Wakuu, Tutakapoanza bulk products hasa za Chuma na mkaa wa mawe, na project za Primary industries machinery, bandari ya Dar haitatosha. Pana ufinyu wa maneuvrebility. Kuna mtaalamu ambaye tuliwahi kufanya naye Tume ya Rais ya Kurekebisha mashirika ya Umma, kama Utilities Advisor akiwa Mtaalamu mwelekezi kutoka Uingereza, Barbara Harris, mwajiriwa wa DfID (wakati huo 1999-2006), yupo ktk mradi huo wa bandari ya Bagamoyo katika jopo la Washauri Elekezi. Ni mtu straight, hawezi kufanya mradi wenye utata.
Jambo moja nililojifunza ambalo naweza kusema ndilo udhaifu wetu kama nchi katika miradi ya kimataifa k(wa uzoefu wangu) ni katika masuala ya mikataba, We seriously lack competence in negotiation skills.
Kuna maeneo ambayo tupende tusipende, tunatakiwa kujenga capacity ya negotiation skills. Na hili haliji ndani ya miaka mitano au kumi. Linatakiwa kuwa eneo la kujengea uwezo constantly hata miaka 20 au 30 mfululizo.
Tumeanza miradi ya Oil and gas kitambo. Tumeweza kujenga uwezo wa wataalamu wa kufanya kazi katika miradi hiyo kwa ngazi ya ufundi lakini hata tukianzisha degree programmes za Legal Aspects of Oil and Gas bado haitatufanya tuwe experts katika maeneo hayo.
Tunatakiwa kuwapeleka wasomi hao kwenye attachments katika nchi kama za Ghuba, Urusi, Venezuela na Afrika Magharibi pamoja na Angola ili waone changamoto zinazopatikana huko na zinavyoshughulikiwa.
Then tutakuwa na uzoefu thabiti wa kuhandle masuala kama hayo.
Katika eneo la masuala ya bandari, pale PSRC tuliwahi kupata ushauri wa wataalamu mahiri kutoka Rotterdam Marine Group (RMG). Rotterdam ni mji-Bandari. Ndilo eneo linaloaminika duniani kote sababu kuna vyuo vya uendelezaji na uboreshaji huduma za bandari chenye kutambulika kimataifa.
Kampuni kubwa kama za kuhudumia Bandari kubwa zaidi duniani kama Hutchinson Wampoa inayoendesha huduma katika bandari kubwa za Hong Kong, Malaysia, Phillipines, Singapore na za Ulaya, wataalamu wake husoma hapo Rotterdam.
Hapa kwetu bado hatuna wataalamu wengi waliosoma kule. Pia tunahitaji kupeleka wataalamu wakasome na kufanya kazi pale na kwingineko kupata uzoefu unaoitwa Intermational Best Practice. Tunalikosa hili katika maeneo mengi yakiwemo maeneo ya uchimbaji na biashara ya madini mbalimbali yakiwemo ya dhahabu, chuma, nickel, cobalt na vito, ambayo tunayo.
Ukisoma LLB ukapata LLM na hata PhD havikufanyi kuwa best negotiator for your country on these technical fronts.
Katika urekebishaji na ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma, tuliajiri Mtaalamu MwelekeI Kiongozi (Lead Adviser) Mwingereza mwenye asili ya Jamaica, Prof. Cesley Sampson. Prof. Sampson alianzisha mpango wa Local Experts Capacity Building in international transactions ambapo kwa kila mradi uliohitaji mtaalamu mwelekezi wa kimataifa, alitakiwa kuajiri local law firm.
Ndivyo jinsi kampuni za IIMMA advocate, Mkono Advocates, Sinare-Mwandambo Advocates na nyinginezo zilivyojenga uwezo wa utaalamu wa mikataba ya kimataifa na kuendelea nayo hata baada ya PSRC kumaliza shughuli zake.
Yatupasa kama taifa kuhakikisha kuwa katika kila sekta muhimu kama madini, oil and gas, railway, port development nk tunakuwa na Mradi unaoajiri timu ya Wataalamu Elekezi ambao wanakuwa wanaajiriwa kwa muda tu kupitia miradi hiyo. Hao watasaidia kutujulisha vipaumbele vya msingi katika Capacity building kwa watu wetu.
Lakini wakati tunajenga hiyo capacity, wataserve kama Proxy Negotiators kwa miradi ambayo inaanza au kuendelea. Itatupuguzia kesi za mikataba ya kimataifa.... [emoji120] I stand to be corrected