bluetooth23
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 348
- 326
Ukitembelea www.roc-nation.com/artisttour na www.jay-z.com utaona jinsi ratiba ya music tours za wasanii hao zinaonyesha kuwa watakuwa nchini Tanzania mwezi oktober mwaka huu. Ujio huo japo haujawekwa wazi ila unahusishwa na tamasha la kila mwaka la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Media Group kwa kushrikiana na PrimeTime Promotions. Inasemekana Joseph Kusaga alikuwa New York mwezi wa pili mwanzoni na kuwah booking ya wasanii hao ambao huwa inaandaliwa kwa mwaka wote na ikishaandaliwa huwa haiingiliwi tena. CMG bado hawajatangaza na tetesi za wasanii hao kuja bongo kwa mara ya pili zinatoka kwa uongozi wa Clouds na kuaminishwa na mitandao ya wasanii hao inayoonyesha uwepo wa tour ya Tanzania.