Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Swali hili nauliza kwa sababu kuna jamaa anasema hivi, nitanukuu ila baadhi ya sehemu za majina nitaficha
"Tulipokuwa JKT Afisa mmoja wa jeshi ambaye ni moja ya viongozi wakuu wa kambi ile alitembelea na kigari chake akatusalimia kisha muda wa kuondoka akamwambia yule mwalimu wetu anayetupa mafunzo kwamba asitupe mafunzo makali sisi wa kwa mujibu jamaa (yule afande aliyepewa maagizo) akaitikia vizuri
Alipoondoka yule kiongozi huyu afande akawa anaendelea kutupa mazoezi na hakufanya mabadiliko yoyote katika mazoezi tunayofanya kila siku. Pale kambini kuna miti mingi basi tukawa tunaambiwa tusimame kwa mikono iliyokunja ngumi miguu ikiwa imetundikwa kwenye ile miti huku tunaamrishwa kuimba sauti zenyewe hazitoki basi tu
Basi bwana kumbe yule afande (kiongozi mkubwa) siku hiyo kaja kwa kunyemelea kapaki kigari chake mbali uko akaja kwa mguu mpaka pale ndo akatukuta katika hali hiyo ya mazoezi aisee alimshika yule afande akampiga, piga sana huku akimuongelesha kwa nini hafuati kile alichomuagiza.
Yule afande (mwalimu wetu) alipigwa mpaka nikaingiwa na huruma aisee tena yeye ni mdogo kiumri na mfupi halafu yule mkuu ni tolu balaa kwahiyo ukiangalia unaweza kusema ni baba anampiga mwanwe"