Je, Azam itafika mbali kwa kujitangazia uadui na Simba?

Je, Azam itafika mbali kwa kujitangazia uadui na Simba?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimeoma mara kadhaa baadhi ya wachezaji na viongozi wa Azam wakiikejeli Simba kwa namna ambayo tunaona mashabiki wa Yanga wakifanya.

Azam wamejitahidi sana kuikamia Simba katika miaka hii miwili na kufanikiwa kuifunga kitu ambacho ni kizuri kwa timu kujipima kwa mkubwa. Hata hivyo tumesikia malalamiko yao mengine pia Simba haina uwezo ila inabebwa na TFF na kuikandamiza timu yao.

Jambo la kusikitisha ni kuwa pamoja na uwekezaji mkubwa waliofanya,bado walitolewa mapema mno katika mashindano ambayo hayasimamiwi na TFF.

Wiki iloyopita nimeoma CEO wao akilaumiwa vikali kuwa ameshiriki katika hujuma ya kutaka Simba asifike hatua ya makundi.Kwa maksudi amefanya vitendo vya kuharibu saikolojia ya timu ili ikishindwa, waungane na yanga kuizodoa Simba na kujaribu kuthibitisha propaganda zao walizozizoea mara zote.

Ninapenda kuwauliza Azam, je kujitangazia uadui na Simba, kunaweza kuwasaidia kufika mbali?

Binafsi nahisi huo ni uswahili na tabia za vigagula. Kwa uwekezaji mkubwa mliofanya itakuwa ni vichekesho mkianza battle na timu ya Simba na sisi mashabiki nyoyo zetu zimeshatumbukia nyongo.Mtaharibu biashara zenu kwani nguvu yetu sio ndogo
 
FB_IMG_16963573793473303.jpg
 
Back
Top Bottom