JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Msanii anayefanya vizuri kunako bongo movie, Jacob Steven maarufu kama JB, hivi karibuni amekwaa scandal mpya ambayo imemshushia HESHIMA kama sio kumpunguzia credit ndani ya tasnia hiyo.

Msanii huyo maarufu amekumbwa na scandal hiyo baada ya muvi yake mpya kutoka inayofahamika kwa jina la MZEE WA SWAGA.

Muvi hiyo inayofanya vizuri sokoni inasadikiwa kukopiwa na ku paste kama ilivyo na moja ya movie maarufu kutoka bollywood inayofahamika kwa jina la "Ladies VS Ricky Bahl".

Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na JB, Kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya "mzee wa swaga" imeiga kama ilivyo kuanzia story hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.

Mtangazaji huyo amelaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya JB huku akijifanya yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa story hiyo wakati ukweli anaujua mwenyewe.

Hata hivyo JB bdo hajazungumzia chochote kuhusu tuhuma hizo zinazomkabili.

===========


 
Kama Aidia Ni Nzur.Na Yeye Akaona Akiiweka Katika Maudhui Ya Kitanzania Itavutia Wengi Tatizo Liko Wapi.Sisi Tunataka Burudani.

Inatuhusu Nini Sisi Kama Alikopi.Istoshe Muvi Yenyewe Inafanya Vizuri Sokoni.Huo Ni Wivu Tu Wa Sisi Wabongo.Tunamtafutia Vikasoro Ili Tumuharibia.

Tusubiri Mpaka Hao Wahindi Wenyewe Walalamike Kuwa Muvi Yao Imekopiwa.Tuache Viherehere
 
Imekaa vizuri nilimuona zama akiadithia jinsi JB alivyo CAP,Kipengele cha Story amesema wangeweka Mtafsiri
 
Kwani wangapi waliiona hiyo ricky ya kihindi, kama aliipenda akaamua kuigiza kuna tatizo, issue ni haku acknowledge alipoitoa
 

kucopy bila kutoa credit kwa uliyemcopy ni wizi
 

Wivu wa nini? Kama kaiga asiambiwe? Kwa nini adanganye movie katunga yeye wakati sio kweli? Hilo ndo tatizo, na hyo sio movie yake ya kwanza kuiba
 
jana nilibahatika kuona hicho kipindi yaani ni balaa walichofanya ni kutafsiri tuu ni zaidi ya plagiarism...😁

Kama n zaidi ya plagiarism na afungwe tu ilu
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni kudanganya katunga yeye wakati sio kweli, we unadhani iko sawa?

Haiko sawa asingejiweka kama mtunzi angempa credit alietunga ye kacopy tu kwanza si kukopi katafsiri tu
 
Kuna nyingine ya kiamerika inaitwa deliver us from eve.
 
Huyu Zamaradi wiki Jana aliisifia sana. Baada ya kuonyeshwa kuwa amecopy anaanza kuponda. Vipindi vingne wanaanzisha hats siyo watafiti mpaka waambiwe
 
Ebu mwambie mshamba huyo, tatizo ni kujifanya katunga yeye wakati sio kweli, huo ni wizi


Angepitia chuo kikuu angejua madhara ya kutumia/kunukuu kazi ya MTU bila kumu acknowledge...

Hata hivyo kwa akili gani walizonazo hao viwavi mpaka walete ubunifu mpya? kwa vichwa vile butu unafikiri vinaweza chemka kubuni vitu vipya?? THUBUTU!!!!
 
Ni kweli sio ya kwanza kuna moja yake pia inaitwa Regina jamani ile kabisaaa alipaste movie ya black Americans inaitwa deliver us from Eva sio Mara ya kwanza kazoea

Yes, regina nayo aliiba japokuwa ilifanya vzur sana ile movie, regina ilikuwa ni bonge la movie, ila aache wizi ajifunze kuwa mbunifu kama hawez kutunga watunzi wako wengi tu
 

Kwanini haku hakusema kuwa amechukua kutoka sehemu fulani au kuonesha kushukuru hiyo movie.? Mnatetea bure tuu ameboronga kabisa huyu hakutakiwa kukopi na kupaste kabisa kila kitu..huyu JB kaishiwa kabisa na amekosa la kujitetea kabisa..
 
Angepitia chuo kikuu angejua madhara ya kutumia/kunukuu kazi ya MTU bila kumu acknowledge...

Hata hivyo kwa akili gani walizonazo hao viwavi mpaka walete ubunifu mpya? kwa vichwa vile butu unafikiri vinaweza chemka kubuni vitu vipya?? THUBUTU!!!!

Nawashangaa kuna watu wana mtetea humu mkuu lusungo mimi niliangalia movie hiyo jama kwenye kipindi cha zamaradi hakika JB kakopi maneno,character ,mpangilio wa movie hadi movement za character halafu anajifanya kuchukia kwa kuwa kasemwa.
 
Last edited by a moderator:

Kweli mkuu umenena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…