rikiboy
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 21,952
- 43,265
Kuna ndugu yangu anataka kuchukua mkopo. Sasa anaomba ushauri je, ajiunge na SACCOSS apate mkopo au achukue mkopo BANK? Ni mkopo kama milioni 5 hivi
Please ushuari wako muhimu sana
=======
========
Please ushuari wako muhimu sana
=======
Amua mwenyewe.
SACCOS
- Siyo sehemu ya kupata mkopo haraka, maana utahitaji kuwa mwanachama na kujiwekea akiba.
- Sometimes, riba yao yaweza kuwa kubwa kidogo maana kuna SACCOS kibao zinakopa bank.
- Unaweza Kupata Mkopo Bila Dhamana. Akiba yako ndio dhamana yako ( Unaruhusiwa kukopa mara 3 ya akiba yako )
BANK
- Riba Nafuu
- Kukopa Ni Faster Kidogo Kama Umekidhi Vigezo Vyao Hususani Dhamana
========
rikiboy
SACCOS ni sehemu nzuri ya kukopa au mtu ambaye hana vigezo vya kukopa benki; wasichokijua wanachama wa SACCOS in kuwa hakuna mkopo ghali kama wa SACCOS.
Ili upate mkopo wa kiasi fulani lazima na wewe uwe na akiba mfano moja ya tatu ya mkopo unaomba; maana yake sehemu ya mkopo ni pesa yako mwenyewe na unailipia riba.
Ukikopa Shs 6,000,000 kwa riba ya 20% utalipa riba ya TZS 1,200,000
Ukikopa SACCOS TZS 6,000,000 kati ya hizo pesa TZS 2,000,000 itakuwa ni akiba yako hivyo kiuhalisia umekopeshwa TZS 4,000,000 ambazo utalipia riba ya TZS 1,200,000 sawa na 30%. Hivyo aliyekopa benki ana nafuu zaidi