JB ataoa sababu ya Bongo movie kufa

JB ataoa sababu ya Bongo movie kufa

Msanii mkongwe muigizaji wa Bongo movie Jacob Steven JB, ametoa sababu ya bongo movie kudorora kwa sasa. Amedai bado haijafa ila inapitia kipindi cha mpito, na kinachoifanya ikafifia ni kutokana na kufanya movie zinazofanana kila mara na watazamaji kuzizoea na kuona haina jipya.

Ametolea mfano kipindi cha uchekeshaji cha Komedi kilivyoanza na watu wakawa wanajazana kwenye TV kutazama lakini baada ya kuzoeleka wakaipotezea na hata Nigeria movie zao zilikuwa zinapendwa sana lakini nao wana tatizo kama la Bongo
Amedai haitakufa ila watakuja wasanii wapya na kiufanya tofauiti.


Maneno ya kujifariji
Iko wapi taarab
Iko wapi reggae ya kibongo
Iko wapi rap ya kibongo
Uko wapi muziki wa dance
Hii ni enzi ya bongo fleva nayo itaondoka
Bongo movie itarudi lakini sio sasa bado sana na itarudi kivingine kabisa na watu wengine kabisa
 
Alichosema kuhusu sci~fi eti hazipendwi na wanafanya sababu tu ya kuishiwa script kakosea kabisa.

Watu wanaopenda sci~fi ni wengi mno, ni genre inayolipa kuliko genre nyingine yoyote. Aangalie top 10 highest grossing films 9 zote ni sci~fi.
 
h
Zitaachaje kufa wakati mnatudanganya kama watoto wadogo. Msanii wa kike anavaa nywele mwanzo wa muvi hadi mwisho hizo hizo, au maiti ina hema. Hebu tupia moja na wewe.
ahhahahahahaaaaaa eti maiti inahema,umeua.au jambazi anavamia nyumba ya mtu hlf anavua viatu. heeeee
 
Bongo movie hakuna kitu kabisa ila nitoe pongezi kwa waliofanya SIRI YA MTUNGI walijitahidi sana mastaa wenye majina makubwa walikuwa wachache,story na ujumbe ulieleweka,sauti na picha ni HD kabisa walifanya vizuri.
Siri Ya Mtungi Imefanywa Na Kampuni Kubwa Ambayo Pia Ina Tawi Afrika Magharibi Ndio Wale Waliotengeneza Filamu Maarufu Za Neria Na Yellow Card.
 
Back
Top Bottom