Je, Affidavit inatosha katika maombi ya ajira kwa wenye changamoto ya majina mawili?

Joined
Jul 30, 2024
Posts
5
Reaction score
13
Kwa mfano jina langu katika NIDA ni Mussa Ramadhani Mussa ila kwenye vyeti vyangu vya taaluma ni Mussa Ramadhani.

Nimesikia kuwa naweza kupata affidavit na nikafanikiwa.

Je, kuna ukweli katika hili?

Naomba ufafanuzi kwa yeyote ajuaye wakuu.

Nawasilisha!🙏
 
Kisheria inabidi itoshe, lakini nchi hii mnaijua wenyewe
 
Kwa mfano jina langu katika NIDA ni Mussa Ramadhani Mussa ila kwenye vyeti vyangu vya taaluma ni Mussa Ramadhani.

Nimesikia kuwa naweza kupata affidavit na nikafanikiwa.

Je, kuna ukweli katika hili?

Naomba ufafanuzi kwa yeyote ajuaye wakuu.

Nawasilisha!🙏
kwanza unachanganya kati ya avidavit na deedpoll kinachokibalika sio avidavit maana avidaviti haisajiliwi wizara ya ardhi, kinachotakiwa ni deedpoll sio avidavit
 
na
Mimi shida yangu sio kubadili jina maana majina yangu yote ni sahihi, ishu ilikuwa ni kuthibitisha tu kuwa jina la tatu ni la kwangu pia
nani kakwambia deedpoll ni kubadili jina mimi vyeti vyangu vinamajina mawili nilipoajiriwa ilibidi nichukur deedpol kuongeza jina la tatu lililopo kwenye kitambulisho deedpoll ndio inatambulika kisheria kwenye marekebisho ya majina sio avidavit wakuu mnapotoka
 
Nikuulize swali kidogo, eti kwa nini deedpoll inasajiliwa wizara ya ardhi hali ya kuwa ni majina tu sio ardhi?
 
msajili wa hati na document yoyote kisheria yupo wizara ya ardhi, so iwe hati ya kiwanja ,iwe kusjili majina , iwe kusajili sijui document gani ni wizara ya ardhi sasa wewe jidanganye kachukue iyo avidavit yako kwa mwanasheria kama itatambulika watu wanataka wakiingia kwenye mafaili wakute kweli ulibadili au uliongeza jina na mafail yapo kwa msajili wizara ya ardhi iyo avidavit inaishia kwa mwanasheria uchochoroni
 
Mtafute mwanasheria akuandikie kiapo cha majina cha kukiri jina la tatu ni lako
wabongo mnakua wabishi kuelewa icho kiapo kinaifadhiwa wap kama sio kuishia tu kwa mwanasheria, mwambie akachukue deedpoll kwa msajili wa hati na document wizara ya ardhi
 
Mimi shida yangu sio kubadili jina maana majina yangu yote ni sahihi, ishu ilikuwa ni kuthibitisha tu kuwa jina la tatu ni la kwangu pia
Majina yangu ni kama yako, hamna tatizo lolote.

Labda kama herufi zingetofautiana ndio ungetakiwa kuthibitisha kuwa ni majina yako
 
kwenye ajira serikalini yanatambulika majina 3 , sio mawili kama vyeti vinamajina 2 ni bora kuchukua deedpol ukaongeza jina la tatu yafanane na kitambulisho
 
na

nani kakwambia deedpoll ni kubadili jina mimi vyeti vyangu vinamajina mawili nilipoajiriwa ilibidi nichukur deedpol kuongeza jina la tatu lililopo kwenye kitambulisho deedpoll ndio inatambulika kisheria kwenye marekebisho ya majina sio avidavit wakuu mnapotoka
Kwamba mwajiri alikuambia uongeze jinala tatu?
Mbona wengine hatukuambiwa hivyo.

Watu wengi wana majina 3 kwenye cheti cha kuzaliwa, na cheti cha kuzaliwa ndio kinatumika kwenye kuniandikisha NIDA ambapo NIDA watatoa majina 3 kama yalivyo kwenye Cheti cha kuzaliwa.

Mfano:
Kwenye vyeti vya shule, chuo ni Bundi Ngedere

Kwenye cheti cha kuzaliwa, na NIDA ni Bundi Ngedere Sgr

Hapo hamna tatizo lolote, tatizo litakuka endapo kutakuwa na tofauti za herufi first na second name, mf Vyeti vya Shule, Chuo ni Bund Ngedere halafu cha kuzaliwa na NIDA ikawa Bundi Ngedere Sgr. Hapa patakuwa na utofauti sababu ya kukosekana herufi (i) kwenye jina la kwanza la vyeti vya shule, chuo.

Hapo ndipo itatakiwa hiyo deedpoll
 
wewe
Kwamba mwajiri alikuambia uongeze jinala tatu?AA

wewe ni muajiriwa serikalini au unaongea tu vyeti vyangu vina majina mawili vitambulisho na cheti cha kuzaliwa ni majina matatu ivyo unachukua deedpol kuonyesha ulikua unaitwa john nguya jina la vyeti ila sasa ivi unaitwa jonh nguya adam jina la kitambulisho na cheti cha kuzaliawa angalizo vyeti vikiwa majina mawili kitambulisho matatu hao ni watu wawili tofauti chukua deedpoll haraka usije kujilaum acha ubishi wa apo hamna tatizo wakati unaona kabisa vyeti mawili kitambulisho matatu
 
Mkuu unabisha sana, ila siwezi kukusikiliza sababu sijapata kikwazo chochote jinsi unavyodai wewe, endapo nikipata hicho kikwazo nitafanya hivyo.

Majina yangu mawili yasomeka kwenye vyeti vya Sekondari(Olevel, Alevel), Chuo, Leseni ya Kitaaluma.

Majina matatu yanasomeka kwenye Cheti cha kuzaliwa na NIDA pekee.

Nipo Serikalini na sijawahi kuambiwa nithibitishe kuhusu jina la tatu.

NIDA imetiliwa mkazo kutumika kama utambulisho miaka ya hivi karibuni, watu walioingia Serikalini kabla ya 2015, wengi wao walikuwa na majina mawili na hawana tatizo hadi sasa.
 
Mdau Hivi mfano mimi Katika NIDA naitwa NGEDERE HAMADI NYANI ila katika vyeti vya form4 na chuo naitwa
NGEDERE HAMAD NYANI ,yani tofauti kule jina la kati lina "I" ila huku hamna "I" je apo nahitaji nini cha kufanya ili mambo yakae sawa.
 
kwanza unachanganya kati ya avidavit na deedpoll kinachokibalika sio avidavit maana avidaviti haisajiliwi wizara ya ardhi, kinachotakiwa ni deedpoll sio avidavit
Mdau Hivi mfano mimi Katika NIDA naitwa NGEDERE HAMADI NYANI ila katika vyeti vya form4 na chuo naitwa

NGEDERE HAMAD NYANI ,yani tofauti kule jina la kati lina "I" ila huku hamna "I" je apo nahitaji nini cha kufanya ili mambo yakae sawa.
 
Utofauti wa Kazi ya affidavit na deedpol ni ipi?

Yaani matumizi ya hivi vitu viwili yanatofautiana wapi?
 
Mkuu unabisha sana, ila siwezi kukusikiliza sababu sijapata kikwazo chochote jinsi unavyodai wewe, endapo nikipata hicho kikwazo nitafanya hivyo.

Majina yangu mawili yasomeka kwenye vyeti vya Sekondari(Olevel, Alevel), Chuo, Leseni ya Kitaaluma.

Majina matatu yanasomeka kwenye Cheti cha kuzaliwa na NIDA pekee.

Nipo Serikalini na sijawahi kuambiwa nithibitishe kuhusu jina la tatu.

NIDA imetiliwa mkazo kutumika kama utambulisho miaka ya hivi karibuni, watu walioingia Serikalini kabla ya 2015, wengi wao walikuwa na majina mawili na hawana tatizo hadi sasa.
Daaaaaaah nimejisikia Vibaya Kuona comment yako Bro. Ni Chuo gani hicho kinachotoa Cheti Kwa Majina mawili?
 
MUHAS.

Majima mawili nimeanza nayo form four, wakati naomba boom matokeo/cheti cha form 4 kilitumika(chenye majina 2).

Wakati na apply chuo(TCU enzi hizo), cheti cha form 4 kilitumika, majina 2 yakatumika.

Nilipopata nafasi kwenda Chuo, walinisajili kwa majina 2 kama waliyoyapokea kutoka TCU baada ya kupangiwa chuo na TCU.

Cheti cha kuzaliwa pia kilitumika kwenye stage zote hizo lakini hawakuongeza surname inayoonekana kwenye cheti cha kuzaliwa, walistick kwenye majina mawili.

Chuo baada ya kuni admit wakabaki na majina mawili hivyo hivyo, na waliokuwa na majina 3 nao waliendelea hivyo hivyo.

Majina 3 nayatumia kwa sasa nikiwa kwa mwajiri na sijaona changamoto yeyote.

Swali: Kumbe kuna vyuo vinakataa majina 2 kwa siku ? hili linaweza kuwa kweli sababu ya mfumo wa NIDA ambao unatambua majina 3 na NIDA inatumika sana siku hizi
 
Back
Top Bottom