Je benki zinatuibia?

Benki zetu Tz wanaibia wateja kwa kuchukuwa advantage ya uchanga wa ushindani katika sekta binafsi. Kwa maoni yangu.

Ku-charge matumizi ya ATM zilizowekwa na benki yenyewe ni kiashiria wazi cha wizi wa benki zetu. Lengo la ATMs kwa mtazamo wa kibenki ni kupunguza gharama za kuajili tellers na kupunguza masaa ya ku-oparate benki huku zikihudumia mteja anayehitaji cash masaa 24. Kwa mantiki hii, ku-charge mteja anayetumia ATM ni wizi 100% kwasababu mteja huyu angekwenda benki, manager wa benki angetakiwa kumwajiri teller ambaye atamlipa mara dufu (ATM sio assets za benki bali ni substitute za tellers ambazo zinapunguza garama za kuendesha benki). Banks should be thankful that wateja wanatumia ATM badala ya kwenda Benki.

Benk katika nchi zilizoendelea sasa zinajaribu ku-automate hata shughuli nyingine za kibenki anazohitaji mteja kama vile manunuzi ya fedha za kigeni, ufunguzi wa account, ulipaji wa bili kwa mteja, na uhamishaji wa fedha kutoka account moja kwenda nyingine..hii yote nikujaribu kukata gharama za kuendesha benki na hivyo kuongeza faida. Kutoza shughuli hizi na zile za ATM ni wizi 100%.

Tatizo Tz bado ushindani wa kibihashara ni almost zero (which defines profit margin), na mteja ndio mteswa katika hali kama hii. Benki zetu zote, comfortably, zimekuwa ziki act oligopolistic na hadi hapo zitakapokuwa zinahofia ushindani ndipo zitaacha ku-archage huduma kama ATM, n.k.
 
Matatizo mengine ni kuona kuwa kila huduma ni Luxury. Katika nchi ukitaka umeme inabidi mteja anunue nguzo za umeme, vitu kama hivi sio vya ajabu.

Nina akaunti yangu CRDB. Inabidi nilipie dollar 2.5 Kila mwezi kwa online access. Na kwa mwaka kuna 5 dollar fee. Na nikirudi bongo naifunga akaunti yenyewe.

Huduma za ATM ni bure kama ATM hipo kwenye banki yako. Hii ni sawa na kwenda dirishani tu.

Ukiwa unachukua pesa kutoka kwenye ATM ya benki nyingine kuna uwezekano wa kulipa fee kwa sababu ya kunaweza kuwa na matumizi ya third party.
 

Pole sana Bazazi kwa observation hiyo.Pamoja na maelezo mazuri ya Bankers kama alovoeleza Mkuu Mzeba hapo juu namna ya kuishikisha adabu benki yoyote ni kuwithdraw amana yako.
Itaje tu benki hiyo, na wakijitoa wateja hata elfu moja tu wenye amana za kutosha, benki hiyo yaweza kufilisika.
 

...Naam naam... tufahamishani hizo benki sugu, CRDB ishatajwa hapa, neeeexxxxt!

...nakereka sana na matumizi ya ATM machine Tanzania. mfano; upo kule juu Lushoto, ATM iliyopo ni ya NMB tu, ukitaka kutoa pesa inabidi ushuke mlima wenye kona na miteremko mikali mpaka Korogwe ndiyo upate ATM yenye Visa logo...

....sasa imagine safari yote hiyo halafu unakuta ATM haina hela. Nazungumzia hili kwa manufaa ya wote, wazawa na tourists ambao spending power inakuwa restricted kwenye few changed dollar bills, kuogopea 'kabali.'

Serikali ishurutishe ATM zote nchini ziwe na withdrawal fee moja, na zitumie pia Visa (labelled) card, miaka ya kutembea na mabulungutu ya fedha yeshapitwa na wakati!
 
Go to school my friend, acha kung'ang'ania kusoma biblia tu!

my friend, nimeuliza nikiwa nataka tu kujua nyie mnaotumia bank how it work, maana personal najiwekea zaangu uchagoni na maisha yanasonga mbele kama kawa sina muda wa kupanda magario tokaa huku kujijini nlipo hadi mjini kisa kufuata bank..........

wend njema
 
Kwa wale waliotembea nje, benki za Uingereza zina ada kubwa ajabu. Za Marekani ni nafuu. Hata kama unaishi Uingereza, unaweza kuweka fedha zako Marekani.

Pamoja na wizi wa mabenki, nchi zinaiba vile vile kwa kupitia mabenki. Ukiweka fedha benki lazima wako watakaozimezea mate tu. Kuna nchi wana kodi inaitwa transaction tax. Yaani wanachukua asilimia fulani ya transaction zako zote za benki.

Australia wanachukua US$10 toka telegraphic transfer yoyote inayopitia Australia. Na nchi nyingi za South Pacific communication systems zao hupitia Auastralia, kwa hivyo watu wote wanaoishi humo huibiwa fedha na serikali ya Australia kila wanapotuma fedha nje.

Mobile Phone Banking ambayo nasikia inaingia Tanzania sasa huenda ikasaidia sana wananchi wa kawaida. Watu wataweza kuweka, kutuma na kuchukua fedha zao kwa kupitia maduka ya mitaani. Naamini fees zitakuwa za kukubalika.

Banks steal from us, and nations use banks to steal from us too.
 
Hazikuibii mzee ndo biashara ya Benki hiyo.

ila ela zangu si wanakopesha watu wanapata interest, ATM na monthly charges ni sawa ila hiyo elifu tano nahisi utakuwa unaibiwa
 
...Naam naam... tufahamishani hizo benki sugu, CRDB ishatajwa hapa, neeeexxxxt!
NBC (National Bank of Commerce) although am not sure if it is real a National bank
- Monthly service fee = 600/-
- ATM or Teller fee per transaction = 400/-
- Kupatiwa kard mpya baada ya kupoteza ya zamani = 11,000/-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…