Je, Afrika tumeshindwa kuwa na demokrasia bila mizengwe ya umafia, fitina, hujuma na rushwa?

Je, Afrika tumeshindwa kuwa na demokrasia bila mizengwe ya umafia, fitina, hujuma na rushwa?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Yapo mambo tunaweza bishana kuwa ama tumefanya vizuri ama tumefanya vibaya; lakini kwenye swala la demokrasia hata anayejifanya kutetea kuwa tunafanya vizuri, ukimwangalia usoni atakwepesha macho kwa aibu.

Kwenye swala la demokrasia nchi zetu nyingi hapa Afrika zivunja moyo. Tukiwa wakweli, Afrika siku utakayoamua kuwa mpinzani wa kweli wa serikali ndio siku utakayoingia kwenye list ya most wanted. Katika nchi zetu nyingi, achilia mbali kukosoa, lakini hata kutoa maoni yako tu kuhusu mambo ya kitaifa tayari unageuka adui.

Hapo Uganda Dr. Kizza Besigye na Robert Kyagulanyi wanashughulikiwa vilivyo na mamlaka za nchi yao. Kwa Gen. Paul Kagame kawaulizie akina Patrick Karegeya, Victoire Ingabire na Diane Rwigara wako wapi. Hapa kwetu ndio tunashindwa hata kuzungumza kwasababu ya doria mtandaoni.

Kuna raha kunapokuwa na siasa huru za ushindani. Huyu anapotoa mawazo haya na mwingine yale ndivyo tunavyoibua mipango mizuri ya kuendesha nchi yetu. Kusema ukweli hata wadokozi wa mali ya umma, wanapoona demokrasia na uwazi umeshamiri wanarudi nyuma. Lakini tunapoua demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, uwajibikaji unaondoka na utawala wa sheria hufa vile vile.

Mimi siungi mkono wapinzani wanaohimiza uvunjifu wa amani na wasiotumia lugha zenye staha kutangaza sera zao, lakini kuwawekea mizengwe ni dalili ya udhaifu. Wananchi watanufaika sana kuwa na CCM kama ile ya Nape na Kinana iliyokuwa inapita kwa wananchi kujibu, kufafanua na kutatua kero za wananchi.

Sisi wana CCM tunapaswa kufahamu kuwa siasa za kuziba watu midomo haziwezi kuwa endelevu. Rais Kikwete aliwahi kutuasa kuacha kutegemea polisi, badala yake tutoke kifua mbele kuyatangaza mazuri yanayofanywa na serikali. Na kama kuna mambo wapinzani wanapotusema yanatuvua nguo, jawabu ni kuacha kuyafanya.

Kazi na utu, tusonge mbele!
 
Shida ya Africa bado ipo kichwani.
 
Zile mila na desturi za mkubwa hakosei na hakosolewi tunazoendelea kuzikumbatia Watanzania na Africa ndo zinazoangamiza hili taifa na bara la Africa kwa ujumla.
 
Zile mila na desturi za mkubwa hakosei na hakosolewi tunazoendelea kuzikumbatia Watanzania na Africa ndo zinazoangamiza hili taifa na bara la Africa kwa ujumla.
Tunahitaji kubadilika! Dhana ya mkubwa hakosei imepitwa na wakati. Tunahitaji kujenga utamaduni wa kuheshimu mawazo ya kila mmoja wetu bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Hivyo ndivyo tutakavyoijenga nchi yetu.
 
Back
Top Bottom