Mkuu Zakumi, nchi haiongozwi na Katiba. Nchi inaongozwa kwa Katiba. Nchi zote duniani zinatakiwa kuongozwa na wanadamu kwa kutumia Katiba. Katiba ni kifaa cha maongozi, ni program inayotoa muongozo. Katiba zote hutungwa na wanandamu, hivyo hubadilishwa na wanadamu kila inpobidi. Katiba inaweza kutumiwa na viongozi na vile vile inaweza isitumiwe na viongozi hao hao. Inapotokea kuwa viongozi wanaacha kutumia Katiba, wananchi wakiwa na uwezo wa kutosha, wanaweza kuilaumu/kuishitaki/kutoichagua na wakati mwingine hata kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Tukirudi kwenye mchango wako mzuri uliotanguliwa na maneno hayo hapo juu, ni wazi kuwa Katiba aliyoitumia Nyerere na Katiba inayotumiwa hivi sasa zina tofauti kubwa (baada ya mabadiliko ya 1992). Wakati wa Nyerere, hakukuwa na vyama vingi vya siasa, na vile vile Muungano ulidumishwa kwa namna ya tofauti na sasa.
Katiba hii, ambayo ndio muongozo wetu, inaweza kubadilishwa wakati wowote na kuchukua sura tofauti kabisa kama viongozi wenye dhamana ya kufanya hivyo wakiamua kuchukua hatua za kufanya hivyo.
Mimi naamini kwa dhati kabisa kuwa Nyerere hana mkono wake katika yanayotokea hivi sasa nchini (japokuwa viongozi wetu wanataka tuamini kuwa wanamuenzi Nyerere katika kuendesha nchi).