Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania

We

Kwakuwa jambo lilipendekezwa na kukubaliwa na Baraza la mawaziri, likalitishwa na ofisi ya mwansheria mkuu wa serkali ,likapitishwa na Bunge Kisha CCM wakalipitisha pia Kama chama Basi kinachoendelea ni kelele tu.

USSR
Weeeeeee SEMA kweli
 
Mimi sizunguki! Mleta mada ndo aliyepuyanga

Hivi zile falme zote ya UAE zisilalamike Dubai kuingia mkataba na Tanzania nyie wamatombo ndo mlalamike muwe na hoja?

Sicilia nikwambie kwa Mujibu wa Katiba ya UAE, Falme saba zinazounda UAE zinaweza kuingia makubaliano na nchi nyingine.

Ndo mana hizo kelele za Dubai kuingia makubaliano na Tanzania huzisikii UAE unazisikia kwa wajinga wapotoshaji waliopo hapa Tanzania
 
Nimefanya utafiti wangu ndo mana nikaja na ilo swali.

Fanya utafiti wako then Jibu swali langu kama lilivyoulizwa!
Huo utafiti wako umeufanyia wapi nasi tukapaone huko ulipofanyia? Siku zote maeneo ya utafiti sio siri, pataje.
 
Lord anazingua. Yani mikataba ya uwekezaji wa rasilimali anachukulia poa wenzetu kwenye IGA wanakuwa makini kweli kweli. Yani Marekani aingie mkataba wa kuchimba mafuta na Kuwait halafu lije li document la IGA halijaainisha mgawanyo wa mapato eti litategemea HGAs? Sisi watanzania ni wajinga sana.
 
Jana usiku nilikuwa wa kwanza kuona uzi, nikaandika nikafuta, nikaandika tena nikafuta.
Wewe,Mama Amon hebu nitafute kwa haraka sana!
 
El Elewa swali ndo ulijibu sio kupuyanga kama mleta mada ambaye amepuyanga ila mwisho kajisahau kasema ukweli kuwa shida kwake ni Waarabu tu
 
Hawawezi kupiga kelele maana kwenye mkataba wametutafuna mpaka mifupa. Yani mtu mpaka umebadili sheria zako ili kumlinda aanze kulalamika? Kwenye mkataba kuna sehemu wameandika kuwa Tanzania italazimika kulinda haki zote za maslahi ya Dubai Ports ama kampuni nyingine itakayopendekezwa na Dibai ports! Halafu unataka walalamike? Yani wana uwezo wa kuamua Kariakoo iwe maegesho yao (Kwa mujibu wa mkataba) na serikali ya Tanzania (Sijui ni serikali ipi?) Inatakiwa kuhakikisha hilo linafanyika. Bado kwa haya unataka walalamike?

Hivi unajua kuwa kwa mujibu wa IGA Dubai Ports amepewa mamlaka kisheria kuingiza chochote nchini ili mradi kitwe relevant company na kifanye kazi popote pale? Unaona hilo ni sawa? Aisee Samia kazingua! Kaiuza Tanganyika na mbaya zaidi matamshi yaliyotamkwa kwenye mkataba kiujanja ujanja yanaiondoa Zanzibar
 
Wametutafunaje? Sheria gani iliyobadilishwa as we speak now?
 
Wametutafunaje? Sheria gani iliyobadilishwa as we speak now?
Mwaka 2019 tulibadili sheria kuzuia mikataba yetu tunayoingia na foreigners kutumia sheria za nchi nyingine. Leo tunaingia mkataba na DP World halafu tunaambiwa utaongozwa na sheria za Uingereza! Hapo kimsingi tumefanya nini?

Kuhusu kututafuna nimekwambia kwenye vipengele vyote vya mkataba kuna mautata makubwa sana. Nimekupa tu mfano mmoja kwamba Dubai Ports amepewa mamlaka ya kufanya kazi na kampuni yoyote aliyopendekeza yeye ifanye kazi yoyote ndani ya eneo lolote la Tanzania na serikali inayoitwa ya Tanzania imepewa ulazima wa kuhakikisha maslahi ya Dp world na hiyo kampuni aliyopendekeza yanalindwa. Umewahi kuona wapi nchi nyingine duniani inakuwa na mkataba wa kijinga hivyo? Yani hata Somalia haiwezi kufanya ujinga wa aina hiyo! Je hapo hawajatutafuna mpaka mifupa?

Kwanza nikuulize. Ule mkataba umeusoma? Tusije kuwa tunabishania kitu na hukijui
 
Mmm wauza nchi mmekaza Fuvu
 
Moja wapo ndo iliyosababisha uzi wangu kutopata jibu hadi muda huu tangu jana
Nondo za kutunga hizi ndio unasema hazijapata majibu, nondo zisizo na authority wala mifano yoyote toka kwako unayejiita mwanasheria!.

Kama ungekuwa na nondo kweli, ungeweza kujibu kila swali uliloulizwa hapa, badala yake unakimbia tu..

Bado utuambie, ni sheria/taratibu ipi duniani inayotaka IGA zote zinazoingiwa zisiwe na vipengele vya mgawanyo wa mapato, na kiasi cha uwekezaji, kisa mbele ya safari kuna HGA?
 
Hata kama mimi sio Mwanasheria; Lakini kama makubaliano yanatakiwa kuwa hivi..., Na ni haya haya Makubaliano ya Hivi ambayo yamelifikisha Taifa hapa na ndio yaliyotumika developed countries kuwa superior na underdeveloped inferior...

Sihitaji kuwa Rocket Scientist kusema makubaliano ya hivyo hata kama ndio utaratibu hayafai....

Na ninaendelea na RAI yangu Mikataba hii mikubwa inayohusu maslahi ya nchi iwe wazi na kwa kuanzia ile yote iliyofanywa na Samia kuanzi USA mpaka Europe iletwe ili sisi wadau tuione - Tena itafsiriwe kwa kiswahili kila mwenye macho aone kama vile Katiba ilivyo wazi
 
Tumieni lugha ya kiswahili, binafsi naelewa, bt jitahidi kutafsiri Ili Elimu iwafikie Watanzania wote.

Prof A. K. A Mama Amon mwenye Uzi wake, ruksa kutumia lugha zote, tutatafsiri🙏🙏🙏
 
Umeuliza swali sahihi, ila nadhani wengi hawajakuelewa. Wanafanya kama ambavyo wewe ulikuwa unafahanya mwanzoni kabisa nilipokuwa najaribu kuwaeleza wewe wenzako kwamba hii IGA ni sawa na BIT. Nafurahi sana kwamba umetambua huu ukweli.

Sasa nirudi kwenye swali lako. Duniani kuna mikataba mingi sana ya kimataifa ya uwekezaji ambayo inazungumzia kiwango cha uwekezaji na kutoa muda wa uwekezaji. Mingi huwa ni ile ya kisekta (Sectoral Treaties) ambayo huwa inazungumzi uwekezaji kwenye sekta moja tu, kama bandari au reli, na inakuwa imeshawataja kabisa wawekezaji watakuwa ni kina nani.

Ila kubwa ambalo unatakiwa kufahamu ni kwamba, BITs na IGAs zimekuja miaka ya kuanzia 1950's hadi kufika leo. Kabla ya hapo kulikuwa na mikataba iitwayo FCN (Friendship, Commerce and Navigation Treaties) ambayo mataifa kama Marekani yalisaini sana kabla ya kuanza kutumia BITs na IGAs. Mikataba hii huweza kuwa na vipengele ambavyo vinazungumzia kiwango cha uwekezaji, japo siyo lazima iwe hivyo.

Sasa nirudi kwenye swali lako ndugu msomi. Ndiyo duniani leo kuna IGAs/BITs/MITs ambazo zinaweka vipengele vya kiasi vya uwekezaji na hata muda. Mfano mzuri ni IGA baina ya Ufaransa na Uingereza kutengeneza The Channel Tunnel Railway. Mfano mwingine ni mkataba wa uwekezaji wa nchi za Ulaya uitwao, The Energy Charter Treaty ambao unaruhusu kufanyiwa marekisho na kuhuishwa kupitia mkataba mdogo (It's a Protocol Ridden Treaty). Mfano wa mwisho kabisa ni mkataba wa uwekezaji na biashara baina ya Marekani, Canada na Mexico almaarufu kama NAFTA, ambao una Ibara zaidi ya 1000 ambazo zimasema mambo mengi sana vikiwemo viwango.

Jambo la muhimu kukumbuka ni kwamba siku hizi mataifa mengi yanaacha kutumia BITs na IGAs kwasababu, mikataba mingi ya uwekezaji inaanza kutekelezwa katika ngazi za kikanda, chini ya jumuiya za kiuchumi (Regional Intergrations) kama EU au EAC. Hivyo, mikataba inakuwa inazungumzia biashara ya kimataifa (International Trade), uwekezaji (Investment) na hata biashara nyingine (Commerce). Ndani yake utakuja kabisa wameamua kuweka vipengele vya mchanganua, na vikokotoo vyake kwa wanachama wote. It's a drafting style that makes a difference.

Msomi, watanzania wenzetu wakiwa wanauliza maswali kama haya ambayo yanahitaji utaalamu hatutakiwi kuwashambulia wala kuwabagaza, bali kuwaelekeza. Nchi hii ni yetu sote, na ni wajibu wa kila mtanzania kusema anapoona jambo limejaa ukakasi.
 
Kaka unatatizo sasa kisa mwenzio kala nya basi nawe uletu! kama uwekezaji hauoneshi kiwango unawekeza nini sasa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…