie kiongozi wa kundi lile la watu watatu.
"Kulikuwa hakuna namna kwa taarifa tuliopata ilikuwa ni lazima kuwaua wale mabinti wote!!" alijibu Amokachi.
"Taarifa ilinifikia ikisema kuna mtu anafuatilia lile gari tangu ilipotoka Tesha baa,hivyo basi tukaweka mtego wa kumnasa ila tulipata taarifa mtu yule alirudia njiani na pia tuliarifiwa na mtu wetu pale baa ya kuwa kuna kahaba mmoja alionekana akiongea na mtu mule ndani" alisema Sukuna huku akijikuna kidevu chake.
"nadhani umeona umuhimu wa sisi kufanya vile!!" aliongeza Amokachi.
Elchapo akajikuna utosini kisha akawatazama kila mmoja kwa zamu yake.
"Inabidi lifanyike jambo moja ila itahitaji ushauri wenu kwanza" Elchapo alisema huku akizungusha macho yake kwa wote wawili na alipoona wanasubiri kumsikiliza akaendelea.
"Kuna vimeo lazima viondolewe,tunaanza na afisa usalama barabarani, yule anaweza kuwa kimeo kibaya sana endapo ukifanyika uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha Solomoni Bukaba. Lakini pia inabidi na Kindo Seleman nae aondoke!"
Mshangao uliwapata wale jamaa wawili.
"imekaaje hii tena!" aliuliza Amokachi huku sasa mikono yake akiikumbata kifuani pake.
"Jamaa aliekuwa anafuatilia gari,huwezi jua kama alisoma namba za gari na kuzikariri inamana kama akiwa ni mpelelezi hiyo itamfikisha pale Kasuku Contractors na hiyo ni hatari sana kuliko sana!" alifafanua Elchapo ambae katika kundi lao alisifika kwa kuwa na mipango thabiti yenye mafanikio..
Amokachi na Sukuna walitikisa vichwa kukubaliana na wazo lile ila Sukuna akaguna kidogo tena..
"Mh!vipi sasa akiondoka si waona mchoro bado si sahihi huu!!" alisema huku akinyoosha kidole kwenye karatasi zilizokuwa mezani.
"Hapa wa kutupa majibu kamili ni Malima na hawezi kutupa majibu bila kuwa nae stoo,mana ndie alipewa kazi, sasa inaonekana inakuwa michoro miwili ambayo haijakamilika na hawawezi kumpa mchoro ukiwa nusu!" alisema tena Elchapo huku akiugeuzageuza ule mchoro uliokuwa kwenye karatasi nne mezani.
"Duh! Ila hii teka ua, teka ua itawaamsha hawa jamaa na mpango wa miaka kumi utakuwa kazi bure eti." alisema Sukuna huku dhahiri akionesha mashaka yake.
"Usiogope Mr X yupo,atatuliza hali ya hewa na tutamalizia tulipobakiza" alisema tena Elchapo huku akimpiga mgongoni Sukuna.
Waliendelea kuzungumza kuhusu mchoro wa jengo ulioko Mezani kwao.
Wakiwa wameshakubaliana na mambo kadhaa ndipo Amokachi alikumbushia jambo.
"Vipi kuhusu Kasuku!!"
"Nani; Remi ama!!" alihoji Elchapo ili kupata uhakika.
"Ndio" akajibu Amokachi
"Huyo nimeambiwa mipango ipo sawia na muda wowote anatia timu himayani" alijibu Sukuna.
Amokachi alifyonza.
"Pimbi yule atanikoma nikimuona machoni pangu walahi"
Hakuna aliemjibu wote wakakaa kimya kwa muda kisha Elchapo akasema.
" Nadhani tuanze na vimeo vyote,kisha tutamalizia na Malima na Remi!!"
Wote waliafiki kwa vichwa vyao huku kila mmoja akijua kitengo chake kinahusika na lipi.
****
Mtega nyoka alitoka nje ya nyumba ya wageni aliolala huku akiwa hajui yaliondelea.
Akaanza kutembea taratibu tu huku akipishana na watu kadhaa waliokuwa wakiwahi kwenye shuguli zao mbalimbali za kujiingizia kipato.
Macho yake yalivutiwa na kundi la watu lililokuwa likipigana vikumbo kwenye kibanda cha muuza magazeti hatua kadhaa kutoka alipokuwa.
Akataka kupotezea ili awahi anakoenda ila akajikuta tu anashawishika kusogea pale kibandani.
Macho yakanasa vichwa vya habari vya magazeti yaliokuwa yamebandikwa Kwenye wavu.
"MWANZA YANUKA DAMU; BASI LAWAKA MOTO USIKU; USIKU WA BALAA WAACHA SINTOFAHAMU MWANZA; GARI LA POLISI LAUA WATATU....." karibia magazeti yote yalizungumzia matukio yaliotokea Mwanza siku hiyo.
Mtega nyoka akavuta hatua na kumwendea muuza gazeti na akanunua moja na kukaa pembeni kusoma.
Hapo ndipo alipojikuta njia panda.
Ni baada ya kusoma tukio la kuungua kwa gari lenye namba za usajili T117DHJ kisha kuripotiwa kuuwa watu kumi wakiokuwamo.
"Wanapoteza ushahidi nyoka hawa!!" ni baada ya kukumbuka idadi ya makahaba walioondoka na lile gari kuwa walikuwa ni kumi tu na ndio waliopatwa na umauti.
"Dereva yu wapi?" alijiuliza Mtega nyoka huku akifunua ukurasa mwingine, na hapo aliganda kama sanamu bila kupepesa macho kwa zaidi ya dakika moja.
Alikuwa anatazama picha ya binti aliekuwa amechafuka mavazi yake na hakuwa mwingine ni yule yule binti aliekutana nae ndani ya Ofisi za Kasuku Contractors kisha kituo cha polisi na sasa anamuona akiwa amepata ajali na akiwa na polisi.
Aliposoma zaidi akagundua majeruhi wote walikimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.
Lakini pia kulikuwa kuna taarifa ya kuungua kwa nyumba ya afisa wa jeshi la polisi Langolango.
Alivutiwa na kumwona Remi ili ajue kipi kinamsibu.
Akapanga kwenda kituo walicholazwa majeruhi wa ajali ile.
.
Lakini akakumbuka jina la Malima.
Wote muhimu, amfuate nani sasa.
Akabaki njia panda.
*****
Nb: kuanzia kesho wale wanaopenda kuinunua itakuwa inapatikana kwa PDF na email kwa wale wasiopenda kutoa namba za simu.
Riwaya hii itapatikana kwa Tsh 3000/= huku ikiambatana na riwaya zingine tatu utakazochagua kati ya hizi
.OPERESHENI JICHO LA PAKA
.DAKIKA ZA MWISHO
.MBWA WA GETI
.UKURASA WA GAIDI
.SAUTI YA MTUTU 1&2
.KIKOSI CHA PILI
riwaya zote hizo ni za kijasusi.Na pia ukiihitaji yenyewe kama yenyewe unalipa Tsh 2000/= tu.
Kitabu cha riwaya hii kinachapishwa awamu ya pili baada ya ile ya kwanza kumalizika mikoa yote kilichokuwapo na kitapatikana tena mwezi huu mwishoni kwa Tsh 10000/=.
Namba ya malipo ni 0758573660. Jina Bahati Mwamba.
Ieleweke kwamba hapa itaendelea kila tukipata muda bila kukatishwa panapo majaliwa.
Ahsanteni
Inamaana namba uliyotoa ni ya kulipia pesa pekee, ila PDF inatumwa huku huku JF kupitia PM? Ama unatumiwa Whatsapp?Ndio
Soma maelezo Chief!Inamaana namba uliyotoa ni ya kulipia pesa pekee, ila PDF inatumwa huku huku JF kupitia PM? Ama unatumiwa Whatsapp?
Soma maelezo Chief!
Nimesema natuma kwa njia mbili emails na Whatsapp
Ukishalipa nambie nikutumie kwa njia ipi kati ya hizo
AfadhaliAmina tuombe heri shaka toa Mkuu
Zipo kwenye orodha mwisho wa sehemu ya 21
Chagua ambayo jina litakuvutia
Mkuu bado haujamuona Kudo, maana sasa hii bure imekuwa aghari mno, per week epsode moja inaweza ikafika mwez wa sita story haijaishaAmina tuombe heri shaka toa Mkuu