Je, bandari kavu Kibaha kupunguza msongamano Dar umeyeyuka?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Mojawapo ya mipango madhubuti chini ya Hayati Dkt. John Magufuli ilikua uanzishaji bandari kavu Kibaha ili kuhamisha shughuli ya uchukuaji mizigo ya ma-container nje ya bandari.

Kusudi la mradi huo ni ili kuondoa msongamano wa malori katikati ya jiji na pia kuondoa msongamano bandari ya Dar es Salaam. Mizigo kwa macontainer ingepelekwa kibaha kwa reli kwa hivyo malori yangeishia kibaha badala ya kuja bandari ya DSM.

Mpango huu utekelezaji huenda ukaenda na mwendazake. Kuna watu hawataki mabadiliko kutokana na jinsi walivyowekeza na mazoea.

Hata kama mipango inahusika vipi kukuza ufanisi na maendeleo wao wataangalia tu maslahi binafsi na kuhujumu mipango ya maendeleo.
Mpango wa bandari kavu kibaha ni wa kimaendeleo sana wahujumu wowote wapigwe vita na kutimuliwa bila kusita.
 
Taarifa mtoa mada: huu ni mpango ulioasisiwa na awamu ya nne chini ya Dr. Jakaya Kikwete Mrisho na Mzee Mkapa aliratibu industrial parks, Je, unapokea taarifa?
 
Hiyo plan ilikuwepo tokea Enzi za kikwete kila kitu kilikuwa Kwenye mstari
 
Ujenzi wa bandari kavu Kwala unaendelea.Sasa hivi wanajenga barabara toka Vigwaza hadi Kwala (15 km)
 
Taarifa mtoa mada: huu ni mpango ulioasisiwa na awamu ya nne chini ya Dr. Jakaya Kikwete Mrisho na Mzee Mkapa aliratibu industrial parks, Je, unapokea taarifa?
Muhimu ni jpm kwa kutekeleza. Nchi hii mipango mingi inaishiaga kwenye makaratasi huku watu wakiwa wamelipwa kupanga tu.
 
kweli mkuu, kama hii ishu ya jana bandarini kwa mimi mburula naona kabisa ni kwamba eneo ni dogo na malorry yanatapakaa kurasini na bandarini mpaka njia inakuwa ndogo cha muhimu waarakishe ile bandari kavu na nafasi itapatikana ya kupakulia mizigo mingine
 
Mojawapo ya mipango madhubuti chini ya Hayati Dkt. John Magufuli ilikua uanzishaji bandari kavu Kibaha ili kuhamisha shughuli ya uchukuaji mizigo ya ma-container nje ya bandari.

Kusudi la mradi huo ni ili kuondoa msongamano wa malori katikati ya jiji na pia kuondoa msongamano bandari ya Dar es Salaam. Mizigo kwa macontainer ingepelekwa kibaha kwa reli kwa hivyo malori yangeishia kibaha badala ya kuja bandari ya DSM.

Mpango huu utekelezaji huenda ukaenda na mwendazake. Kuna watu hawataki mabadiliko kutokana na jinsi walivyowekeza na mazoea.

Hata kama mipango inahusika vipi kukuza ufanisi na maendeleo wao wataangalia tu maslahi binafsi na kuhujumu mipango ya maendeleo.
Mpango wa bandari kavu kibaha ni wa kimaendeleo sana wahujumu wowote wapigwe vita na kutimuliwa bila kusita.

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Ilikuwa ni idea nzuri and still is, hivi walikuwa watumie SGR au hii MGR ya zamani?
 
Weka picha tuthibitishe usemacho
Sina picha ila mkandarasi, Estim, yupo site tangu January na nimetoka huko wiki mbili zilizopita. Na bango linaonesha barabara ni ya zege. Ukiwa hapo Mizani huwezi kuona maaana wameanzia kwa mbele kidogo.
Kakamate pori huko kabla wengi hawajastuka.
 
Ujenzi wa Bandari kavu Maeneo ya Ruvu ndio ulikuwa Mpango wa Serikali, na lengo ilikuwa ni kupinguza msongamano katikati ya Jiji na haswa bandarini.

ila baadhi ya viongozi wamesha sahau.
 
Huko kibaha sijui kuna balaa gani!nakumbuka kulikua na mradi wa mambo ya malaria hadi mizengo pinda alienda kuzinduasijui kama bado ule mradi au ndio kifo cha mende na wenyewe!
 
Ujenzi wa Bandari kavu Maeneo ya Ruvu ndio ulikuwa Mpango wa Serikali, na lengo ilikuwa ni kupinguza msongamano katikati ya Jiji na haswa bandarini.

ila baadhi ya viongozi wamesha sahau.
Wamesahau tena vipi wakati ujenzi unaendelea?
 
Sina picha ila mkandarasi, Estim, yupo site tangu January na nimetoka huko wiki mbili zilizopita. Na bango linaonesha barabara ni ya zege. Ukiwa hapo Mizani huwezi kuona maaana wameanzia kwa mbele kidogo.
Kakamate pori huko kabla wengi hawajastuka.
Mkuu barabara ya 15km ya zege inatumia muda gani kujengwa?
 
Siwezi kujua.Ila hiyo barabara ni tambarare mno na ina maji mengi sana.Kipindi cha mvua hakuna gari iliyoweza kupita maana madimbwi yalikiwa makubwa sana.Naona wametumia muda mwingi kunyanyua tuta
 
Back
Top Bottom