JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

Unasema sio wewe ulieandika haya? Kwa hiyo ni coincidence tu huyo mwandishi Daniel Manege naye kaandaa filamu ya safari ya Gwalu jina linaloendana na id yako ya jf?
 
Mwambie utetezi wake ni dhaifu kabisa....mwambie kwanini aliandika mtunzi wa story ni JB?
Kwanini haku acknowladge?
Kwanini JB mwenyewe haoneshi kukubali kosa anajifanya kukomaza shingo huku akijua inaweza vunjika?

Muulize kwa hiyo anajaribu kusema kukopi na kupaste ni jambo la kawaida?Muulize ni movie ngapi hadi sasa amekopi na kupaste?

Muulize tusinge baini alipanga kusema ukweli lini?
Mwambie akaandike utetezi mwingine!
 
Hilo ni angalizo zuri,
Ila tujue pia tasnia yetu idara zake nyingi sio makini hivyo kuna makosa mengine muandika script au muigizaji mkuu yanakuwa sio yao moja kwa moja....
Ila ndio hivyo goli mkifungwa linakuwa ni kosa la timu nzima

Ina maana story za kuigiza zimekwisha? Mbona kuna watu waandika script vizuri hawawapi tenda?
 
Duuh! mkuu hilo jina lako la pili kule kwetu huwezi kulitamka!
 
Umeeleweka mkuu tena bora daniel amejitetea sema humu jf kimekuwa kama kijiwe cha wahuni na mafundi wa kushushua wenzao. Mleta mada amem quote mwandishi wa hiyo muvi sasa mtu mnamuattack mleta mada its not fair.
 
Tena asituchefue tukaanza kupekua na movie nyingine za kihindi maana hyo sio movie ya kwanza kuiba hyo, Regina nae aliiba tukamchunia kimya hii nayo tena kaiba, tatizo wanaona wote wanaoangalia bongo movie ni matahira kam wao
 
Umeeleweka mkuu tena bora daniel amejitetea sema humu jf kimekuwa kama kijiwe cha wahuni na mafundi wa kushushua wenzao. Mleta mada amem quote mwandishi wa hiyo muvi sasa mtu mnamuattack mleta mada its not fair.

Huu utetezi ulipaswa kuletwa na JB toka mwanzo si kusubiri mbeleko! hata hivyo utetezi wako ni moja ya utetezi dhaifu kabisa! Kilicho wafanya waandike mtunzi ni JB?
 
Kwahiyo ndio kusema hizo mikitu yenu mnayoigiza ni copy za original ili mayaya waelewe Holywood world?basi igizeni Tekken 1 maana mtaani kwangu mayaya wanaipenda
 
Huu utetezi ulipaswa kuletwa na JB toka mwanzo si kusubiri mbeleko! hata hivyo utetezi wako ni moja ya utetezi dhaifu kabisa! Kilicho wafanya waandike mtunzi ni JB?

Imekuwa utetezi wangu tena mm ndo manege acheni hizo angalau amejaribu kujitokeza na kujieleza mbona mnakuwa hivyo. Tena wewe rutta ungetulia maana huwa mtetezi sana wa mafisadi.
 
Hakuna kitu kwamba eti ni jambo la kawaida duniani kutumia maudhui ya filamu nyingine... huu ni uongo usio na maana yoyote vinginevyo kusingekuwa na suala la hati miliki kwenye filamu! Jana hapa nimetoa mifano mingi kwamba, hata script, achilia mbali filamu, nazo zinakuwa copyrighted, so how come tena mtu apoteze gharama zake ku-copy right material yake halafu iwe avaialble to anybody??

Kinachokubalika kwenye filamu ni kuchukua wazo/idea na sio maudhui/content na hata katika ku-copy right, huwezi ku-copy right wazo/idea ingawaje unaweza kuuza wazo/idea! Unaruhusiwa kuchukua kasehemu kadogo sana kafilamu, tena kasikofika hata dakika moja kisha ukaka-develop... kwamba kale kasehemu, kanakuwa ni idea ambayo unai-develop into a new script... hilo linakubalika lakini sio kuchukua madakika kadhaa ya filamu husika au scenes kadhaa za script husika halfu watu waseme hiyo inakubalika... hakuna kitu kama hicho na ukiona kimefanyika basi fahamu wamekubaliana! Mathalani, Hollywood huwa wananunua indie movies (filamu zinazotengenezwa na vimapuni vidogo/indie companies) na kuzi-develop into major movies! Hizi indie movies hawazinunui sokoni au supermarket bali wanazinunua kutoka kwa wamiliki... yaani, assume Producer ameiona filamu ya Mzee wa Swaga ya JB na ameipenda! Hapo ana-opt kufanya biashara na JB na kuinunua movie husika kwa thousands or millions of dollars kisha yeye anaenda kuitengeneza upya! Katika mazingira kama haya, mahudhui/content inaweza kufanana lakini pia kunakuwa na makubaliano mtu kama JB atapata nini akitokea third part akaipenda the same film lakini kutokea kwa new producer/mmiliki!!! Wakati wanauziana, haya yanakuwa tayari wameshayaweka sawa manake anaweza kutokea mwingine akataka kutumia hayo mahudhui kutengeneza series! Je, JB alifanya kitu kama hicho? Na more important, hata kama huyo producer amenunua filamu kwa JB lazima kwenye filamu yake mpya atoe credit... je, JB amefanya hilo jambo?

Hapa wanatetea ujinga na wala hawaelekei ikiwa wanafahamu hizi habari za filamu at higher level.
 
Imekuwa utetezi wangu tena mm ndo manege acheni hizo angalau amejaribu kujitokeza na kujieleza mbona mnakuwa hivyo. Tena wewe rutta ungetulia maana huwa mtetezi sana wa mafisadi.
Amejitokeza baada ya kuumbuliwa!
 
Anasema anaumia mno na kuumiza akili katika kutunga story! warumi umemwelewa huyu mvivu? Sasa anataka kazi yake iwe nyepesi....! Sipendi kuangalia movie ya bollywood version ya kibongo tena bila credit kwa vile ulitingwa! Uli na matingo jobha

Amatingo ghikufuma kughu gwe mwanike!?
Wakati mtu kawaomba msamaha!!

Itapendeza mwamko huu tuuonyeshe kwenye filamu zote basi....
Pia inafurahisha kwamba movie hii imefuatiliwa sana
 
Last edited by a moderator:
Amatingo ghikufuma kughu gwe mwanike!?
Wakati mtu kawaomba msamaha!!

Itapendeza mwamko huu tuuonyeshe kwenye filamu zote basi....
Pia inafurahisha kwamba movie hii imefuatiliwa sana

Mr Gwalu, unaweza wewe na Jb mkatutafsiria white house down kibongo movie halafu JB ndio anamuokoa kikwete dhidi ya magaidi wa amboni au panya road?
 
Mr Gwalu, unaweza wewe na Jb mkatutafsiria white house down kibongo movie halafu JB ndio anamuokoa kikwete dhidi ya magaidi wa amboni au panya road?

Hahahahaha maatope ndugu yangu acha kunishikia chini bana...
Ila huu ukali inabidi muwe nao kwenye movie zote aisee.
Dogo amejitetea na amekubali lawama

Ila hivi ni vitu vya kawaida sema tu kamba hukatikia pembamba
 
Last edited by a moderator:
Umeeleweka mkuu tena bora daniel amejitetea sema humu jf kimekuwa kama kijiwe cha wahuni na mafundi wa kushushua wenzao. Mleta mada amem quote mwandishi wa hiyo muvi sasa mtu mnamuattack mleta mada its not fair.

Ahsante Queen Kyusa,
Watu wanaongozwa na hisia hata kutulia hamna basi ni rahisi hata kutokuona kuwa mhusika amewaomba msamaha!!
 
Last edited by a moderator:
Amatingo ghikufuma kughu gwe mwanike!?
Wakati mtu kawaomba msamaha!!

Itapendeza mwamko huu tuuonyeshe kwenye filamu zote basi....
Pia inafurahisha kwamba movie hii imefuatiliwa sana

Kuomba msamaha ndio mwisho wa mjadala? JB ana jadiliwa kwa kuwa kitu kama hiki hakikutegemewa kifanywe na yeye.
 
Kuomba msamaha ndio mwisho wa mjadala? JB ana jadiliwa kwa kuwa kitu kama hiki hakikutegemewa kifanywe na yeye.

Sio lazima mjadala ufungwe Rutta,
Ila mjadala unaweza ukabadili muelekeo sasa...
Huyo Miss niliyekuwa namjibu alisema kuwa "ndi na matingo" (kinyakyusa) akimaanisha malingo...
Naamini alikuwa akimaanisha Daniel,
Hivyo nikamjibu, malingo yanatokea wapi wakati mtu ameomba msamaha...
 
Unasema sio wewe ulieandika haya? Kwa hiyo ni coincidence tu huyo mwandishi Daniel Manege naye kaandaa filamu ya safari ya Gwalu jina linaloendana na id yako ya jf?

Mkuu naomba nikuhakikishie kuwa aliye present ujumbe huo yaani JouneGwalu sio Dan Manege, nje ya JF wote nawafahamu, hata shughuli zao ni tofauti.

Kidogo nipo tofauti na wengi kwa sababu kwanza namuona Script writer ni mtu unayeelewa uzito wa hili suala. Naamini alinuia vema kuandaa epistle hiyo kama sehemu ya confesion ya kutumia idea ya mtu ktk kazi yake pasipo prior owners acknowledgement.

Pamoja na udhaifu huo amekiri, na ninadhani sasa huu uwe msingi wa kujenga ushirika na wasanii wa filamu Tanzania ili kuongeza ideas ambazo hazijatumika.

Kwa Pamoja tunaweza.
 
Kijana anajikana ! hii inadhihirisha uongo kwenu jad
maelezo yako yanadai una filamu inaitwa safari ya gwalu, id yako je
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…