Javier Tebas anaharibu mpira wetu aondolewe

uwe hodari

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
4,045
Reaction score
8,608
Huyu mzee kila siku kuipendelea Real madrid,chuki kibao kwa barcelona na kuzusha uongo kila uchao dhidi ya barcelona

Ameipakazia barcelona ilikuwa inawalainisha waamuzi kitu ambacho ni cha kipuuzi kabisa,inajulikana wazi Real madrid ndio amekuwa akipata faida na waamuzi katika historia ya laliga

Alichangia pakubwa kusababisha Leo Messi aondoke laliga akushirikana na yule fisadi mwenzie Bart

Alitambulisha sera mbaya kuhusu usajili na mishahara ndani ya laliga

Na hivi majuzi ametia doa kuhusu bwana mdogo Gavi juu ya maswali ya mkataba

Amesababisha Laliga imepungukiwa msimumuko
Imefikia hatua El classico inachezwa mapema ili watu wastream wengi lkn bado watazamaji wameshuka tofauti na zamani mechi usiku lkn ndio mechi iliyokuwa unatazanwa zaidi

Mechi ya manchester united vs barcelona ndio ilikuwa na watazamaji wengi kuliko el classico

Nasema hivi huyu Rais aondoke kwa maslahi mapana ya mpira wetu na watu wa dunia

Tebas siku zako zinahesabika
 
Laliga inataka kufanana na ligi1 isiyokuwa na msimumko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…