JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

Hebu niunganishe nao mimi fasta mkuu. Nina sababu mbili za kujiunga nao haraka
1. Kwenye mifumo ya aina hiyo ya upigaji kama ya upatu vile kama ilivyokuwa DECI wewe wekeza haraka haraka mapema kabisa mwanzo mwanzo. Tena weka hela ndefu ndefu,vuna vuna fasta fasta halafu shtuka kaa pembeni na pesa yako ndefu uliyovuna mara 3 mpaka 4 ya mtaji wako
2. Ukiwa muoga kila wakati huwezi kufanikiwa. Risk takers mara zote ndio zinazotusua

Tamaa ya pesa huijui vizuri, leo utavuna kesho utapanda zaidi ili uvune zaidi.

Ukitaka kujiweka pembeni tamaa zinakutuma weka tena upige za mwisho, ghafla akaunti imezuiwa kwa uchunguzi!!
 
Tamaa ya pesa huijui vizuri, leo utavuna kesho utapanda zaidi ili uvune zaidi.

Ukitaka kujiweka pembeni tamaa zinakutuma weka tena upige za mwisho, ghafla akaunti imezuiwa kwa uchunguzi!!
Kwa mtindo kama huo usijaribu kuwa na tamaa. Kitakachokuzuia kuwa na tamaa ni ksbb tayari unajua unachokifanya,tofauti na ile tamaa ya kutokujua. Piga hela mara isizidi mara mbili ndefu ndefu,sepa zako,sahau kabisa kuhusu kuwepo kwa hiyo kampuni,yaani hukuwahi hukuwahi hata kuisogelea.
 
Hebu niunganishe nao mimi fasta mkuu. Nina sababu mbili za kujiunga nao haraka
1. Kwenye mifumo ya aina hiyo ya upigaji kama ya upatu vile kama ilivyokuwa DECI wewe wekeza haraka haraka mapema kabisa mwanzo mwanzo. Tena weka hela ndefu ndefu,vuna vuna fasta fasta halafu shtuka kaa pembeni na pesa yako ndefu uliyovuna mara 3 mpaka 4 ya mtaji wako
2. Ukiwa muoga kila wakati huwezi kufanikiwa. Risk takers mara zote ndio zinazotusua
Ingia play store download app yao inaitwa jatu
 
Unajua soko la wenye kiu ya kutapeliwa ni kubwa. Utapeli wa aina na aina hautakaa ukaisha kama wenye nyota ya kutapeliwa wapo!! HAKUNA MTU WA KUKUZALISHIA FEDHA. amka wewe KENGE!!
 
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika

Kwann wasilime wenyewe😁😁
 
Kuna mtu anajiita JATU na yeye ana model kama ya Mr kuku, ile ya kwamba toa pesa ulimiwe na uvuniwe.

Huyu JATU kawavuta watu wengi sana mara mashamba Kitetto mara Morogoro.

Model anayo tumia ni ya upatu ni Pyramid ambapo watu wa mwanzo hufaidika ili kuvuta watu wa mwesho ambao huja kuwa victim.

Hawa watu huwa kujitangaza sana ndo jadi yao, kufanya mikutano kwenye hoteli kubwa kubwa ndo jadi yao ila zote hizo huwa ni mbinu za kuvuta watu waingie wapigwe pesa.

Kama JATU anaona kilimo kinalipa kwa nini asiingie akalima pekee akapiga pesa? Kwa nini asichukue mkopo alime huko kiteto apige pesa? Mbona Summury analima pekee yake huko kwao Sumbawanga?

Watu wawe makini na hizi Pyramidi za kwamba toa pesa ulimiwe. Kwa nini asilime yeye?

Mboma MO hawaiti watu wakalime katani huko Tanga? au mbona Interchick hawaambii watu waende wafuge wote kuku?

Jamani tujizidishe Watanzania tunapigwa kirahisi sana.
Watanzania wengi walemavu wa akili. Hutaka vitu vifanyike bila wao kula gharama, so wengi huishia kugharamika mara mbili.
 
Kwani wana tofauti gani na hizo wanazoambiwa Watu watoe mia tano waboreshewe maisha?, mwisho anachaguliwa mmoja anapewa kiasi kadhaa mnaambiwa mtoe tena mia tano msichoke.

Kuhusu sisi wenye mamlaka si kwamba hatuoni, ni makusanyo tu yakifikia mahali tunaingia zinaingia mfuko mkuu...si unajua kuwa huwa haturudishi kwa Wahanga.
 
Ofisi zao Jatu PLC ziko jengo la PSSSF lililokuwa PPF House makao makuu. Ni makutano ya Barabara ya Morogoro na Samora. Story zao ni too sweet to be sour. Walinipa somo bahati mbaya wakanikuta ninaelewa mno na niliwapa challenge sana wakakosa majibu ya msingi. Nikajua iko siku watu watalizwa.
 
Kuchukua Offisi pale ni mitego mkuu ni kama wale wa Network Marketing huwa wanafanyia mikutano yao kwenye mahoteli makubwa ili msiwashitukie

Hiyo ndiyo strategy za wapigaji mkuu. Nakumbuka kuna boss wangu mmoja alikuwa anafanya kazi one of the Regional banks na alikuwa stationed huko West Africa. Nakuambia walikuja matapeli na suti zao tena wanakaa conference ya Bank. Hahahaha. Kuja kushtuka alishapigwa dollar za maana.
 
Hii Jatu si ndio hii iliyosajiliwa kwenye soko la hisa la hapa bongo (DSE) au sio hii inayojadiliwa hapa???
 
Hii Jatu si ndio hii iliyosajiliwa kwenye soko la hisa la hapa bongo (DSE) au sio hii inayojadiliwa hapa???
Huko DSE tayari kuna notice nimeona website yao, suspension ya mauzo ya hisa za JATU.
Tuendelee kutizama, watatangaza faida kwenye financial statements zao.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom