mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Hivi ni kweli biashara ya bar na kumbi za starehe ina laana? Zamani nilikuwa na rafiki yangu mfanyabiashara aliyekuwa anaishi Chunya, Mbeya. Wakati huo, mimi nilikuwa katika biashara za magari, zote tukiwa tumerithi kutoka kwa wazazi wetu.
Katika mazungumzo yetu kuhusu maisha na biashara, nilimshauri kwamba, kwa kuwa alikuwa na fedha, angeweza kuanzisha sehemu ya starehe Chunya, kwani wakati huo hakukuwa na sehemu nzuri za starehe.
Alinijibu kwa urahisi na kusema, "Mwanangu, biashara ya bar ina laana. Chunguza familia ambazo ama baba, mama, au familia kwa ujumla wanamiliki biashara hiyo – wengi huishia kuharibikiwa, kufilisiwa, kuchoka, kufa na magonjwa ya aibu, au kupata ajali. Hakuna maisha marefu kwenye hiyo biashara, na usijaribu hata kufikiria."
Miaka ilipita, na rafiki yangu huyo aliaga dunia. Siku moja, nilikuwa kwenye sehemu ya starehe mjini Mbeya (City Pub), ambapo nilikutana na mfanyabiashara mwenzangu. Katika mazungumzo yetu, nilieleza kisa hicho kuhusu biashara za starehe. Naye alinipa ushauri mkubwa akisema kuwa biashara hiyo haina baraka, na hata alitoa mifano kutoka kwenye Biblia. Maneno yake yalinishtua na kuanza kujiuliza kama kweli biashara hii ina matatizo.
Nilichogundua ni kwamba:
Nauliza kwenu: Biashara ya bar na kumbi za starehe huko kwenu imekaaje?

- Biashara hii huvuma kwa muda mfupi na kisha hufa ndani ya miaka michache.
- Inahusisha dhuluma nyingi.
- Familia nyingi zimepoteana baada ya biashara hii kufilisika.
- Wengi huanza biashara hii, lakini wachache sana huweza kudumu.
- Ni vigumu kupata muda mwafaka wa kuendelea kuboresha biashara hiyo.
- Faida yake ni ndogo sana, na mtaji na faida havilingani.
- Matukio ya vifo vya wamiliki wake hufanana sana – iwe ni magonjwa, ajali, nk.