Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
Kumbe omondi ni muislam nilikuwa sijui
 
Mwenyezi mungu hua anajitetea mwenyewewe hatetewi na binadamu wenzetu huwa wanatetea kejeli za dini yao kwakutojua tu
 
Kwenye video ya hate me now ya nas naye yupo msalabani,..ile single iliuza album kiny*ko...acheni upuuzi,yesu hakuwa wa kwanza kusulubiwa msalabani..ebo!!
 
HABARINI! TOKA jana kwenye mitandao ya kijamii Mchekeshaji Erick Omond amejiwa juu na baadhi ya watu kwa kile Alicho Fanya na kuleta mvutano mkubwa sana katika Imani!

Mimi ni mkristo,Lakini sijaona Kosa kwa kile Alichokifanya Erick Omondi! kabla ya Kuja kumuhukumu Erick Omond .....Tujiulize Je Erick Omond ni nani na anafanya nini? ERICK ni Mchekeshaji na anafikisha ujumbe kwa njia ya kuchekesha na kuimba!

Sasa kile alichokifanya ni moja ya uigizaji wake na Lengo lake ni kufikisha ujumbe! Jumbe ulifika tatizo liko wapi? Tujiulize Je mtu akiigiza kama Rais ni kweli anakuwa Rais? au mtu akiigiza Ana maambukizi je kweli anakuwa mayo?

Moja ya watu walio Kuja juu ni baraka De prince Lakini mm sioni kama ni sawa kumuhukumu Eric kwa Alicho fanyaView attachment 442376

Sasa Tujiulize wote Je Alicho Fanya Eric ni Sahihi? Kwangu mimi yupo sahihi

BARAKA de PRINCE NI MWEHU NA MWENDAWAZIMU.., ANAONGEA KITU ASICHOKIJUA KAMA ILIVYOFANYA DIMPOZ BAADAE AKAUMBUKA.. YESU ALIMWAMBIA YULE MWIZI UMESAMEHEWA, NA HICHO KIBAO KINASEMA MWIZI FORGIVEN(mwizi amesamehewa).. sasa hapo kuna tatizo gani..Kweli Watanzania tuna safari ndefu ya mafanikio.. Hivi huyu BARAKA ndio alidanganya Watanzania kwamba ana Nyumba kubwa anajenga akaonyesha kwenye TV, kumbe ile nyumba ni ya mama wa mwanamke anaye-ZINI (anayefanya-naye uasherati)(MAMA NAJMA) .. Baraka ni mtu wa kupuuza tuu
 
Sisi watanzania kila kitu tunajua.......mwacheni mwenzenu apige hela amesomea kazi hiyo hakurupuki unadhani ni Joti yule??
 
Hamuwezi kumpigania Mungu aliyewaumba Ni Mkuu kuliko nyinyi kama huyo kamdhihaki then atamjibu yeye. Nadhani pia hamjaona stand up comedy za mbele nyie wanavyoongelea part za dini kristo ma mengine and wala husikii wakilia huko...Mimi Ni mkristo but kila Mtu atalipwa sawasawa na ya kwake. By the unajua kuwa YESU hakuwa wa kwanza kusulubiwa msalabani!??? Ulikuwa Ni mfumo wa adhabu za warumi enzi hizo
 
Amekosea hayupo sahihi.kwasababu hapo hamuigizi yesu kama mafundisho ila anakejeli.kwani ukiachilia mbali mtu kusulubiwa ila yesu pekee ndio alikuwa na maandishi juu.sasa huyu ameiga af kutengeneza maana mbaya ambayo haifundishi chochote juu ya imani ya kikristo
 
Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
Hata Yesu ambaye ndiye msingi wa imani hii alitukanwa wazi kabisa na yule mwizi pale msalabani lakini hakujibu lolote. Tunaheshimu imani, sawa lakini hakuna funzo lolote katika maandiko linalotutaka kuwahukumu au kuwaumiza wale wanaokejeli imani tofauti na kwa wenzetu. Sisi kwetu tunaagizwa kumsamehe na kumuombea kila mtu. Kwani Mtume Paulo aliua watu wangapi wa Mungu na alisamehewa itakuwa huyu comedian ambaye hakumuumiza yeyote physically?

Yesu alimzuia mmoja wa wanafunzi wake kutumia silaha pale bustanini dhidi ya watesi wake. Na hata mwisho pale msalabani kilichodhihirisha HAKI na UTUKUFU wa mwana wa Mungu ni ile miujiza mikuu iliyotukia baada ya yeye kukata roho na si vurugu zilizofanywa na wafuasi wake.
 
Mzee bahati mbaya sijaishika sana biblia. Nilikuwa naisoma niingiapo katika kipindi dini. Na nilikuwa naingia kwa sababu maalum. Utanisamehe sana. Nilichokiona kwa Bwana Erick ndicho nilichofkiri, kumbe yeye alimaanisha mengine.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
bora hcho kiumbe chenye pumZi kimekaa kwnye msalaba kuliko yale masanamu makanisani....kama ni dhihaka bs ile ndo imezidi na imeandikwa
 
Yesu alisurubiwa katikati ya wezi wawili na wote walikua msalabani. Mi naona katika hio video ni yule mwizi aliesamehewa msalabani. Katumia sanaa kufikisha ujumbe sijaona kosa lake. Nachoona wengi wamechukulia Erick amejifananisha na Yesu. Ila kama ni mfatiliaji utajua ni yule mhalifu aliesamehewa
 
Kosa afanye ERIC OMOND AKIFANYA BRIAN DEACON AU ROBERT POWELL SI KOSA......BARAKA LABDA HAKUTAMBUA BRIAN NI MUIGIZAJI TU KAMA OMOND...ERIC KAPONZWA NA WEUSI WAKE ANGELIKUWA MZUNGU ANGEELEWEKA
3d3d33be202004085c5f5a7ab07a0a58.jpg
 
Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
bible inatuasa kuwa tukae mbali na wenye mizaha. ni kwamba shetani now days mjanja sana anatrick nyingi za kuanza kupotosha maandiko au kuona maandiko ni kitu cha kawaida.
 
Tatizo lipo hapo kwenye hiko kibao yeyote anaweza'fanya hivyo hata wewe unaweza ila hayo maandishi hapo yanakwaza...anamzungumzia nani wakristo tunajua aliyesulubiwa hivyo ni Yesu Kristo na hakuwekewa maandishi yenye maana hiyo huyo hayo kayatoa wapi au kayaweka kama nani?
kweli wewe uliwai tazama hiyo filamu? hakuwa na mwizi tena alisamehewa?
 
Back
Top Bottom