Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Wasomi wa siku hizi bwana! Eti tuilinganishe Tanzania na Botswana! Population ya Botswana ni nusu ya population ya Dar es Salaam. Ka-nchi kenyewe ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha Madagascar, ina wilaya tisa tu tena ndogo ndogo! Botswana wana dhahabu, almasi nasikia hata uranium wanayo. 'Wasomi' ndani ya JF wanataka tuifananishe Botswana na Tanzania na tumpongeze Rais wa kwanza wa Botswana kwa kujenga democratic institutions na tumponde na kumkejeli Rais wetu wa kwanza kwamba hakuna la maana aliloifanyia nchi hii!
Hizo democratic institutions zinamsaidiaje mwananchi wa kawaida ambaye, tangu 1966 Uhuru wa Botswana ulipopatikana mpaka sasa, anaisha kwa kipato cha dola moja na ushei kwa siku? Kwa utajiri wote uliopo Botswana ukilinganisha na udogo wa nchi hiyo tungetegemea wenzetu wangelikuwa wanaishi kama wako peponi!
Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!
Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?
Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.
Amen.
Najua Vijana wataanza kunicharukia kwa bahati ya kwenda kutibiwa bure! Karibu Prof. Mwakyusa atawaletea Apollo pale mlimani ili sote tufaidi matunda ya tiba ya uhakika. Mwakyusa - a product of Ujamaa wa Nyerere!
Umeongea vizuri sana bibi. Mi nnakuunga mkono asilimia 100. Tufanye kazi! Marehemu alifanya nafasi yake. Na kweli wengi wetu tumesoma kwa sababu ya huo Ujamaa. Bila Ujamaa huo sijui wangapi tungekuwa na mapesa ya kwenda shule. Tuwe na shukraniWasomi wa siku hizi bwana! Eti tuilinganishe Tanzania na Botswana! Population ya Botswana ni nusu ya population ya Dar es Salaam. Ka-nchi kenyewe ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha Madagascar, ina wilaya tisa tu tena ndogo ndogo! Botswana wana dhahabu, almasi nasikia hata uranium wanayo. 'Wasomi' ndani ya JF wanataka tuifananishe Botswana na Tanzania na tumpongeze Rais wa kwanza wa Botswana kwa kujenga democratic institutions na tumponde na kumkejeli Rais wetu wa kwanza kwamba hakuna la maana aliloifanyia nchi hii!
Hizo democratic institutions zinamsaidiaje mwananchi wa kawaida ambaye, tangu 1966 Uhuru wa Botswana ulipopatikana mpaka sasa, anaisha kwa kipato cha dola moja na ushei kwa siku? Kwa utajiri wote uliopo Botswana ukilinganisha na udogo wa nchi hiyo tungetegemea wenzetu wangelikuwa wanaishi kama wako peponi!
Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!
Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?
Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.
Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere ni product ya mkoloni kwa maana kwamba ndiyo waliomsomesha na alisoma wakati wa mkoloni. Lakini Mwalimu hakuwa kasuku wa kumeza ujinga wote wa mkoloni. Hakukubali kuwa indoctrinated. Pamoja na kupata elimu ya mkoloni aliweza kujikomboa kifikra, kuondokana na kasumba ya mkoloni. Ndiyo maana alikuwa "jeuri" kwa hao jamaa. Hakuwaogopa hata kidogo kwenye masuala ya ukweli.Kwa mtaji huo Nyerere ni product ya mkoloni. Hivyo tushukuru wakoloni kwa kutusomeshia watu wa mfano wake.
Naona sasa tupo kwenye masuala ya syntax na semantic. Katiba ya sasa haina tofauti kubwa na ya wakati wa chama kimoja.
Labda kama unazungumzia katiba ya CCM.
Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!
Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?
Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.
Nimesoma kwa makini sana ulichokiandika. Nilichoshindwa ni kuelewa msimamo wako katika issue nzima inayozungumziwa.
Kwanza umemsema Dikteta Mjamaa Nyerere na vita yake dhidi ya utajiri. Baadae ukaongelea faida za dikteta huyo huyo kwa watoto wa wakulima wa vijijini waliopata elimu na kusababisha wajukuu zetu kufaidika nayo. Je, ni Dikteta huyo huyo mwenye kutoa haki namna hiyo?
Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere ni product ya mkoloni kwa maana kwamba ndiyo waliomsomesha na alisoma wakati wa mkoloni. Lakini Mwalimu hakuwa kasuku wa kumeza ujinga wote wa mkoloni. Hakukubali kuwa indoctrinated. Pamoja na kupata elimu ya mkoloni aliweza kujikomboa kifikra, kuondokana na kasumba ya mkoloni. Ndiyo maana alikuwa "jeuri" kwa hao jamaa. Hakuwaogopa hata kidogo kwenye masuala ya ukweli.
Lakini cha zaidi ni kwamba alitufundisha watanzania pia kuondokana na kasumba ya ukoloni. Unakumbuka maneno aliyotamka mwalimu baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar kugoma miaka ya 60 wakisema afadhali enzi za mkoloni?
Kutokana na fikra za Mwalimu watanzania tuko huru kwa kiasi kikubwa kutokana na kasumba ya ukoloni kuliko - naamini - mataifa mengi jirani zetu.
Umeongea vizuri sana bibi. Mi nnakuunga mkono asilimia 100. Tufanye kazi! Marehemu alifanya nafasi yake. Na kweli wengi wetu tumesoma kwa sababu ya huo Ujamaa. Bila Ujamaa huo sijui wangapi tungekuwa na mapesa ya kwenda shule. Tuwe na shukrani
Recta,
Kwa ubongo wangu wa ndege ni kuwa umeshindwa kumwelewa Bibi Ntilie alivyotumia neno dictator. angalia alivoliweka katika ya hizo mark. Bila shaka alikusudia kusema kama mnamwita dictator au ni huyohuyo dictator. Ni uandishi tu. Au wakati mwingini ni sarcasm. Upo mkuu hapo mkuu wa seminary?
Mkuu Zakumi, Katiba ya sasa ina mabadiliko mengi sana ukilinganisha na Katiba ya wakati wa Nyerere. Kuna vifungu vilivyofutwa na vingine vilivyoongezwa. Kwa mfano,
1. Katiba ya chama kimoja haikuwa na Tume ya uchaguzi
2. Katiba ya chama kimoja haikuwa na vyama vingi
3. Katiba ya chama kimoja ilimsema Makamu wa Rais kuwa ni Rais wa Zanzibar
Na kadhalika. Ukitanua wigo huo hapo juu tu, utagundua kuwa Katiba imebadilika sana.
Ila ni kweli kuwa Katiba hii ya sasa inakipendelea zaidi chama tawala.
"Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo" J.K. Nyerere
Katiba ya Tanzania haikubadilika. Mabadiliko ya katiba ya sasa ni sawa kamati ya olimpiki duniani kufuta olimpiki ya walemavu. Na baadaye kuwashauri wanariadha walemavu (vyama vya upinzani) na kushiriki kwenye olimpiki proper pamoja na wanariadha wasio walemavu (CCM).
Zakumi,
Mkuu wewe kiboko yaani umezungukwa na watu woten hawa bado unahema... ama kweli mwenzangu Bepari.. sijui kama unaujua ubepari maanake kila naposoma unamlaumu Nyerere na unashindwa kuelewa maelezo ya watu wengine..
Mkuu wangu nimemtumia Hitler kuonyesha jinsi haki na sheria inavyoweza kutafsirika iwe kwa mabaya au mazuri kinachotakiwa ni kusimamisha ili kulinda haki na amani ya wananchi wako. Na nimesema wazi kwamba kosa la Hitler ni pale alipotaka kuitawala dunia lakini within Germany huyu Hitler alionekana kuwa kiongozi bora kama kina Churchill, Washington, Lincoln,Trudeau, Mao tse tung na hata huyo wa Botswana..Kila mmoja wao alichofanya ni kusimamisha sheria iwe ya Kidikteta au Demokrasia lakini wote ktk mitazamo wayo ni ktk malengo ya kusimamisha haki na amani baina ya watu. wake. Umeona mwenyewe Saadam ambaye alikuwa dikteta na uchafu wqote aliofanya lakini sasa hivi nchi imewashinda.. Demokrasia imeshindwa kufanya kazi kabisa...
Nitarudia tena kukwambia kwamba Huwezi kumlinganisha Nyerere na rais wa Botswana hata kidogo... Mimi nimekaa pale Gabarone ni mji mdogo kuliko hata mji wowote wa mikoa ya Tanzania. Nchi nzima ina watu wasiozidi millioni mbili tena wanaishi ktk robo ya eneo la nchi hiyo sehemu zingine zote ni jangwa..
Sasa ikiwa nchi inaingiza mara tatu ya kipato cha tanzania na una population ya watu wa wilaya ya Temeke utashindwa vipi kuiendeleza nchi hiuyo.. Kifupi wWabotswana wanaibiwa vibaya sana kuliko sisi, mabillioni kwa mabillioni yanaibiwa na hawa viongozi wao kila mwaka.. kwa sababu uchumi wa nchi hiyo ni ziada kila siku ya Mungu..Yaani raia wao anaweza kugawa dollar millioni kwa kila raia na fedha ikabakia..That's how rich they are!..Lakini ukweli ni upi?.. Botswana bado wapo bado ktk nchi maskini! ni miaka ya hivi karibuni tu ndio kidogo unaweza kuona mabadiliko hata Gabarone penyewe na sii ya hivyo ukalinganisha na Dubai au Kuwait..
Kuhusiana na katiba, Mkuu sheria ya vyama vingi imeandikwa kabla ya vyama kuzinduliwa hivyo huwezi kusema ni Olimpiki ya walemavu wakati hapakuwepo na walemavu kabla ya.. Ni matusi makubwa sana unayatumia hapa.. na yote haya yanatokana na kushindwa kupata jawabu la matatizo tuliyokuwa nayo. Unachofanya ni kutafuta mchawi... yaleyale ya Miafrika ndivyo tulivyo!.. hapa Unaua albinos tu...
Zakumi, inaelekea umesoma Katiba moja tu (ya chama kimoja , kabla ya 1992), au umesahau moja ya Katiba (ya awali) ama hujasoma zote mbili (ya chama kimoja na ya vyama vingi - 1992). Nakushauri ujaribu kutafuta muda uzisome zote mbili halafu uje kujenga hoja hapa.
Mimi sioni lolote linalohusiana na mwongozo wa Nyerere katika utawala wa nchi yetu tangu tuvunje Azimio la Arusha na maazimio mengine yote, tangu turekebishe Muungano (kikatiba), tangu tubadilishe mwelekeo wa kiuchumi wa Taifa na tangu tuanze sera mpya za ubinafsishaji, biashara huria na kuingia kichwa kichwa kwenye globalization (bila kuielewa kwa kina na kuiandalia makao yake katika jamii yetu).
Zakumi, nchi hii haiyumbi kwa kuwa Nyerere aliamua hivyo. Nchi hii ilikuwa imara wakati wake. Sheria zilikuwa msumeno, viongozi walikuwa waadilifu zaidi na wananchi walikuwa na usawa wa wastani kuliko sasa. Sera zozote zilizokuwepo zilitekelezwa bila kujali eneo, rangi ya watu, uwezo n.k. WaTanzania walikuwa waTanzania wa kweli japo masikini.
Hivi sasa tumebadili mwelekeo kiasi kwamba, ili tuweze kurudi hadi pale alipotuachia Nyerere, tunahitaji kupigania uhuru upya. Na ni baada ya kufanya hivyo ndipo tunaweza kujiendeleza tena na kufika kwenye ustaarabu tunaoutaka. Kuna njia panda ambayo tulikosea kuchagua upande wa kupita na sasa tumepotea. Lakini tatizo letu si kukosea njia tuliyopita baada ya kufika njia panda, bali ni kuendelea kujidai hatujapotea na kuendelea na safari yetu hadi tutakapopotea zaidi na kushindwa kurudi tulipotoka.
Hilo ndilo linalotia hofu kuu.