Je, aliyewahi kuacha kazi anaweza kuomba tena kazi na akapata?

Je, aliyewahi kuacha kazi anaweza kuomba tena kazi na akapata?

mwenye shamba

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
978
Reaction score
1,766
Wakuu kwema?

Wayback kidogo bro wangu aliajiriwa serikalini sekta ya afya huko mtwarwa, alifanya kazi kwa miaka 3 na akaacha kazi kwa sababu anazozijua yeye. Baada ya muda kupita maisha yamemnyoosha vilivyo,nimeona juzi anadai amefanikiwa kutuma maombi

Swali; Je, anaweza kuajiriwa tena?
 
Wakuu kwema? Wayback kidogo bro wangu aliajiriwa serikalini sekta ya afya huko mtwarwa, alifanya kazi kwa miaka 3 na akaacha kazi kwa sababu anazozijua yeye. Baada ya muda kupita maisha yamemnyoosha vilivyo,nimeona juzi anadai amefanikiwa kutuma maombi,swali je,anaweza kuajiriwa tena?
Kama alipata Check no na akawa anapata Mshahara Ni ngumu kupata tena kwa utaratibu wa Kawaida.

Hata akichaguliwa, akifika kwenye Halmashauri atakayopangiwa ATAKWAMA.

Screenshot_2022-04-28-17-53-31-161_com.adobe.reader.png
 
kwani huko kazini bado anaonejana mtoro au washamfutilia mbali,halafu unapisa maisha yamemnyoosha unamaanisha nini kwamba anashindia mihogo kama marehemu dokta Shika
 
Akinahatika kupangiwa kituo cha kazi, mwajiti atamuombea kurejeshwa utumishi wa umma na kuendelea kutumia check nba yake.
Hayo maombi yanaelemezwa ofisi ya katibu mkuu utumishi. kuna utaratibu atapitia ikiwa pamoja na kufanyowa vetting na kitengo cha usalama wa serikali(GSO) kuona kama bado ako na sifa za kuwa mtumishi wa umma, then taarifa yake ndio itawaongoza kama karibu mkuu kiongozi ampatie kiabali ama la!
Ni mchakati mrefu saa kwa kweli na unatka moyo sana , unaweza kutumia miaka miwili ama hata mitatu mpka kurejeshwa.
 
Unaacha kazi ya laki 6 serikalini unakimbilia million 1.5 ya private kwa mkataba wa miaka miwili matokeo yake ndio haya.
Watu ni wapumbavu sana, wanataka mafanikio ya haraka kisa eti serikalini mishahara midogo.
 
Akinahatika kupangiwa kituo cha kazi, mwajiti atamuombea kurejeshwa utumishi wa umma na kuendelea kutumia check nba yake.
Hayo maombi yanaelemezwa ofisi ya katibu mkuu utumishi. kuna utaratibu atapitia ikiwa pamoja na kufanyowa vetting na kitengo cha usalama wa serikali(GSO) kuona kama bado ako na sifa za kuwa mtumishi wa umma, then taarifa yake ndio itawaongoza kama karibu mkuu kiongozi ampatie kiabali ama la!
Ni mchakati mrefu saa kwa kweli na unatka moyo sana , unaweza kutumia miaka miwili ama hata mitatu mpka kurejeshwa.
Ahsante sana, bilashaka hata wewe unaweza ukanisaidia waraka niliomuomba MosesKing hapo juu.
 
Watu ni wapumbavu sana, wanataka mafanikio ya haraka kisa eti serikalini mishahara midogo.
Hiyo inaitwa short term pleasure for longterm painfully vijana wanataka walale masikini waamke tajiri
 
Mkuu vipi, unao waraka unaoelezea utaratibu wa kurejea ktk utumishi wa umma baada ya kuacha kazi?
Sina mKuu, mara nyingi nyaraka huwa zinaishia kwa maafisa utumishi
 
Mke wa jama yangu alikimbia kazi kwa zaidi ya miaka miwili(Mikopo ilimzidi akatoroka), baada ya mda maisha yakampiga sanaa....

Mwaka juzi akaanza process za kurudi, alirudi kituoni kwa kufanya kazi kama Mwaka hivi bila malipo, January mwaka huu akarudishwa official.
Sijui imekuaje ila inaonesha kuna hela Ndefu alipewa, maana ndani ya mda mfupi tuu akajenga na mambo mengi, na Sio mkopo tena.

Sasa nashindwa kujua, jee alipewa ya kipindi chote alichokua mtaani au ni ule mwaka aliofanya kazi bila malipo..
BTW baada ya kurudi kazini, walitema ndio akawa anamringishia nyumba n.k.

Yeye ni Mwalimu, kwahio kuna namna inawezekana, process ndio sijazijua.
 
Back
Top Bottom