Je, baada ya James Rugemalira wa IPTL kuachiwa huru, nini hatma ya majizi waliotajwa bungeni na Mh. Tundu Lissu?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592

Je nini hatma ya wote hawa waliodaiwa kugawiwa hela za Escrow na James Rugemalira wa IPTL?

Je hao watu walioitwa majizi na Mh. Tundu Lissu bungeni ndio tuhuma zilizowakabili zimefutwa na sasa nao hawana hatia?

Je hii ina maana gani zaidi ya kwamba hizo hela walizovuna zilikuwa halali zao!

Je kitendo hicho kimetoa funzo na tafsiri gani kwa wananchi walipa kodi wa taifa hili?
 
Kuna fukuto la Rugemalila kuishtaki serikali kwa kumfunga bila kumfikisha mahakamani na kutowepo ushahidi wa kutosha.

Hivyo hitimisho laweza kuwa ni kwa serikali (kwa kushirikiana na mpangaji wa ile ghorofa ya nje) kuyamaliza nje ya mahakama na James Rugemalila na malipo kuwa ni siri.

Ila serikali itajifunza kuhakikisha ina vigezo na vielelezo vyote vya ushahidi juu ya mtu yoyote inaemtuhumu kwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
 
View attachment 1942762

Je hii ina maana gani zaidi ya kwamba hizo hela walizovuna na juzitafuna zilikuwa halali zao!

Je kitendo hicho kimetoa funzo na tafsiri gani kwa wananchi walipa kodi wa taifa hili?
Wacha wajitafunie mapesa wajanja.

walikurupuka kufungua kesi wasizoweza kusimamia

in fact kesi ya Ruge ingeenda na wengi.

Ruge ni mwanaume. He does not bow on anything
 
Kwa kweli nasubiri kwa hamu kumuona Ruge anachukua hatu gani kwani miaka minne jela si mchezo. Wakati anafunguliwa kesi na kuwekwa ndani SSH alikuwa makamu wa Rais na sasa baada ya corona kumwahi bosi wake karithi kiti na Ruge kaachiwa. Hapo ndipo patamu na ndipo unafiki wa Watanzania unapotia fora! Adui mkuu wa taifa hili hakika ni CCM.
 
Ila serikali itajifunza kuhakikisha ina vigezo na vielelezo vyote vya ushahidi juu ya mtu yoyote inaemtuhumu kwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Hilo halikuwa tatizo kwa dhalimu mwendakuzimu, alikuwa anazoa tu kama kokoro, sheria iwepo isiwepo. Akikohoa tu rugaruga wanapigana vikumbo kutekeleza hata pale agizo ni haramu. Adui mkuu wa taifa letu ni CCM.
 
Kwa kweli nasubiri kwa hamu kumuona Ruge anachukua hatu gani kwani miaka minne jela si mchezo. Wakati anafunguliwa kesi na kuwekwa ndani SSH alikuwa makamu wa Rasi na sasa baada ya corona kumwahi bosi wake karithi kiti na Ruge kaachiwa. Hapo ndipo patamu na ndipo unafiki wa Watanzania unapotia fora! Adui mkuu wa taifa hili hakika ni CCM.
Hana hiyo jeuri na hata hawezi kuishitaki serikali
 
Kwanza hata Rugemalila hakuwai kuwa mwizi tuache janja janja TANESCO WALIPASWA KULIPA KIASI WALICHOMLIPA KWA UZALISHAJI UMEME HATA LISSU MWENYEWE KUNA HOTUBA ANASEMA WAMEONEWA HIVO SOMETIMES SIASA TUZIWEKE PEMBENI!!! Magufuli alikuwa shetani kabisa yan
 
Wanaotuhumiwa kuvuna hela za ESCROW ni pamoja na aliyekuwa Rais, Mawaziri, Wabunge, Waendesha mashtaka, Majaji, Viongozi wa dini, Wakuu wa Idara na Taasisi mbali mbali, Vyombo vya dola na wengine wengi tu.

Kwa Ruge kuachiwa huru ni kwamba wote hao wamesafishwa na kama walivuna ilikuwa halali yao...hii hali yafikirisha kweli kweli na inaonesha how low we have sunk kama taifa. Adui Mkuu wa taifa hili bila kupepesa macho ni CCM.
 
View attachment 1942762

Je nini hatma ya wote hawa waliodaiwa kugawiwa hela za Escrow na James Rugemalira wa IPTL?

Je hao watu walioitwa majizi na Mh. Tundu Lissu bungeni ndio tuhuma zilizowakabili zimefutwa na sasa nao hawana hatia?

Je hii ina maana gani zaidi ya kwamba hizo hela walizovuna zilikuwa halali zao!

Je kitendo hicho kimetoa funzo na tafsiri gani kwa wananchi walipa kodi wa taifa hili?
Wewe mi kila kulala, Seth inatakiwa mludishe ml.300
 
View attachment 1942762

Je nini hatma ya wote hawa waliodaiwa kugawiwa hela za Escrow na James Rugemalira wa IPTL?

Je hao watu walioitwa majizi na Mh. Tundu Lissu bungeni ndio tuhuma zilizowakabili zimefutwa na sasa nao hawana hatia?

Je hii ina maana gani zaidi ya kwamba hizo hela walizovuna zilikuwa halali zao!

Je kitendo hicho kimetoa funzo na tafsiri gani kwa wananchi walipa kodi wa taifa hili?
Lissu si aliwaita wezi kutokana na report ya tume ya Zitto Kabwe na Deo filikunjombe au?
 
Wanaotuhumiwa kuvuna hela za ESCROW ni pamoja na aliyekuwa Rais, Mawaziri, Wabunge, Waendesha mashtaka, Majaji, Viongozi wa dini, Wakuu wa Idara na Taasisi mbali mbali, Vyombo vya dola na wengine wengi tu.

Kwa Ruge kuachiwa huru ni kwamba wote hao wamesafishwa na kama walivuna ilikuwa halali yao...hii hali yafikirisha kweli kweli na inaonesha how low we have sunk kama taifa. Adui Mkuu wa taifa hili bila kupepesa macho ni CCM.
Inakuwaje adui awe CCM wakati hata wapinzani na wao wanatetea mafisadi na wanafurahia mafisadi wakiachiwa?
 
Alivyokamatwa tulilalamika nakusema kaonewa.

Ameachiwa tunalalamika tunasema kapendelewa.
 
Wanaotuhumiwa kuvuna hela za ESCROW ni pamoja na aliyekuwa Rais, Mawaziri, Wabunge, Waendesha mashtaka, Majaji, Viongozi wa dini, Wakuu wa Idara na Taasisi mbali mbali, Vyombo vya dola na wengine wengi tu.

Kwa Ruge kuachiwa huru ni kwamba wote hao wamesafishwa na kama walivuna ilikuwa halali yao...hii hali yafikirisha kweli kweli na inaonesha how low we have sunk kama taifa. Adui Mkuu wa taifa hili bila kupepesa macho ni CCM.
Ukiwa na akili finyu utasingizia wasioonekana au ujumla ili ufiche umoja. Mfano adui wa nchi hii ni CCM! Hivi una akili kweli? CCM haiwezi kuwa baya bali watu binafsi walio katika CCM. Aliyeasisi Wizi wa Escrow ni JK, unaogopa kumtaja unaitaja CCM. Lazima muondokane na akili za upunguani kuhangaika na ujumla baadala ya umoja ili kuinusuru nchi yetu.
 
Kuna fukuto la Rugemalila kuishtaki serikali kwa kumfunga bila kumfikisha mahakamani na kutowepo ushahidi wa kutosha.

Hivyo hitimisho laweza kuwa ni kwa serikali (kwa kushirikiana na mpangaji wa ile ghorofa ya nje) kuyamaliza nje ya mahakama na James Rugemalila na malipo kuwa ni siri.

Ila serikali itajifunza kuhakikisha ina vigezo na vielelezo vyote vya ushahidi juu ya mtu yoyote inaemtuhumu kwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Huna akili. Unasema bila kumfikisha mahakamani na kule Kisutu alikuwa anaenda ni nyumbani kwenu.
 
Back
Top Bottom