Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jay-Z ameripotiwa kujichagua mwenyewe kuwa msanii mkuu atakayetumbuiza katika kipindi cha mapumziko cha mchezo wa Super Bowl 2027.
Kampuni ya burudani ya rapa huyo, Roc Nation, imekuwa ikishiriki katika kuchagua wasanii na kuandaa maonesho ya kipindi cha mapumziko cha ligi ya NFL tangu mwaka 2019. Sasa, kwa mujibu wa taarifa za tovuti ya habari ya Puck, Jay-Z ameamua kupanda mwenyewe jukwaani na kutumbuiza katika onesho hilo.
Wasanii wengine waliotajwa kuwa walifikiriwa kwa nafasi hiyo ni Justin Bieber na Miley Cyrus.
Onesho hilo linalosubiriwa kwa hamu litafanyika katika uwanja wa SoFi Stadium, jijini Los Angeles, mwezi Februari mwaka 2027.