Wakuu nimekutana na haya madai kuwa upungufu wa nguvu za kiume unaweza kusababishwa na ugonjwa wa Bawasiri.
- Tunachokijua
- Bawasiri, inayojulikana kama piles, ni hali ambapo mishipa katika njia ya haja kubwa na sehemu ya chini ya puru huvimba na kutanuka. Kulingana na eneo lao, bawasiri zinaweza kuainishwa kuwa za ndani au nje kulingana na kuwa ndani ya puru au chini ya ngozi karibu na njia ya haja kubwa.
Dalili za Bawasiri.
Tovuti ya kliniki ya Cleverland inabainisha kuwa kuna dalili za Bawasiri ya nje na Bawasiri ya ndani. Bawasiri ya ndani mara nyingi hazisababishi maumivu na kwa kawaida huwezi kuzihisi, isipokuwa zinapotoka nje ya njia ya haja kubwa. Watu wengi huwa hawajui kama wanazo kwa sababu ziko ndani ya puru.
Dalili zinaweza kujumuisha
- Kuona damu nyekundu ang’avu kwenye karatasi ya chooni, kwenye kinyesi au ndani ya choo.
- Bawasiri kutoka nje kupitia njia ya haja kubwa (prolapse). Wakati mwingine inaweza kurudishwa taratibu ndani.
- Kuwashwa au muwasho kuzunguka njia ya haja kubwa.
- Vimbe au mabonge magumu karibu na njia ya haja kubwa yanayoweza kuwa na maumivu au kuhisi uchungu.
- Maumivu au hali ya kuuma kwenye njia ya haja kubwa, hasa unapokaa.
- Kutokwa na damu unapojifuta baada ya kujisaidia.
JamiiCheck iimefuatia machapisho na tafati za afya ambazo zinabinisha kuwa si kweli kuwa ugonjwa wa bawasiri unaweza kuwa chanzo cha upungufu ama kutokufanya uume kusimama imara.
Daktari Benjamin Kimaro, Bingwa wa Uzazi na Magonjwa yake (Gynaecologist) kwa Wanawake na Wanaume kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili anafafanua kuwa;
"Ieleweke kwamba njia ya haja kubwa na njia ya uzazi kwa wote, wanawake na wanaume ni njia ambazo haziingiliani kabisa na ieleweke kwamba haiwezekani kabisa mtu akiwa na bawasiri ikawa changamoto ya nguvu za kiume au ikawa changamoto kuleta shida kwenye homoni au changamoto ya kuweza kumpa mwanamke ujauzito kwa maana ya mbegu, haviingiliani kabisa."
Dkt. Kimaro anaendelea kufafanua kuwa;
"Labda kama mtu atakuwa na bawasiri katika ile gradi kile kiwango cha juu sana labda inaweza ikamsababishia yeye kutokuwa na ile raha ya kutaka kufanya tendo ikapunguza uwezekano sasa wa yeye kukutana na mwenza wake kwa ajili ya kupata mtoto.
Lakini kifiziolojia au kipatholojia hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwamba mtu mwenye bawasiri atapata changamoto ya nguvu za kiume atapata changamoto ya homoni zake kuwa na shida au atapata changamoto ya zile mbegu kuto kutokuwa na nguvu au hazitoshi haina mahusiano ya moja kwa moja labda tu imletee shurba ya ku yeye kutoweza kufanya vizuri katika tendo ili aweze kumpa mwanamke ujauzito".