Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania

Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania

Nondo za kutunga hizi ndio unasema hazijapata majibu!.

Kama ungekuwa na nondo kweli, ungeweza kujibu kila swali uliloulizwa hapa, badala yake umekimbia tu..

Bado utuambie, ni sheria ipi duniani inayotaka IGA zote zinazoingiwa zisiwe na vipengele vya mgawanyo wa mapato, na kiasi cha uwekezaji?
Hilo boya achana nalo. Halijui kama IGA inaweza kuleta vita kati ya nchi na nchi kama imeingiwa kijinga! Kama hii ya kwetu ni Rubbish takataka la dampo. Wajinga hawajui kuwa kwa mujibu wa mkataba Samia ameuza Tanganyika yote mpaka Air space yake kwa DP World. Hayaelewi na yanacheka kuunga mkono.
 
El
Elewa swali ndo ulijibu sio kupuyanga kama mleta mada ambaye amepuyanga ila mwisho kajisahau kasema ukweli kuwa shida kwake ni Waarabu tu

Swali tumelielewa na kulijibu kikamilifu, lakini wewe ndio huelewi majibu. Ni hivi:

1. A Framework Contract (FC) is an abstract contract between two parties, which can be between two governments, between a government and a non-government, or between two between two non-governments.

2. A framework contract between governments is called an Intergovernmental agreement (IGA) aka Heads of States Agreement (HSA). aka Bilateral International Treaty (BIT)

3. An example of Framework Contract between Vodacom and HELIOS is a FC between two non-governments, which exemplifies a FC between two governments, which exemplifies an IGA, which exemplifies a BIT.

4. So, the IGA/BIT example you requested has been given.

What else do you want?
 
IGA ya Italia na Algeria mwaka 2022 kwenye masuala ya nishati iliwekwa wazi kwamba Italia wangwekeza $4billions kwenye mashirikiano hayo.

Unauliza swali la kitoto sana, hata watu kukujibu wanaona uvivu. Kuna malaki ya IGA dunia na wewe sio ajabu hujawahi kuona hata zaidi ya tatu, halafu IGA za uwekezaji haziwezi kuwa sawa na za utamaduni, sheria, mazingira n.k
Ubarikiwe🙏🙏🙏🙏
 
Nimefanya utafiti wangu ndo mana nikaja na ilo swali.

Fanya utafiti wako then Jibu swali langu kama lilivyoulizwa!

Back to basics:

1. A Framework Contract (FC) is an abstract contract between two parties, which can be between two governments, between a government and a non-government, or between two between two non-governments.

2. A framework contract between governments is called an Intergovernmental agreement (IGA) aka Heads of States Agreement (HSA). aka Bilateral International Treaty (BIT)

3. An example of Framework Contract between Vodacom and HELIOS is a FC between two non-governments, which exemplifies a FC between two governments, which exemplifies an IGA, which exemplifies a BIT.

4. So, the IGA/BIT example you requested has been given.

What else do you want?
 
Umeuliza swali sahihi, ila nadhani wengi hawajakuelewa. Wanafanya kama ambavyo wewe ulikuwa unafahanya mwanzoni kabisa nilipokuwa najaribu kuwaeleza wewe wenzako kwamba hii IGA ni sawa na BIT. Nafurahi sana kwamba umetambua huu ukweli.

Sasa nirudi kwenye swali lako. Duniani kuna mikataba mingi sana ya kimataifa ya uwekezaji ambayo inazungumzia kiwango cha uwekezaji na kutoa muda wa uwekezaji. Mingi huwa ni ile ya kisekta (Sectoral Treaties) ambayo huwa inazungumzi uwekezaji kwenye sekta moja tu, kama bandari au reli.

Ila kubwa ambalo unatakiwa kufahamu ni kwamba, BITs na IGAs zimekuja miaka ya kuanzia 1950's hadi kufika leo. Kabla ya hapo kulikuwa na mikataba iitwayo FCN (Friendship, Commerce and Navigation Treaties) ambayo mataifa kama Marekani yalisaini sana kabla ya kuanza kutumia BITs na IGAs. Mikataba hii huwezi kuwa na vipengele ambavyo vinazungumzia kiwango cha uwekezaji, japo siyo lazima iwe hivyo.

Sasa nirudi kwenye swali lako ndugu msomi. Ndiyo duniani leo kuna IGAs/BITs/MITs ambazo zinaweka vipengele vya kiasi vya uwekezaji. Mfano mzuri ni IGA baina ya Ufaransa na Uingereza kutengeneza The Channel Tunnel Railway. Mfano mwingine ni mkataba wa uwekezaji wa nchi za Ulaya uitwao, The Energy Charter Treaty ambao unaruhusu kufanyiwa marekisho na kuhuishwa kupitia mkataba mdogo (It's a Protocol Ridden Treaty). Mfano wa mwisho kabisa ni mkataba wa uwekezaji na biashara baina ya Marekani, Canada na Mexico almaarufu kama NAFTA, ambao una Ibara zaidi ya 1000 ambazo zimasema mambo mengi sana.

Jambo la muhimu kukumbuka ni kwamba siku hizi mataifa mengi yanaacha kutumia BITs na IGAs kwasababu, mikataba mingi ya uwekezaji inaanza kutekelezwa katika ngazi za kikanda, chini ya jumuiya za kiuchumi (Regional Intergrations) kama EU au EAC. Hivyo, mikataba inakuwa inazungumzia biashara ya kimataifa (International Trade), uwekezaji (Investment) na hata biashara nyingine (Commerce). Ndani yake utakuja kabisa wameamua kuweka vipengele vya faida kwa wanachama wote. It's a drafting style that makes a difference.

Msomi, watanzania wenzetu wakiwa wanauliza maswali kama haya ambayo yanahitaji utaalamu hatutakiwi kuwashambulia wala kuwabagaza, bali kuwalekeza. Nchi hii ni yetu sote, na ni wajibu wa kila mtanzania kusema anapoona jambo limejaa ukakasi.
Swali lake lilieleweka vizuri, tatizo lake hakuwa na authority yoyote ya maana kuthibitisha kile alichokuwa akisimamia, hakuwa hata na mifano ya IGA iliyoingiwa bila hivyo vipengele anavyodai, vikapelekwa HGA, yeye akawa anaimba tu.

Ndio maana kila akiulizwa kwanini kila IGA isiwe na hivyo vipengele, kama cha mgawanyo wa mapato, lazima viende HGA, is it a worldwide rule? if yes aseme inaitwaje, anakosa majibu.

Hapo kwenye hiyo mifano mitatu uliyompa ya hiyo mikataba, umemaliza mjadala wake, naamini sasa ameondoa ujinga kichwani mwake, na yupo mwingine akaomba kuchukua sehemu ya ujinga wake, ili akatengeneze ujinga mwingine Pascal Mayalla msitujazie server ya JF kwa ujinga wenu.
 
Mwaka 2019 tulibadili sheria kuzuia mikataba yetu tunayoingia na foreigners kutumia sheria za nchi nyingine. Leo tunaingia mkataba na DP World halafu tunaambiwa utaongozwa na sheria za Uingereza! Hapo kimsingi tumefanya nini?

Kuhusu kututafuna nimekwambia kwenye vipengele vyote vya mkataba kuna mautata makubwa sana. Nimekupa tu mfano mmoja kwamba Dubai Ports amepewa mamlaka ya kufanya kazi na kampuni yoyote aliyopendekeza yeye ifanye kazi yoyote ndani ya eneo lolote la Tanzania na serikali inayoitwa ya Tanzania imepewa ulazima wa kuhakikisha maslahi ya Dp world na hiyo kampuni aliyopendekeza yanalindwa. Umewahi kuona wapi nchi nyingine duniani inakuwa na mkataba wa kijinga hivyo? Yani hata Somalia haiwezi kufanya ujinga wa aina hiyo! Je hapo hawajatutafuna mpaka mifupa?

Kwanza nikuulize. Ule mkataba umeusoma? Tusije kuwa tunabishania kitu na hukijui
Wapi inesemwa hivyo?
 
Moja wapo ndo iliyosababisha uzi wangu kutopata jibu hadi muda huu tangu jana
Swali la kijinga haliwezi pata majibu!!

Unaambiwa makubaliano hayo yanavunja Katiba na Sovereign ya nchi,

We unatuambia wapi duniani wamewahi enda tofauti na Utaratibu wa DP World!!!

Yoda kakujibu, Italy makubaliano Yao yameonyesha kiwango Cha uwekezaji hujajibu!!!

Jibu ni Rahisi, Watanzania hatutaki Nchi moja au Kampuni kuwa na mamlaka juu ya ardhi yetu yaliyo juu ya Katiba.

TUMEKATAA UHUNI!!!
 
Kaka unatatizo sasa kisa mwenzio kala nya basi nawe uletu! kama uwekezaji hauoneshi kiwango unawekeza nini sasa ?
Anataka kulazimisha eti Kila mwanamke akojoe amechuchumaa anasahau kuwa wanawake wazee sana nyonga zao haziruhusu kuchuchumaa, wanajisaidia wamesimama!!!
 
View attachment 2702775
Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

Kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba mithili ya IGA iliyosainiwa kati ya Tanzania na Dubai unaotaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework ontracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani radi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine. Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

View attachment 2702567

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulaiza wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA. Mchoro ufuatao unafafanua zaidi.

View attachment 2702566

Mifano ya Mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
Hakuna haja ya IGA kati ya Tanzania na Dubai

Baada ya kusema hayo hapo juu sasa nafanya majumuisho muhimu kwa kuzingatia hoja yafuatayo:

Njia mojawapo ya kusanifu hoja, ni kuanzia kwenye ufanano wa vitu viwili. Njia hii huzalisha hoja yenye muundo ufuatao:
  1. Kitu X na kitu Y vinafanana kwa sababu kila kimoja kinazo sifa a, b, and c.
  2. Kitu X pia kinaonekana kuwa na sifa nyingine d.
  3. Kwa hiyo, kitu Y pia kinapaswa kuwa na sifa hiyo d.
Kwa kutumia mantiki hiyo hapo juu, sasa nawea kukujibu kikamilifu kama ifuatavyo:

Mosi, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza na kammpuni ya DPW kutoka Dubai zinafanana kwa kuwa zote ni Kampuni za wawekezaji wa Kigeni wanaotaka mazingira tulivu ya uwekezaji ili wafanikiwe kuwekeza, kuvuna na kuhamisha faida kutoka nchini Tanzania, ambapo HELIOS anajenga na kuendesha minara kwa kuikodisha kwa makampuni yanayosafirisha mawimbi ya simmu hapa Tanzania, wakati DPW anajenga na kuendesha bandari za mmajini na nchi kavu kwa kuzikodisha kwa watu wanaosafirisha mizigo.

Pili, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza inao uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza.

Na tatu, kwa hiyo, Kampuni ya DPW kutoka Dubai inapaswa kuwa na uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai.

Yaani, timu ya Johari Hamza haikuwa na weledi katika mambo haya.

Hitimisho na mapendekezo

Mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inawezekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.
This is thec truth but not quitecthe whole truth - it us too presumptious, too bland for general use.

Mfano wa a+b+c+d ni mzuri, as long as kuna uelewa wa pamoja wa mutual interdependence.

Yaani kampuni ya Kenya na ya Tanzania na Canada hakuna ubaya kuingia mkataba bila mwavuli wa dola, hasa kama makampuni yana ukubwa roughly ule ule, tuna uzoefu wa siku nyingi.

In the case of countries like Somalia au Bosnia au Haiti, yenye historia ya ukorofi, ni vyema kujihami kwa kushirikieha doka za nchi husika. Hiyo ndiyo IGA ili mkianza kuoenena dola iweze kuingilia. Hii huitwa umbrella protection, yaani uko chini ya ulinzi wa mwavuli wa dola.

Mfano kama huu ni taasisi za Umoja wa Mataifa. Mkataba wa Tanzania na UN ni wa muda mrefu, hauna ukomo, haufi hivihivi yaanini kama IGA.

Lakini miradi wa taasisi za Umoja wa Mataifa, mathalani njaa (FAO) au malaria (WHO) au Uchaguzi (UNDP) una mashariti kamili na kikomo kamili (kama malaria ulivyoisha Zanzibar na WHO).

Anachosema Mjumbe ni sawa, lakini IGA hutoa comfort on BOTH SIDES, haipunguzi chochote anachokusema wala haiathiri chochote.

Kamati ya Johari ilikuwa makini na imeona mbali zaidi kwa kuweka KPI - key performance indicators - kwa kila mradi, ambazo ni SMART - specific measurable achievable relationable timebound.

Kitu pekee ambacho kingejitosheleza bila IGA ni iwapo kampuni tanzu ingesajiliwa Dar es Salaam Stock Exchange, soko la hisa, ambalo taratibu na kanuni zake tayari ni za limaraifa. Mifano halisi Tanzania nu SWISSPORT ya Uswisi, TCC (sigara, ya Japan), TBL (beer, ya Makaburu) na NMB (benki, ya Uholanzi).

Lakini hata hizi nyingi ziba IGA tayari. IGA kazi yake ni kama mwavuli wa swerkali zote mbili, to give comfort to both sides.

Imagine kampuni kama TANAPA au Mwebdokasi iingie ubia na kampuni ya Mongolia au Papua New Guinea, wapi na wapi?

Au imagine DPW waje halafu 2030 CHADEMA watawale kwa kutumia mgombea binafsi millionaire Donald Trump kwa sera ya uraiapacha na majimbo, achukue Kilimanjaro yote na Kanda ya Kusini kwa kuhonga.

Cha kwanza atakachofanya ni kufuta Mkataba wa DPW kwa mabavu ili upewe kampuni ya Tundu Lissu au ukoo wa Mbowe. Leo hii DPW watakubalu? No, ni lazima pawe na kipengele kuzuia matumizi ya mabavu.

Kumbuka IGA haizuii mkataba kufutwa au kukoma, kinachotakuwa ni taratibu zifuatwe.

LGFMwambalule
Kawe.
 
Nimekuuliza swali la msingi. Mkataba umeusoma?
Hajawahi kuusoma ule mkataba, haujui nina hakika, ndio maana toka mwanzo wa hii issue nikiwa namuuliza maswali kuhusu ule mkataba hakuwahi kunijibu hata moja.
 
Swali lake lilieleweka vizuri, tatizo lake hakuwa na authority yoyote ya maana kuthibitisha kile alichokuwa akisimamia, hakuwa hata na mifano ya IGA iliyoingiwa bila hivyo vipengele anavyodai, vikapelekwa HGA, yeye akawa anaimba tu.

Ndio maana kila akiulizwa kwanini kila IGA isiwe na hivyo vipengele, kama cha mgawanyo wa mapato, lazima viende HGA, is it a worldwide rule? if yes aseme inaitwaje, anakosa majibu.

Hapo kwenye hiyo mifano mitatu uliyompa ya hiyo mikataba, umemaliza mjadala wake, naamini sasa ameondoa ujinga kichwani mwake, na yupo mwingine akaomba kuchukua sehemu ya ujinga wake, ili akatengeneze ujinga mwingine Pascal Mayalla msitujazie server ya JF kwa ujinga wenu.
Haya mambo yanahitaji twenda taratibu na kuelekezana. Maana hii ni taaluma na inahitaji utaalamu na uzoefu wa muda mrefu. Kuna baadhi ya mambo hapa, hata mtoa mada wetu ameteleza sana na yamenipa ukakasi, sema sintayasema. Ila kwenye hili, watanzania tunahitaji kwenda taratibu sana bila kutunishiana misuli. Kuna giza kubwa sana huko mbeleni...
 
Sasa kwa nini msiseme hamna majibu? Kuna shida gani mkikubali kuwa mmeshindwa?
Swali la kijinga haliwezi pata majibu!!

Unaambiwa makubaliano hayo yanavunja Katiba na Sovereign ya nchi,

We unatuambia wapi duniani wamewahi enda tofauti na Utaratibu wa DP World!!!

Yoda kakujibu, Italy makubaliano Yao yameonyesha kiwango Cha uwekezaji hujajibu!!!

Jibu ni Rahisi, Watanzania hatutaki Nchi moja au Kampuni kuwa na mamlaka juu ya ardhi yetu yaliyo juu ya Katiba.

TUMEKATAA UHUNI!!!
 
Hiyo ni opinion yako. Opinion yako sio jibu la swali ukiloulizwa. Pekeka hiyo opinion yako kwa Dubai huko wakujibu.

Unajifanya unatoa maelezo mengi kumbe unajibu opposite na ulichoulizwa.

Kama huna jibu sema sina jibu na utoe hiyo opinion yako.

Stress breaker...

1690707990570.png
 
Back
Top Bottom