Je, bangi si haramu? Tunaelekea wapi baada ya Morocco kuhalalisha?

Je, bangi si haramu? Tunaelekea wapi baada ya Morocco kuhalalisha?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Hili limenishtua sana. Morocco ni nchi ya Kiislamu kwa asilimia 99.9 inawezaje ruhusu ulimwaji wa Bhangi kwa kusema ni zao la Biashara? Hapa mbona kama wanatuchanganya?

Screenshot_2022-10-07-09-00-49-669_com.twitter.android~2.jpg
 
Morocco ni nchi yenye viongozi wenye akili sana. Bangi ni zao la biashara! Kwa Tanzania linastawi katika maeneo mengi! Bangi ikilimwa kama zao la biashara, vijana wengi watajikwamua kiuchumi!

Bangi inahitajika kwa wingi katika nchi za Ulaya na Marekani, kwa ajili ya kutengenezea dawa, na pia kama kilevi!

Viongozi wetu wakiamka kutoka usingizi wa pono, nchi hii itaendelea sana kiuchumi. Huwa napata maumivu makali sana nionapo askari polisi na wakuu wa wilaya wakiteketeza mashamba ya bangi yaliyo stawi vizuri, na kuwakamata wakulima!! Hongera sana kwa serikali ya Morocco kwa kuugundua huu mgodi unaotembea!

Siku nikiwa Rais wa nchi hii, kilimo cha bangi kitaruhusiwa mara moja kama ilivyo kwa kilimo cha tumbaku. Kuna watu wanavuta bangi, na hawana shida yoyote ile.
 
Bangi sio haramu, na kama ni haramu hata alie ifanya atakuwa ni haramu pia
 
Sheria yetu ya kudhibiti bangi ni ya hovyo sana

Jana Biden kasamehe wafungwa wote wa bangi, na itahalalishwa marekani
 
Back
Top Bottom