Morocco ni nchi yenye viongozi wenye akili sana. Bangi ni zao la biashara! Kwa Tanzania linastawi katika maeneo mengi! Bangi ikilimwa kama zao la biashara, vijana wengi watajikwamua kiuchumi!
Bangi inahitajika kwa wingi katika nchi za Ulaya na Marekani, kwa ajili ya kutengenezea dawa, na pia kama kilevi!
Viongozi wetu wakiamka kutoka usingizi wa pono, nchi hii itaendelea sana kiuchumi. Huwa napata maumivu makali sana nionapo askari polisi na wakuu wa wilaya wakiteketeza mashamba ya bangi yaliyo stawi vizuri, na kuwakamata wakulima!! Hongera sana kwa serikali ya Morocco kwa kuugundua huu mgodi unaotembea!
Siku nikiwa Rais wa nchi hii, kilimo cha bangi kitaruhusiwa mara moja kama ilivyo kwa kilimo cha tumbaku. Kuna watu wanavuta bangi, na hawana shida yoyote ile.