JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

Attachments

  • 1424900410213.jpg
    1424900410213.jpg
    39.2 KB · Views: 427
  • 1424900431264.jpg
    1424900431264.jpg
    50 KB · Views: 416
Huyo zamaradi wake ni wivu tu na muvi idea yake ya kigodoro haijampeleka popote sasa kabakia kupondea na kuonea wivu wenzake
 
Daah asee nilichek clouds tv comparison ya hio movie ya kibongo Na hio ya kihindi, for sure jb amecopy kwa asilimia 90 and above
 
Sio siri...filamu za kibongo zinatia ukakasi kuzitazama ikiwa wewe ni mtu wa quality na unazifahamu movie...
unatakiwa uwe na moyo wa kishujaa na kizalendo haswa kuziangalia hizi movie za kibongo
 
Kuna movie 1 inaitwa baad shah ya kihindi ya shahrukh khan ameiga almost kila scene kutoka kwenye movie ya mr. Nice guy ya jack chan, sijui kama jamaa walimu acknowledge j.chan
 
Kama Aidia Ni Nzur.Na Yeye Akaona Akiiweka Katika Maudhui Ya Kitanzania Itavutia Wengi Tatizo Liko Wapi.Sisi Tunataka Burudani.

Inatuhusu Nini Sisi Kama Alikopi.Istoshe Muvi Yenyewe Inafanya Vizuri Sokoni.Huo Ni Wivu Tu Wa Sisi Wabongo.Tunamtafutia Vikasoro Ili Tumuharibia.

Tusubiri Mpaka Hao Wahindi Wenyewe Walalamike Kuwa Muvi Yao Imekopiwa.Tuache Viherehere

Asante
 
attachment.php



Inasikitisha sana kama wasanii wetu wanaweza kufanya uhuni huu na kutuaminisha watanzania kwamba wametunga wao.

Binafsi nimeangalia muvi ya Ladie Vs Ricky Bahl mwaka 2011 na ni moja kati ya movie ya kihindi niliyoipenda kutokana na maudhui yaliyo kwenye movie hiyo.

Ricky Bahl alicheza kama Conman mtaalam aliyekuwa anawalaghai wadada mbalimbali kwa mapenzi ya dhati kumbe alikuwa akiwaaminisha ili awatapeli na kweli alifanikiwa kufanya kwa wadada hao.

Alikuwa ana uwezo wa kubadilisha muonekano wake na ku-appear tofauti tofauti hivyo kuwa ngumu kumtambua.

Sasa huyu bwana mkubwa bonge la Bwana kaiba idea nzima nzima bila hata kufigha,nafikiri alidhani kwakuwa tokea hiyo muvi ya kihindi imetoka ni muda mrefu(2011) hivyo watu tutakuwa tumesahau, kumbe sio!!

Niliangalia vizuri Kipindi cha Zamaradi kwa jinsi alivyokuwa akielezea na nilistaajabu sana. Kuiba idea sio vibaya kama utaweka umma wazi kuwa ile movie umechukua idea na kuitengeneza katika maadhi ya Kibongo bongo.

Hata ukiangalia wahusika wakuu, kwenye muvi ya Kihindi walikuwa watano na hata ya JB watano pia ( Mwanaume mmoja na wadada Wanne).

Nisieleze mengi lakini jamaa kaiba kwa asilimia 99 na mbaya zaidi kaudanganya umma na mashabiki wake kwamba yeye ndio mtunzi wa muvi hiyo.

Wasanii tubadilike, Tunaitia Tanzania aibu.

Asanteni.
 

Attachments

  • MUVI JB, Bahl.jpg
    MUVI JB, Bahl.jpg
    31.2 KB · Views: 3,441
Kuna movie 1 inaitwa baad shah ya kihindi ya shahrukh khan ameiga almost kila scene kutoka kwenye movie ya mr. Nice guy ya jack chan, sijui kama jamaa walimu acknowledge j.chan

ahsante kitu gan na wewe ebu acha umbea,mtu akiiba asiambiwe? na kwa nini ajifanye katunga yeye wakati sio kweli? ki ufupi jb kajishushia heshima sana
 
Wasanii watambue kuwa huo ni uhalifu. Nashangaa sana kwani yako mambo mengi sana ya kuact kwa uhalisia wa kitanzania na yakawa mazuri. Niliipendaga sana ile Movie ya kina Hemedi ya kuokota mtoto mchanga na kumtunza. Jamani majuzi nakuja kuiona Movie exactly kama hiyo! Japo nikiri sifahamu nani kaiga ila kama ni wabongo si vizuri, mbona kuna vituko vingi tu wanaweza kuact na vikapendeza. Tusiwaige wanaigeria ambao mpaka movie ya zamani ya 'Coming to America' aliyoigiza Eddie Murphy wameicopy na kuipaste!
 
JB Mapovu yanamtoka uko insta,ngoja nimfuate uko uko nikampe vichambo vyake,atajuta mpaka aji block mwenyewe,pumbav zake mwizi mkubwa
 
Tatizo ni kudanganya katunga yeye wakati sio kweli, we unadhani iko sawa?
Tatizo sio kudanganya tu bali suala zima halikubaliki kisheria! Unaweza kuchukua idea kisha ukai-twist kivyako... hiyo inakubalika! Aidha, jambo lingine linalokubalika ni kuchukua few seconds of a particular scene na kui-develop kuwa new story, hilo pia linakubalika! Lakini unapochukua kila kitu au scenes kibao, hilo halikubaliki hata kidogo unless kuwe na makubaliano! Na hata kukiwa na makubaliano, lazima utoe credit kwa original movie!

Tena kwa jinsi ilivyo, hiyo Ladies VS Ricky Bahl tayari ni movie lakini hata kama ingekuwa ni script ambayo haijawa produced, pia haikubaliki kisheria na ndio maana hata script huwa zinasajiliwa! Unaweza kuchukua a small part of a particular scene kwenye script kisha ukai-develop, hapo sawa lakini unabeba scenes kibao, hapo hata kama utatoa credit kwa mwandishi, no one will ever understand you... ukiwa sued, lazima jumba bovu likudondokee!

c.c zedlyn
 
Last edited by a moderator:
zamaradi popote ulipo chukua tano kwa kumuaibisha huyu kweli kanumba tangu afe hakuna upinzani nilicheka sana kuona hiki kipindi kuna sehemu huyo stering wa kihindi alikuwa anawachungulia hao mabinti JB na mtumbo wake nae eti anachungulia ,we si unasema umeokoka huo nao ni wizi kama wizi mwingine tatizo tasnia ya filamu bongo imejaa failures,umefanya pargarism lakini ukikuta mtu kafanya pairacy kazi yako unamind aibuuuuuu
 
mnaoangalia muvi za kibongo hongereni kwa moyo wa kishujaa!!!!!!
 
ahsante kitu gan na wewe ebu acha umbea,mtu akiiba asiambiwe? na kwa nini ajifanye katunga yeye wakati sio kweli? ki ufupi jb kajishushia heshima sana

We unaf1rw4 nn kuna sehemu yoyote nimesapot akichokifanya Jb, soma post vzr
 
Haishangazi sana JB kuwa mwizi wa idea za watu, coz anatoka kwenye ukoo ule ule

wasanii.jpg
 
Na ile muv ya dam yang ya steve nyerere na mainda wamecopy kene mr&mrs smith jmn bra kanumba angekuepo
 
Back
Top Bottom