Wakati Atheists wanakiri hadharani kwamba akili zao zimeshindwa kuielewa dhana ambayo wao wameibatiza jina na ku iita " The problem or Evil" , Watu wanao amini kuhusu uwepo wa Mungu nao wana ielezea Atheism kama " The Problem of Atheism"
Kwanza kabisa Haya yote ni mawazo yako tu, Theist kwa ujumla hawana maelezo kama haya.
Huwezi/hamuwezi tegua epicurean paradox kwasababu kuu moja tu na si vinginevyo.
Sababu yenyewe ni kwamba habari ya Mungu mnayeamini ni story ya uongo tu, na si vinginevyo.
But tofauti na Atheists ambao akili walizo pewa na Mwenyezi Mungu wameshindwa kuzitumia vizuri kuielewa dhana ya " The problem of Evil" ambayo kwao( kwa viwango vyao vya ufahamu) inabaki kuwa mystery, Theist wao tayari wameshapata majibu ya tatizo la Atheism( The problem of Atheism)
To the Theists, Atheism ni tatizo la afya ya akili..
Unaposema kwamba atheist wamepewa akili na Mwenyezi Mungu unakuwa unafanya upuuzi mmoja mkubwa sana pasipo kujitambua.
Yan unatumia dhana ambayo unapaswa kuiprove katika kujenga hoja za kuwaelezea watu hao hao ambao wanakutaka uprove.
Hapo unakuwa kama hauelewi unachokifanya
Siwezi kukataa wala kukubaliana moja kwa moja na hoja hii ya hawa Theists lakini ninacho weza kusema ni kwamba Atheists ni watu wasio penda kuumiza vichwa vyao.
And vice versa is true.
Theist hupenda jibu jepesi, hawataki kuumiza vichwa kuchanganua mambo.
Asilimia kubwa ya atheist kwanza wanaelewa dini, wanajifunza na mambo mengine mengi tu ikiwemo science.
Wanapenda kudadisi kwa kina mambo kuhusiana na Cosmology.
Theist wao wanakuwa kwenye illusion ya imani za wazazi wao.
Hawawezi kuhoji mambo kwa kitisho cha kukufuru.
Hawawezi kukubali kujifunza kitu tofauti na imani walizopewa tangu utotoni.
Theist (hasa Abrahamic) are lunatics.
Walipo ndipo wamefika.
To me Atheism is just an escape root. They are escaping their responsibility . The responsibility to give answers. So by resorting into just saying there is no God, they are just escaping their responsibility through imagination.
Hawana tofauti na Adam alie ulizwa a very simple question " have u eaten the forbidden fruit"? " Ni huyu mwanamke ulie nipa"
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuleta habari za Adam as if ni true.
Huwezi kuthibitisha habari za Adam kwasababu ni habari za uongo.
Yan umekubali habari za Adam?
Na unazitumia kujenga hoja hapa?
Tutaamini vipi kama ni kweli kama huwezi kuthibitisha habari hizo, wala kumthibitisha Mungu kama yupo?
Huoni kama unatumia uongo katika kuutetea uongo mwingine?
Wanakwepa jukumu la kutoa majibu ambayo Mungu amewauliza wanadamu.
Kabala ya kauli hii unapaswa kuthibitisha Mungu yupo.
Unapotoa hoja kwamba Mungu hayupo kwa sababu eti Mungu mwenye upendo wote mwenye nguvu zote na mjuvi wa yote hawezi kuruhusu watu wake wateseke ni sawa na mtu anae sema " Huyu si baba yangu kwa sababu amenitesa na ana mtesa mama yangu " majibu ya kitoto kabisa.
Mkuu naomba tuelewane,
Unaposema Mungu kaumba vyote, pia ukasema Mungu huyo ni muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, then tukashuhudia mabaya kwenye hii dunia.
Hapo tyari unakuwa umejipinga mwenyewe.
Mungu huyo kwa uwezo wake angeweza kuumba ulimwengu usiowezekana kabisa kutokea kwa mabaya ili kulinda sifa yake ya upendo.
Sasa kulinganisha na habari ya baba yangu sio sawa.
Baba yangu si muweza wa yote,
Si mjuzi wa yote
Na wala hana upendo wote.
Kumbuka kwamba, baba yangu anathibitika kabisa kwamba ni baba yangu.
Mungu ni dhanio (hypothesis)
Mungu is just like a theory trying to explain the origin of the universe 🌌
Atheist na theist wote kwa pamoja hawana majibu ya uhakika.
Sasa theory hii lazima iwe challenged via logical arguments.
Na ukichallenge utaona haifiti katika mzani wa kimantiki.
Hizo Epicurean paradox ni moja ya tochi inayoumulika uongo wa wazi kabisa.
Sema kama unabisha
Unatakiwa utoe majibu sahihi yenye kumake sense. Ukisema Mungu hayupo kwa sababu ya kukosa majibu ya swali hilo hapo juu unakuwa unaongelea kuhusu swali na sio kutoa majibu ya swali. Una kimbia swali kwa kusema " Mungu hayupo". Unakuwa sawa sawa na mwanafunzi anae sema swali hili limekosewa kwa sababu hajui jawabu lake. Kwa hiyo Athiests acheni kukimbia swali. Njooni tuumize vichwa kwa pamoja tuje na majibu ya swali hilo hapo juu pamoja na maswali yote mnayo kuuliza.
Na inaonekana huelewi maana halisi ya atheist & atheism kwa ujumla
Kwanini Mungu mwenye upendo wote, mwenye uweza wote na mjuvi wa yote anaruhusu viumbe wake wateseke? Hilo ni swali ambalo wewe mwanadamu umeulizwa na Mungu
Unapaswa kuthibitisha mungu huyo kwanza.