Jay Z aibuka kuwa Rapa bilionea wa kwanza duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Jay Z ndiye rapa wa kwanza duniani kuwa bilionea, kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Forbes iliyowekwa wazi wiki hii.

Rapa huyo ambaye ni moja kati ya wafanyabiashara wakubwa ametajwa kuufikia ubilionea kupitia biashara zake za muziki pamoja na uwekezaji katika sekta nyingine.

“Katika kipindi cha chini ya muongo mmoja, Jay Z amekusanya ukwasi ambao unakamilisha jumla ya $1 bilioni, hali inayomfanya kuwa mwana hip-hop wa kwanza kufikia kiwango hicho cha utajiri,” ameandika Zack O’Malley, mwandishi wa Jarida la Forbes.

Jarida hilo limetaja vyanzo vya mapato vya rapa huyo mkongwe kuwa ni pamoja na kuwa na hisa ya $70 milioni kwenye kampuni ya usafiri ya Uber, $70 milioni kwenye masuala ya sanaa, $50 milioni kwenye umiliki wa majumba ya kupangisha na muziki, umiliki wa ‘Tidal’ inayouza nyimbo mtandaoni pamoja na umiliki wa Kampuni ya Roc Nation.

Jay Z alizaliwa katika mitaa ya Brooklyn nchini Marekani na kuishi maisha ya shida akilelewa na mama yake. Aliingia rasmi kwenye ramani ya muziki mwaka 1996 alipoachia albam yake ya kwanza ‘Reasonable Doubt’.

Mapema mwaka huu, albam yake ya sita aliyoitoa mwaka 2001 ya ‘The Blue Print’ iliwekwa kwenye Maktaba ya Taifa hilo ikitajwa kuwa miongoni mwa albam zinazostahili kuwa za kihistoria na zenye faida halisi kwenye jamii.

Jigga amemuoa mwanamuziki Beyonce na wamebarikiwa kuwa na watoto watatu.

Mwaka 2004, Dr. Dre alitajwa kuwa ndiye mwanamuziki wa kwanza kuwa bilionea, akitajwa kuwa angeingiza $1.1 bilioni kupitia mauzo ya headphone zake za ‘Beatz by Dre’ kwa kampuni ya Apple.

Hata hivyo, baada ya mahesabu ya makato mbalimbali, kipato chake halisi kilibainika kuwa chini ya $1 bilioni na kumuondoa kwenye orodha hiyo ya kihistoria.
 
Watu wana pesa aseee
 
Jamaa anazeeka anazidi kuwa kijana tu daah nakumbuka maneno ya Chris Rock Money is the best lotion ever
 
Mmenifanya niskilize hizi ngoma pamoja na instrumental zake aisee.

Dead Presidents na Hard Knock Life.

Hatari sana.
 
Hata Jacob Makalla(JCB)na Chindoman ni ma'bilionea sema tu hawanaga njaro za show off chaliangu.
 
Safi sana it's good to see a Nigga on top of the league....kwa bongo maswali bado ni mengi.....vijana wenye B kama usd 500000/400000 wanahesabika hiyo fedha ni nje ya mzunguko wa biashara yake.....tena mfumo ulivyokuwa mgumu watapotea kabisa...wengi walitengeneza fedha kwenye madini....na biashara za China to kariakoo wakati w JK....nazungumzia biashara halali.... though kulikuwa na ukwepaji wa kodi....
 
Hivi wanawezaje kuzitenganisha hela zake/investments na za mkewe?
 
Now that all the smoke is gone, lighter
And the battle's finally won, gimme a lighter

Victory is finally ours lighter's up, lighter's up

History so long, so long, so long, so long

In search of victory she keeps saluting me

If only we can be together momentarily
We can make love and make history
 
Back
Top Bottom