Je, Bagamoyo Port itakuja kuwa White Elephant Port?

1.Usiendeleze bandari yoyote
2.Usijenge barabara hata za kusini
3.Umiliki wa ardhi miaka 99
3.Usihoji kuhusu matumizi ya Ardhi
4.Marufuku TRA kufika Bagamoyo
5.Gawio la mapato ya bandari litaamriwa na mwekezaji atakapopenda.
.
.
.
Nikasema waliokubali mkataba kama huu ni uzao wa Mangungo.
 
Kuhusu stendi nakuunga mkono kuna ujinga mwingi umefanyika. Kuna mikoa stendi iko karibia km20 toka mjini, yaani ni mateso wakati basi zinazoingia stendi kwa wakati mmoja hazizidi 10.
 
Serikali watachukua maoni yako Kwa ajili ya Taifa
Nalog
 
Ijengwe tu.
Tunapenda vya Bwerere. Na mchakato ufanyike haraka ikiwezekana ndani ya this year wachina wawe washatia timu kuanza ujenzi. Kwa Tanzania ina kilomita za mraba ngapi.? Hata tuhangaike na Kaardhi kadogo ka Bagamoyo.
Kama ni vyanzo vya mapato tunavyo vingi.
Wakituachia baada ya hio miaka 100.
Wajukuu zetu watafaidika. Watatuona mababu zao tulikuwa magenius kuwaachia huo mradi.
Naunga mkono hoja Bagamoyo port. Lazima ijengwe..! 🤗🤗🤗
 
Mataga na misukule mingine haitaki kabisa kuamini kuwa msukule mkubwa kashatangulia
 
Unajiona umeandika point za msingi kumbe ni upumbavu mtupu, tariff hupangwa na kuendeshwa na nchi husika, China akijenga bandari bado atakuwa hana mamlaka ya kukusanya kodi, eti unasema bandari ya dar inajitosheleza hivi nyie mnakula vyakula gani vinavyoondoa akili zenu, kwani hata xikijengwa bandari 50 kuna ubaya gani? Propaganda alizowalisha mwendakuzimu kwel ziliwakaa kichwani nyie wadanganyika.
 
Mwamba umemaliza
Mwamba ummemaliza
 
Kwa hiyo serikali kutochangia hata 100 huo ndo umeona ujanja.....yaani mtu akujengee nyumba usitoe hata 100 halafu uendelee kuamini akilini mwako kwamba hiyo nyumba ni yako, huoni hapa kuna kiini macho.....

..mimi nimemuelewa tofauti kidogo.

..hebu tuangalie mifano hii miwili.

A: chukulia mfano wa hasara ya ATCL ambapo zimewekezwa fedha za walipa kodi wa Tz.

B: linganisha na hasara ya kampuni ya ndege kama Precision Airline ambayo 100% ni fedha za muwekezaji.

..kati ya hasara hizo mbili wewe unaona ipi ina afadhali?

..ukipata jibu sasa lihamishie kwenye bandari ya Bwagamoyo.

Cc Mkaruka
 
Nenda kanye mbele huko mtu gani huna zuri hata moja, ni nchi gani ilinunua ndege kwa pesa zake ikapata faida ndani ya muda mfupi, pili nikukumbushe tu kazi ya serikali ni kutoa huduma sio kufanya biashara, sasa kuwa na soko au stend nzuri unataka serikali ipate faida we zuzu nini, magufuli ana mabaya yake kama binadamu lakn sio kama unavyosema wewe, time will tell, tuombe uhai
 
Kaka umeongea kama muelewa na mchambuzi makini, kuna watu wanaleta ushabiki na chuki dhidi ya jpm. Lazima tuelezwe tuelewe bandar ya bagamoyo itafanya nini na port zetu zitafanya nini na faida na hasara
 
5. Pia serikali itagharamia kazi ya kuongeza kuna cha bandari
 
Sio inefficient mzee, maana ya inefficient ni kwamba kazi zipo lakn haiperform, itakua domant kabisa no work mzee
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bandari yetu itakuwa the most inefficient in EA, tupo hapa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa ni ndogo sana kwa ustawi wa Uchumi hasa ukizingatia kuwa tumeshaingia uchumi wa kati, tunatakiwa kwenda juu zaidi.
Mbona unajichanganya hivi?

Kusudi la mada yako ni lipi hasa, kuelezea juu ya hizo 'access na exits' ulizoweka humo kwenye mada?

Huyo "white elephant", mbona hukumwonyesha nasi tumwone?
 
Je hao wachina wanaotaka kuwekeza bandari ya trillion 23 bagamoyo mizigo wataitoa wapi?
Watapitishia nini hapo?
Hili lina jibu lake, huenda hujalitafuta vya kutosha hata humu humu JF.
Bila shaka kwenye mazungumzo mkataba wa bandari ya bagamoyo utapitiwa upya na kufumua mashariti yote yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Hili ndilo ninalolitazamia sana kwenye hiyo timu ya majadiliano. Kama kweli kuna watu wanaoijali Tanzania kwenye timu hiyo, sina pingamizi na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Hiyo bandari itakuwa ni ya manufaa makubwa sana kwa nchi yetu.
 
Huyo mwekezaji wa kichina atafaidi kila kitu kwa 100%, yaani ni kana kwamba hilo eneo tumewazawadia wachina wafanye uwekezaji wao, bwerere, waluguru wanasema chobwedaa.........na hapo hapo watatudai pesa ya kuichimba hiyo bandari, hatari na nusu....
 
Uzi wako umechanganyachanganya maneno ya kiingereza ili uonekane msomi, lakini hamna lolote. kwanza mradi wa Bagamoyo sio wa serikali wala mkopo kwetu, hivyo hiyo white elephants ni kwa hao wawekezaji, je kuna muwekazaji wa kuweka $10b= 23t kwenye hasara? Na inawezekana vipi mtu ajenge mradi wa bandari wa 23t ashindwe kuweka hizo barabara za kufika hapo bandarini? Ifahamike mbali ya ujenzi wa hiyo bandari kutakuwa na ujenzi wa viwanda zaidi ya 900, hata kama sio kwa mpigo ila hiyo ndio plan. Acheni kujifanya wasomi huku mkifanya upotoshaji wa kijinga.
 
Huyo mwekezaji wa kichina atafaidi kila kitu kwa 100%, yaani ni kana kwamba hilo eneo tumewazawadia wachina wafanye uwekezaji wao, bwerere, waluguru wanasema chobwedaa.........

Hivyo viwanda vitakavyojengwa hapo navyo watafanya kazi wachina tu? Isitoshe huo mradi ni ushirikiano baina ya China na Oman. Kuna upotoshaji usio wa msingi, na sababu hasa ni serikali yetu kuficha mikataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…