Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,306
- 3,228
Haya mambo mengine ni child abuse, unyanyasaji wa watoto.Baba yangu alikuwa kanali wa jeshi la wananchi (jwtz)huko kusini mwa Tanzania mkoa unaozalisha mahindi kwa wingi hapa nchini mzee wetu alikuwa mkali Sana
Kweli alizidisha ukali na ukatili pia. Na nyie muwe waangalifu msiwe kama mzee wenu kwani mtoto wa nyoka nyoka pia.Baba yangu alikuwa kanali wa jeshi la wananchi (jwtz)huko kusini mwa Tanzania mkoa unaozalisha mahindi kwa wingi hapa nchini mzee wetu alikuwa mkali Sana
Nakumbuka mwaka 2008 wakati Mimi nko darasa la sita ,kaka yangu mkubwa first born yupo form one na mdogo angu marehemu kwa Sasa (r.i.p) tulipewa kazi ya kubeba tofali 100 Mimi na Kaka, mdogo wetu abebe tofali 50 na sehemu zilipokuwa tofali ni mbali Sana hakuna gari unabeba kichwani unavuka Kama mitaa 3 mikubwa nakumbuka siku Ile tulibeba tofali mpaka unalia njia nzima unapumzika ukikutana mtu mnaye fahamiana anakupiga tafu kidogo,nakumbuka bimkubwa alikuwa ana toa machozi kutuhurumia na sauti kwa mzee hana ilibidi tupambane tu
Tukio lingine home tulikuwa na eneo kubwa mzee alipanda miti ya matunda na migomba kila mtu alipewa miti yake ole wake mti wako unyauke utachezea fimbo na adhabu zakutosha
Ukirud shuleni baada ya kula unachukua ndoo zako unaenda mtoni kuchota maji tulikuwa tunaisha karibu na mto na usiku ata arudi saa 6 anachukua tochi anapita kugagua kila mti Kama umepata maji ya kutosha ole wako usimwagilie utaenda mtoni usiku kuchota maji umwagilie
Nakumbuka nilikuwa mchezaji mzuri Sana wa mpira nishachaguliwa Sana umintashuta na umisenta kwenda kuwakilisha shule kwenye soka Ila tatizo mzee alikuwa hataki kusikia habari za mpira alichotaka yeye ni kusoma tu na saa 12 jioni uwe ndani kipaji kikapotea...
Tukio lingine nyumbani tulikuwa tunafuga kuku Kuna siku moja kuku mmoja jogoo kumbe hakulala ndani na sisi hatukukagua na tulikuwana na jogoo mmoja tu kwa wakati huo usiku kumbe mzee ajalala anasikilizia saa 9 jogoo awike kimya saa 11 alfrajiri Tena kimya jogoo ajawika akatoka kwenda chumba Cha kuku kuangalia kumbe yule jogoo hayupo nakumbuka tuliamsha wote nyumba nzima tukatafute kuku Hadi tumpate ilikuwa kasheshe kila pori tunatafuta hatuna ata tochi tulifanikiwa kumpata asubuhi kesi ikaisha
Ni matukio mengi Sana yalitokea home mzee alikuwa mafia afu acheki ovyo majirani walikuwa wanamuogopa Sana
Nw kastaafu yupo nyumbani tu Japo ukali umepungua wajukuu na ndugu wanaoishi pale wananienjoy tu
Wasukuma wengi wana ukatili mkubwa.Naskia Marehem Maghufuli alishawahi mueleza mkewe kwamba Kuna mtu ataleta mchanga tipa moja, mwambie amwage sehemu flan, watu wa mchanga walipokuja mama Janet hakusimamia ule mchanga umwagwe sehemu ambapo Maghufuli alisema umwagwe, Maghufuli kurudi akamwambia mke wake kwamba, kwa sababu ulizembea mchanga ukamwagwa ndipo sipo, usombe upeleke nlipokuwa nimesema, mama wa watu akaanza kuusombelea na karai anabeba kichwani .
Sawa, usisahau kuwapa na mbinu za kutengeneza pesa ni muhimu sana angali mapemaNinatabia kama za baba yako, minacheka humu Jf tu..☹️
Km ni kweli yule mzee alimfanyia hivyo mkewe basi alistahili kilichompata.Naskia Marehem Maghufuli alishawahi mueleza mkewe kwamba Kuna mtu ataleta mchanga tipa moja, mwambie amwage sehemu flan, watu wa mchanga walipokuja mama Janet hakusimamia ule mchanga umwagwe sehemu ambapo Maghufuli alisema umwagwe, Maghufuli kurudi akamwambia mke wake kwamba, kwa sababu ulizembea mchanga ukamwagwa ndipo sipo, usombe upeleke nlipokuwa nimesema, mama wa watu akaanza kuusombelea na karai anabeba kichwani .