Huyu mzee kuna mazuri na mapungufu aliyoyafanya, kwangu moja ya pungufu kubwa la Mwalimu, ilikuwa kutoheshimu utawala wa sheria na ndilo tatizo kubwa linalotula Tanzania sasa hivi, tumedumaa kiuchumi, kielimu, kisiasa ni kwa sababu ya kutojua kuheshimu sheria wala haki, mbegu za matatizo ya kisheria na hali tuliyonayo sasa aliyapanda yeye mwenyewe no wonder alijua kuwa kuna siku hatutabaki salama,
- Alimuona kwa macho yake Salmin akiiba uchaguzi, akanyamaza akidai eti ameongea na Salmin amemuahidi kuwa ataunda serikali ya mseto, serikali ya mseto my foot! ndio maana leo huko Visiwani hakuna salama, sasa how can one call huu kuwa ni utabiri?
- Utabiri of what wakati ni wewe mtabiri unayeyapanda hayo hayo matatizo yatakayokuja kuleta matatizo halafu you turn arround na kutabiri kwamba matatizo uliyoyapanda yatakuja kuleta matatizo? I do not get it!
Mkuu FMEs,
Hakika mwalimu alikuwa mwalimu kweli.. ebu soma tena maneno yako hapo juu kisha vuta maneno ya mwalimu hapa chini
"Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo"
J.K. Nyerere
Mkuu ni exactly alichosema mwalimu na kinaleta maana kabisa.. Hapa tunazungumzia maneo ya mwalimu ili tuyapime na hali iliyopo, tayari watu wamekwisha ibuka manabii wanaotaka kumhukumu mwalimu...
Mkuu tafadhali, unajua fika kwamba Salmin alipoingia Ikulu ya Zanzibar ni mwaka 1990, mwenyekliti wa CCM alikuwa Mwinyi, iweje leo kweli tuanze kumzungumzia mwalimu ambaye aling'atuka kwa kila makosa ambayo yametokea..Hivi kweli tunaweza kumlaumu Mkapa kwa chaguzi zote za Kikwete kwa sababu tu alikuwa rais kabla ya Kikwete!..
Haya maswala kudumaa kielimu na Kisiasa kweli umeyafanyia utafiti au?.. mkuiu ulikuzwa na mwalimu na tunayaona matunda yake wewe ukiwa mfano mzuri wa somo la mwalimu...inakuwaje leo unaanza na habari kama vile sii wewe mwandishi...Nitakukumbusha tena kuwa hapa JF bado naamini kabisa wanafunzi wa mwalimu ndio shina la elimu zote tunayopata humu....
Mwalimu had power, yes hilo linafahamika lakini mwaka 1990, ni mwaka ambao Mwinyi alianza kuchukua mwelekeo wake..
Kweli yawezekana mwalimu hafuati sheria lakini sii yeye aliyeanzisha vyama vingi na akapingwa na viongozi na wananchi wengi..Je, leo hii kutofanikiwa kwa demokrasia nchini tunaweza kumlaumu kweli Nyerere ati kwa nini alipindisha sheria na matakwa ya wananchi kutokuwa na vyama vingi isipokuwa CCM..
Hivi kweli kama sii kuwepo kwa vyama vingi leo hii mzee wangu FMES ungeweza kusema haya unayoyasema hapa..watu kama Mbowe, Dr. Slaa, Zitto, Mwakyembe, Mama Kilango hawa wote ni matunda ya mwalimu tena basi kama unakumbuka bunge la mwaka 1995 jinsi lilivyokuwa na upinzani wenye nguvu sidhani kama ungefikia kusema haya yote.....
Lau kama kile chama cha NCCR kilichowaunganisha wanasiasa wakongwe kingeendelea kuwepo hadi leo sidhani kama CCM ingekuwa madarakani....sidhani...Lakini tumekuja vuruga sisi wenyewe kwa kugombania hizo ruzuku na posho.. Na CCM wajanja wameweka kiwango kikubwa cha posho na ruzuku za Wabunge ili muuane wenyewe..
Kinachotokea leo sii unabii bali ni manabii wa Uongo, wagombea ruzuku na posho za serikali kwani wenye uchungu husimama imara hata kama wanapingwa na bunge zima.. Na tunawajua!