Je,ana haki ya kunishitaki?

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Habari WanaJF,Poleni na majukumu ya kujenga taifa.
Mimi ni mhitimu kutoka chuo kimoja hapa nchini.Nikiwa likizo ya mwaka wa kwanza nilienda likizo kijijini kwetu,kule nilikutana na mdada katika mazingira ya kutofikiria kabisa nikalala nae.Bahati mbaya alipata ujauzito,huyo dada wakati ule ndo alikua amebakiza miezi miwili kuanza NECTA form four.Aliniomba hela ili aitoe ile mimba mimi nilikataa coz nilidhani mambo ndo yangeharibika zaidi kwa sababu anaweza kufa wakati wa kutoa mimba.Yule dada alipoona simpi hela ya kutolea mimba,alijitahidi akafanya mtihani mpaka akamaliza,baada ya kumaliza alitoka kwao na kwenda kuishi kwa wazazi wangu,mimi baada ya kuona hivyo nilikaa kimya tu coz ile mimba ilianza kuhudumiwa na wazazi wangu.
Mwaka juzi alijifungua salama akiwa kwa wazazi wangu,kusema ukweli yule dada sikua nimejiandaa kuishi nae,lakin baada ya kumpa ujauzito na akijifungua nikaona nimwendeleze kielimu kupitia resources za kwao coz kwao wanauwezo zaidi kuliko kwetu,tulielewana vizuri na tukakubaliana ila nikamwambia kua mimi nakusaidia kusoma tu ili upate upeo mpana wa kujitegemea na kupambana na changamoto za maisha yako hapo mbeleni lakin mimi sikuoi saiv kwa sababu halikua tegemeo letu! cha ajabu aliposikia hivyo alikataa kwenda shule na kung'ang'ania kwa wazazi wangu huku akidai haendi shule et nitamwacha.
Baba yake pia anatishia kuishitaki familia yetu na kudai fidia ya miaka aliyokaa mtoto wake kwetu,kiukweli mi najitahidi kugharamikia matunzo ya mtoto ila yeye nimesitisha kumhudumia na simtaki tena coz yeye hataki kwenda shule.Tatizo nalo hofia saivi baba yake akianzisha kesi,je anaweza anakanitia hatiani? Toka mtoto wake apate mimba mpaka leo sijawahi kurundi nyumbani na sijaonana nae kwa miaka mitatu mfululizo.
Naomba ushauri wa kisheria km ana haki ya kunishitaki kua nimekataa kumuoa kwa hiyo nimlipe fidia au la,ahsanteni na omba mawazo yenu jamani.
 
mimi cmwana Sheria ila naww Elimu yako cdhani km imekusaidia kusoma Uelewa wa huyo Mzazi mwenzio kitu cha kwanza Ulitakiwa ujue kwanini kahamia kwenu Ukichukulia kwa maelezo yako unasema kwao maisha ni Mazuri so Tatizo umelifanya liwe kubwa 7bu ya HASIRA umeenda SHULE umekutana naVISTER du! umeona dawa ni kumlipkia huyo wa hom Inategemea wazazi wako wakati wanampokea kulikuwa na Makubaliano gani? Nway ngoja tusubiri wenye fani yao,,!
 
Ungewauliza wazazi wako. Haya mayai ya kisasa yanawadumaza mnachelewa kukua!
 

Mkuu sijapata visista hata kidogo lakini huyu dada yeye kila nikimshauri mambo ya kwenda shule hataki kabisa,kisa et ntamwacha,sasa mtu wa hivyo asiyewaza mambo ya mbeleni nawaza kusaidiwa as mwanaume ndo kila kitu,hata km nikimkubalia mawazi yake kua akae tu,je,ikitokea siku mmoja nikatangulia mbele ya haki atajitemeaje km saiv kashindwa?
 
Wewe huna akili na hapa nakuombea upate mabalaa na ikiwezekana usizae kabisa liwe fundisho na naomba tena babamtu asikushitaki ila akuloge ukome kabisa kuchezea watoto raha kuoa hamna na elimu yako bure
 

Dawa ni kuoa tu hili halikwepeki,inabidi tuwe responsible for our actions na sio kukimbia matatizo tena you lucky coz wazazi wako wanamwangalia mtoto
 
Wakati unamto..mba bila kondomu hukufirikiria swala la mimba na usomi wako?
alafu unasema humpendi uliwezaje kutia mimba usiyempenda au kwa kuwa hajafika chuo kama wewe?
msalaba ni wako na huyo msichana ana mtoto wako ambaye ni damu yako usiache wateseke anza naye maisha
 
nashindwa kuelewa hvi ni lazima msichana uliezaa nae umuoe huyo huyo??
 
Dawa ni kuoa tu hili halikwepeki,inabidi tuwe responsible for our actions na sio kukimbia matatizo tena you lucky coz wazazi wako wanamwangalia mtoto

Mkuu sijakimbia majukumu hata kidogo,mtoto mpaka saiv nahudumia hata yeye wakati nikiwa na boom nilikua namsave sana,ila baada ya yeye kugoma kwenda shule amenikatisha tamaa sna coz namwona anamawazo tegemezi sana
 
Mkuu sijakimbia majukumu hata kidogo,mtoto mpaka saiv nahudumia hata yeye wakati nikiwa na boom nilikua namsave sana,ila baada ya yeye kugoma kwenda shule amenikatisha tamaa sna coz namwona anamawazo tegemezi sana

Mpe an alternative to raise some income kutokana na mazingira anayotoka mkuu.Kama hataki shule usimlazimishe
 
Mpe an alternative to raise some income kutokana na mazingira anayotoka mkuu.Kama hataki shule usimlazimishe

Mkuu nimekuelewa lakini nimejaribu kufanya kila altenative za kumsapoti,mathalan,nilijibanaga mwaka jana nikamkodishia shamba bt cha ajabu alipopata mazao na kuuza alianaza kumnunulia vitu vusivyo vya maana mama yake!
Pia kuna siku aliniombaga nimnunulie simu lakin cha ajabu ile simu alimpa mama yake....ki ukweli kila nikiwaza nachoka mkuu mwishowe nita-apply umafia tu.
 
Hamna just be patient with her Huyu ni mama hupaswi kushindana nae,huwa wanapenda sana mama zao hata wa kwangu yuko hivyo.Just accept her na ayafanyayo na mrekebishe taratibu tu
 
Ujielewi wewe cheza na vyote ila c mwanamke.

wap nsipojielewa ndugu... sijajua concept ya kuzaa na ndoa wangap wamelelewa na baba au mama ambao sio biological parents ina maana nao hawajajielwa....
 
peleka jukwaa la mapenzi wakina king'asti wakushauri..
 
Mie naona kama wamtafutia sababu tu msichana wa watu. Reason ya kumwambia kwenda shule ilikua ni nini? (urudie mwenyewe kusoma hapo juu)
Na sasa unasema humtaki sababu hataki kwenda shule!!!!
Mbona inaonyesha wazi? Ulitaka kumchezea mtoto wa watu. Ana umri gani huyo msichana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…