Je, Aristotle ndie chawa tajiri Tanzania? Je, ni Mtanzania?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225


Mwanzo Aristotle alikuwa ni msusi wa wanawake, baadaye akajiongeza kuuza weaving na wigs na wateja wake walikuwa ni mastar wakubwa na celebrities wa Tanzania wa hapo Dar-es-Salaam. Aliupata umaarufu kwa jinsi alivyokuwa akitangaza biashara yake kupitia Mtandao.

Mara ghafla akaamza kuwa chawa wa Diamond na Uwoya, lakini ukimsikiliza Kiswahili chake ni kama kina lafudhi ya Wakongo kabisa, ambao wengi walifika Dar kwa kazi ya kusuka na kuwaremba wanawake pamoja na kunengua na kuimna miziki ya dansi. Ametumia mtandao wa Instagram na TikTok kuonesha ukwasi wake na jumba lake la kifahari kubwa sana na zuri.

Swali langu ni kwamba, Aristotle ndie chawa tajiri Tanzania ambae ana asili ya Congo ama ni Mkigoma tuu? Uchawa unalipa nami niuanze? Hawa ndio influencers ambao Mh. "Zakayo" kutoka Burundi alisema wataanza kulipishwa Kodi?

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Ni Mkongo, swali la kuuza ni je, ana sifa za kumiliki ardhi nchini Tanzania?
 
Muhimu kama sio mtanzania tujue bayana. Hao hawakawiagi kugombea ccm hata ubunge. Kuna yule mkenya alijiingiza tz akapiga hela hadi kua mwenyekiti wa chama cha mpira nchini na kujipa jina alhaji fulani😂. Alipoingia matawi hatakiwi ndio wakamvua mask na kumu escort hadi namanga wakamdump pale akaingia zake nairobi na kutokomea.🚶🏼‍♂️🚶🏼‍♂️🤣😆
 
Mimi najua nyumbani kwake anapoishi. Maeneo ya mapinga. Nyumba ya kawaida tu self ya vyumba vitatu

Hawa wasanii unaweza ukafaka kihoro kwa vitu wanavyopost kujifanya vyao ,kumbe pale wanafanya matangazo ya nyumba au vitu ,maana wakishapost kuna watu wanaenda inbox kuuliza kama anauza.

Yaani Mfanyabiashara ana ofisi ya kontena 20 feet pale warioba Mikocheni awe tajiri? Si angeingia tu Palm Village akodishe floor nzima afanye ofisi yake?
 
Nadgani tunapaswa kubadili mindset zetu kuhusiana na haya mambo


So long as hajavunja sheria, basi tumuache na ukwasi wake.

Sisi tuahangaikie vyanzo vyetu vya uchumi tuweze kujikomboa
 
Endeleni kushupaza shingo eti sio nyumba yake...
Tafuteni hela siku hizi kuishi nyumba nzuri wtt kusoma vizuri kula vzr kuendesha gari zuri ndo maisha ya kijana wa kisasa tena katika umri mdogo..unafaidi maisha ukiwa na nguvu zako...cha msingi ni kipato halali na kisiwe kipato cha kujitoa utu wako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…