MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wakuu nimetuliza sana akili na kufikiria kauli ya Mbowe kwamba alimwomba aachie ubunge kwa madai kwamba tayari alishamtafutia ajira ya kulipwa USD 15000 kwa mwezi. Kuna maswali kadhaa nimejiuliza nikaona nilete thread hapa huenda tukapata majibu yaliyojaa facts toka kwa wafuasi wa Chama Cha Mbowe na wasio wafuasi;
1. Kwanza kwanini iwe ajira kwa Mdee peke yake? Wengine hawakuwa na umuhimu? Ina maana mwenyekiti ana watu muhimu na wasio na umuhimu kwenye chama?
2. Kwanini amtafutie ajira kwa nia ya kumwachisha ubunge ambapo baadae ingembidi mwenyekiti amweke mtu mwingine? Si angemsamehe bila masharti ya kuachia ubunge kama alishaona shida ya Mdee ni njaa?
3. Kwanini awe na huruma kiasi kwamba amtafutie ajira ya 34m ili kuacha ubunge wake ambao mshahara haufiki hata 20m?
4. Mbowe haoni kama kimaadili inaleta ukakasi na kufanya watu waone nae anafanya kitu kilekile kinachoitwa kununua watu?
5. Je, kwa kauli ya Mbowe kutaka kuhusisha hadi fedha anawapa uhalali wanaosema chuki dhidi ya kina mama 19 imetokana na Mbowe kushindwa kupachika majina yake kwenye viti maalum?
Maswali ni mengi ila hayo yanatosha. Kimsingi hadi sasa hivi kwa upande wangu Mbowe hana tofauti na watu wanaofanya siasa zenye rafu nyingi.