Javier Hernandez (Chicharito) kurudi Uingereza

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Klabu ya West Ham wanakaribia kufanikiwa kumnunua mshambuliaji wa Mexico, Javier Hernandez kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Klabu hiyo ina matumaini makubwa ya kufanikiwa kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, 29, ingawa kufikia sasa hawajakamilisha makubaliano kuhusu bei yake.

Mwezi Mei mchezaji, Hernandez – maarufu kwa jina la utani la Chicharito, aliibuka kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Mexico katika historia baada ya kufunga bao lake la 47.

Hernandez alifunga mabao 59 katika mechi 156 alizochezea United tangu alipotua Old Trafford mwaka 2010, kabla ya kuhamia Leverkusen kwa pauni milioni 7.3 mwezi Agosti 2015 na kuifungia klabu hiyo ya Ujerumani jumla ya mabao 39 katika michezo 76.

Na mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu hiyo katika saa 48 zijazo baada ya West Ham kuafikiana na Stoke City.

West Ham walikuwa wamewasilisha dau mara mbili zikikataliwa lakini sasa inaarifiwa Stoke wamekubali dau la karibu pauni milioni 24.

Arnautovic, 28, alijiunga na Stoke kutoka Werder Bremen miaka minne iliyopita na alikuwa ametumikia miezi 12 pekee mkataba wake wa sasa wa miaka minne klabu hiyo.

Alifunga mabao saba katika mechi 35 alizocheza mashindano yote msimu uliopita.

West Ham pia walifanikiwa kumsajili kipa wa Uingereza anayechezea Manchester City, Joe Hart kwa mkopo wa mwaka mmoja siku ya Jumanne.

Chanzo: Bongo5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…