Mwanzo Aristotle alikuwa ni msusi wa wanawake, baadaye akajiongeza kuuza weaving na wigs na wateja wake walikuwa ni mastar wakubwa na celebrities wa Tanzania wa hapo Dar-es-Salaam. Aliupata umaarufu kwa jinsi alivyokuwa akitangaza biashara yake kupitia Mtandao.
Mara ghafla akaamza kuwa chawa wa Diamond na Uwoya, lakini ukimsikiliza Kiswahili chake ni kama kina lafudhi ya Wakongo kabisa, ambao wengi walifika Dar kwa kazi ya kusuka na kuwaremba wanawake pamoja na kunengua na kuimna miziki ya dansi. Ametumia mtandao wa Instagram na TikTok kuonesha ukwasi wake na jumba lake la kifahari kubwa sana na zuri.
Swali langu ni kwamba, Aristotle ndie chawa tajiri Tanzania ambae ana asili ya Congo ama ni Mkigoma tuu? Uchawa unalipa nami niuanze? Hawa ndio influencers ambao Mh. "Zakayo" kutoka Burundi alisema wataanza kulipishwa Kodi?
Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app