JAY millions zazua utata, Mteja anataka dhulumiwa 100M na VodaCom

JAY millions zazua utata, Mteja anataka dhulumiwa 100M na VodaCom

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,193
Reaction score
515
Habari na Dotto Mwaibale — MSHINDI wa mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions Danny Paul Njau kupitia jina la Innocent Daniel Njau ametishia kwenda Mahakama kuishitaki kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushindwa kumpa zawadi yake ya ushindi sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions.

Njau ametoa siku saba kwa kampuni hiyo kuhakikisha inampatia fedha hizo vinginevyo atakwenda mahakama kutafuta haki yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Njau alisema amesikitishwa na danadana anazopigwa na kmapuni hiyo kushindwa kumpatia kitita chake hicho baada ya kushinda.

"Tayari nimetoa malalamiko yangu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuhusu suala hilo lakini mpaka hivi sasa bado hajafanikiwa" alisema Njau.

Njau alisema kwamba tangu kampuni hiyo ianze kucheza mchezo huo alikuwa akishiriki kucheza kila siku na ilipofika Januari 14, 2015 saa 5:8 asubuhi kupitia simu yake alipokea ujumbe sms iliyosomeka hivi 'hongera wewe ni mshindi wa leo wa Tzs Miliioni 100 utapigiwa simu na wafanyakazi wa Vodacom. Kwa maelezo zaidi ndani ya masaa 48 ambapo alisubiri bila ya kupigiwa simu kama alivyoelekezwa.

Alisema Januari 20, 2015 alienda ofisi za vodacom na kuwaelezea kuhusu jambo hilo ambapo aliambiwa awape muda na aliporudi Januari 22 alikutanishwa na maofisa wa Jay Millions na kufanyanao kikao akiwepo mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ambapo aliambiwa kuwa eti sms hiyo ni ya kwao lakini ilitoka mapema kwenda kwake.

Njau alisema kwamba kauli hiyo ilimshangaza sana ukizingatia kuwa katika kipindi hicho cha mchezo kulikuwa na matangazo yaliyokuwa yakisema kila siku kutakuwa na mshindi mmoja wa sh.100, washindi 10 milioni 10 na washindi 100 wa sh.milioni 1 na kuwa yeye alifuata taratibu zote za kucheza mchezo huo Jay kwenda 15544 na kuona sms ya ushindi.

Alisema baada ya majadiliano na maofisa hao walimuuliza wampe sh. ngapi kwa kuwa zawadi hiyo imetoka mapema na kabla ya watu hawacheza na kuwa wao hawana pesa nyingi anayoifikiria.

Alisema hakuamini kilichokuwa kikifanywa na kampuni hiyo katika uchezeshaji wa mchezo huo na kuwa aliomba apewe muda wa kutafakari ambapo aliamua kupeleka malalamiko yake kwenye bodi ya michezo ya kubahatisha na kwenye vyombo vya habari.

Jitihada za mtandao huu kumpata mmoja wa maofisa wa Vodacom Tanzania ambaye alitajwa kuwa ni Meneja, Kelvin Twisa ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kupigwa zaidi ya mara nne bila ya kupokelewa, pia hali kama hiyo ilitokea kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas Tarimba ambaye simu yake ilikuwa imefungwa jitihada hizo zinaendelea ilikutoa fursa kwa maofisa hao kutoa ufafanuzi ili umma wa watanzania upate kujua kinachoendelea katika kampuni hiyo.


 
Mkuu kwanza Happy Join Day (Join Date : 6th June 2012) kwa kutumia Miaka 3 Leo.


hii michezo ya Bahati nasibu mimi Binafsi huwa siamini. Ntakuja kuamini labda siku nishinde mimi na kupewa kitita changu.

Pia hizo sababu walizompa haziingi akilini kabsa.
 
tangu hili shindano lianze nilisikia mshindi mmoja tu akitangazwa kuwa kashinda yule dada wa kilolo huko sjui..tangu hapo naskiaga tu kuwa kila siku kuna watu wanashinda basi sijawahi skia tena hao washindi wakitangazwa..hata huyo wa mshindi mil 1 tu sjawahi skia hata siku noja akitangazwa na wanasema kila siku kuna mshindi..!! bora hata lile la airtel shindano la gari lilikuwa linatia moyo maana washindi angalau walikuwa wanatangazwa na kuhojiwa waziwazi...ila voda!??
 
Mkuu kwanza Happy Join Day (Join Date : 6th June 2012) kwa kutumia Miaka 3 Leo.


hii michezo ya Bahati nasibu mimi Binafsi huwa siamini. Ntakuja kuamini labda siku nishinde mimi na kupewa kitita changu.

Pia hizo sababu walizompa haziingi akilini kabsa.
Daaah! Kwahiyo huiamini lakn unashiriki?
 
Vodacom ni wizi mtupu, hata salio lina kwanguliwa kutoka kwenye simu.
 
bahati nasibu ...ndio mchezo....kila siku unalizwa
 
Huu ni sawa na Kamari tu.
Mnaweka pesa mezani mnalipia woote wateja kisha wengine mnaliwa.

Huyo dada itakuiwa issue imebuma,yaani walietegema kummegea ikadunda.
Mungu huwa hamfichi mnafiki,sasa hapo ndio alipowaumbua.

We unakuta mtu unaambiwa Mama lishe au Baba Lishe ameshinda,ukimuona hali taabanii.
Na unaweza kushangaa unakuta mtu anaambiwa umeshinda Milioni kumi,wala hastkuki,anaona zake poa,unamsikia haya.
Yaani unaona kabisa kwamba mambo sio ndio.

Hata kama wametuma kwa Bahari mbaya na sms ni yao,inabidi ulipwe kwa kuwa ni mshiriki.Nakama imetumwa kwa makosa inamaana kuna watu huwa wana set system kwamba pesa iende kwa nani.
Mbona sie tukipiga sim kwa makosa kwa mtu mwingine huwa tunakatwa,sasa na wao ile kwao.

Komaa nao Sister hadi kieleweke.
Issue ya kupiga imebuma hapo.

Thanks God kwamba Tangu nazaliwa sijashiriki KAMARI hii ya kwenye sim.
Tukiulizana kila alieshinda hali yake leo ipo,ni taabani.
 
Shindano naloliamini lisilo na ubabaishaji ni haya ya kwenye soda aka Chini ya kizibo. Kwani nlishashinda Laki Moja mara ya pili nkashinda 10000 na soda za bure kibaaao
 
bora ukabet utapata hela yako lakin cyo hao matapeli voda
 
awapeleke tu mahakamani na achukue mwanasheria machachali wa kumtetea
 
Nafikiri amtafute Tundu Lissu au Mabere Marando, ili akamsimamie mahakamani...lazima watalipa na fine pia!

Halafu kuna mtu ajaiita January Makamba, anataka kugombea urais wa Tanzania wakati unaibu waziri tu unamshinda......ebu ona malalamiko ya wananchi kama haya na mengine lukuki ya kutapeliwa na makampuni ya simu na hasa VodaCom anayapa kisogo, sasa atawezaje kutatua matatizo ya watanzania yanayohusu nyanja mbalimbali?

January hufai, tena hufai! Eti unataka urais.

..my .sss!
 
Aende mahakamani atapata haki yake. Watanzania tuache kulalamika tu kwenye kutafuta HAKI
 
Hawa vodacom ni weziiii huwa wanakukwangua salio sasa ndyo hyo jay milionea?komaaa nao wapeleke mahakamani
 
Nafikiri amtafute Tundu Lissu au Mabere Marando, ili akamsimamie mahakamani...lazima watalipa na fine pia!

Halafu kuna mtu ajaiita January Makamba, anataka kugombea urais wa Tanzania wakati unaibu waziri tu unamshinda......ebu ona malalamiko ya wananchi kama haya na mengine lukuki ya kutapeliwa na makampuni ya simu na hasa VodaCom anayapa kisogo, sasa atawezaje kutatua matatizo ya watanzania yanayohusu nyanja mbalimbali?

January hufai, tena hufai! Eti unataka urais.

..my .sss!
lowasa hana share huku voda?am curious maana nlisikiaga ana hisa nyingi tu sasa ukimchukua Tundu haitapenyeza maji kweli kw alowasa/
 
Back
Top Bottom