Je ALLY MAKOA ni nani haswa!!!?

Je ALLY MAKOA ni nani haswa!!!?

1120ulimwengu

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
252
Reaction score
422
Habari wakuu!Naomba kupata CV na biography full ya mbunge ALLY MAKOA ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya maadili,haki na madaraka ya bunge.Nadhan ni vizuri kumuelewa bwana huyu kwakuwa wenyeviti kadhaa wa kamati hii waliopita walijitahidi sana kulinda majina yao katika maamuzi kama George Mkuchika,Emmanuel Mwakasaka nk.
Maspika wamekuwa wakiitumia kamati hii kuadhibu,kudhalilisha na kutweza utu wa wasema ukweli.Job Ndugai aliitumia kamati hii kumtweza CAG wa wakati huo Prof.Mussa Asad kwa kusema bunge ni dhaifu akirejelea udhaifu wa bunge kutochukua hatua juu ya ubadhirifu uliobanika kwenye ripoti.Pia alifanya hivyohivyo kwa Halima Mdee kwa eti kuunga mkono maneno ya Asad!Ndugai pia alimtweza Makonda kwa kumuita katika kamati hyohyo kufuatia kauli yake kwamba wabunge husinzia bungeni(kitu ambacho actually hata mtoto wa darasa la tatu anajua wabunge husinzia bungeni)!Wenyeviti wa wakati huo at least walikuwa na soni..huyu Makoa anaonekana ni pushover sana kufuatia sakata la MPINA.Naomba kumfaham
 
Hata member mwenzetu mmoja aliwahi kukaangwa na hiyo kamati ya ndugai Pascal Mayalla mpaka leo ni siri yake kilichomkuta huko!
 
Ni kweli mambo niliyokutana nayo huko ni siri yangu na kamati, ila siri nyingine ni za ki uzalendo tuu, kama unapokutana na dingi wako kona fulani, huwezi kumwambia maza, kutawasha moto home, halafu baadae unakuja kukuta kimefyatuliwa ki foto copy na dingi utadhani kajizaa, by that time dingi ni mstaafu, fungu limekata!, unajikuta unawajibika kusaidia school fees ya hako ka copy, bila kutoa siri ya dingi!, ila dingi ana taarifa zako unavyo okoa jahazi kimya kimya na anakuheshimu kwa hilo!.

Kile nilichoitiwa, kilipokutwa ni kweli tupu, inabidi Bunge linyamaze, na mimi kwa uzalendo, nimenyamaza kimya kulinda na kutunza heshima ya mhimili.
P
 
Alikuwa Mtumishi wa CCM makao makuu, amegombea mara kadhaa huko kwao Kondoa akakosa until 2020 akapata. Kuhusu CV siifahamu hayo ni mambo ya afisa mwajiri wake.

Ni mtu wa kawaida tu. Labda anafanya hayo kujihakikishia anajichimbia mizizi zaidi kwenye "system ". Ubunge una leo na kesho, hata ukianguka unahakikisha "watu" hawakusahau kwa kazi iliyotukuka waliyokutuma ufanye.
 
Back
Top Bottom