Kwa kufuata mfumo uliopo, vyombo vyote vya dola vinatakiwa viwe na uwezo na ufahamu wa kushughulikia mambo haya. Lakini hali halisi ya vyombo vyetu inasikitisha wakati mwingine.
- Polisi wengi ngazi za chini wakipata taarifa hiyo wataanza kufikiria watapataje rushwa kwake na waendelee kumdai kila wakiishiwa. Yanaonyeshwa kila mara, kwani majambazi wengi wana mtandao wao na BAADHI ya polisi wetu. Sasa hii inaweza msitua Jasusi akaingia gizani au hata akahamishwa.
- Ukitumia kitengo kisicho na utaalamu wa kutosha vilevile, inaweza mrusha ndege wetu tusimwone tena.
Ushauri
Nikianza na angalizo, jasusi hasa hatakwenda kufanya kazi yake kijijini, hivyo uwezekano wa kuwa huko ni mdogo. Kama hii ni kweli basi atakuwa mahali ambapo kuna vyombo vya ngazi nzuri tu ya kutoa taarifa (kama Mkuu Kibunago alivyoshauri)
Ushauri
- Mahali mwafaka ni ofisi za DSO (District Security Officer) zipo ofisi zote za wilaya, RSO, ofisi zote za mikoa. Usikatishwe tamaa na maswali utakayoulizwa na vipingamizi utakavyo wekewa kwani ndio usalama wenyewe huo, sema na tenda kwa uhakika watalifanyia kazi.
- Vituo vikubwa vya Polisi, mahali kwenye OCD/RPC waliotulia (wako ambao nao wapo kutuliza fujo kwa nguzi/misuli, watamrusha ndege wetu) wape taarifa za uhakika, kwa ufasaha ili wajue waanzie wapi na vipi.
- Ni vyema kutoa taarifa kwa mtu mmoja tu, akiwa pekee na taarifa ziwe kamili, kama vile umemwona wapi, kama anaishi au huonekana hapo, alama zipi ulihisi zinaashiria ujasusi, tahadhari gani ulichukua n.k. Yote ni kufanya mtu unayempa taarifa awe na nondo za kutosha kukuamini, la sivyo itakuwa mambo ya mnigeria wa marekani juzi.
- Wewe mwenyewe endelea kumfuatilia kwa uangalifu, maana (kama alivyosema Mlango wa Gunia na Renegade) jasusi mzuri na mkubwa atakutambua haraka na ni hatari, waweza hata poteza maisha yako.
Mwisho, Hiongera kwa kuwa Mtanzania mzalendo halisi na tunaomba wananchi wote tuwe hivyo, maana usalama wetu uko mikononi mwetu, na vyombo vyetu vinahitaji msaada wetu, kwani sisi ndio tunaishi na wote hao.