Je, agizo la Rais Samia Suluhu kufuta kesi zisizo za msingi limepuuzwa?

Wale
Seth na Ruge hapana,321b wafutiwe kesi?
Wale ni wahanga wa chuki na ujangili wa bwana yule naona kale kamgao kalimpitia mbali akaamua kulazimisha unyang'anyi na ndio maana Ruge alikataa kukiri makosa. Mwenye ishu no Seth sio Ruge
 

Inawezekana ulimtafsiri vibaya; yeye alisema wasipeleke kesi mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha. Akasema si vizuri serikali kupeleka kesi mahamakani, halafu ikashindwa. Hakusema "nendeni mkafute kesi zisizo na msingi."
 
Piga chini kesi ya uamsho,Seth na Ruge.

Hapo kwa uamusho nakuhakikishia mpaka anatoka madarakani haitafutwa. Hawa waliwekwa ndani kipindi cha JK na si JPM.
 
Hapo kwa uamusho nakuhakikishia mpaka anatoka madarakani haitafutwa. Hawa waliwekwa ndani kipindi cha JK na si JPM.
Sijaelewa hoja yako Ni Nini;
Hata Kama Ni kipindi Cha JK kwani kopindi chake yeye hakuwezi kuwa na makosa?, Pili Ni kwamba mwenye power kwa Sasa Ni Mama Samia (na ameonesha dhamira ya kusimamia haki) na si JK Tena....swali la msingi Ni je ushahidi unatosheleza kuwaimplicate na makosa hayo,na Kama unatosheleza why all that time?kwanini hukumu haitoki? Kama hakuna ushahidi ndipo Mama anapomuhimiza DPP afanye Jambo.
Kumbuka hizi Ni zama zingine na nabii Ni mwingine usishangae kitabu kikawa kingine.
Mfano mdogo kwani Babu Seya si alifungwa kipindi Cha JK? Si ameachiwa na JK si alikuwepo?
 
Mimi hushangazwa sana hii hali kwakweli kama ushahidi haujakilika kwanini watu wanakamatwa na kuwekwa ndani kwa muda mrefu?
 
Hata wiki haijaisha. Mkuu, analysis zinatakiwa zifanyike zaidi. Sio kukurupuka huku unakofikiria.
 
Statement za Jumla jumla huwa ni za kisiasa zaidi..., Msingi inaweza ikawa subjective...
 
Wewe ni nani uwapangie majukumu huoni ni kipindi cha kwaresma?
 
Ushahidi unatosha?Kama ushahidi upo mbona wanavuta miguu muda wote huo?
zile hela walizokuwa wanagawa kwenye viroba mpaka watu wakaita mil 10 hela ya mboga ni za kwao? mbona waliogaiwa walirudisha. watz mbona mnasahau haraka
 

Yes una haki ya kutonielewa maana kweli nimegeneralize kwa comment ya kwanza,pengine niiweke hivi,Swala la Uamsho ni Complicated sana kuliko tunavyofikiri,ni hawa hawa Uamsho kipindi hicho wameshamiri Zanzibar ndiyo kulitokea mauwaji ya Wakristo wengi akewemo Padre mmoja na kumwagiwa tindikali Mabinti wa Kimarekani wakiwa huko kwa Utalii,ni kipindi hicho Uamsho walikuwa wanaendesha mikutano ya kuhamasisha hisia za chuki kati ya Wanzanzibar na huku Bara (kumbuka hapa ni kuhatarisha Muungano).Kama utakumbuka vizuri ni katika hicho Kipindi Serikali ya Marekani ilitoa tamko kali dhidi ya yaliyokuwa yanaendelea Zanzibar na baada tu ya lile Tamko,uamsho wakakamatwa na si tu walibaki Zanzibar bali walihamishiwa Bara kabisa. Kwa muktadha huo swala la Mashekhe wa uamsho liko Complicated sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…