Je, biashara ya Bar ina laana?

Je, biashara ya Bar ina laana?

Basi wenye viwanda vya kutengeneza pombe wangekua na laana wote, biasha zipo palepale kinachofanya muone ni laana ni kwamba wamiliki wa hizo biashara wanakua maarufu hivyo kila wanachofanya mnakiangalia kwa makini
 
Vipi biashara ya Guest, haina laana maana kwa kiasi kikubwa ndio nyumba za kunyanduana kuliko kulaza wageni
 
Laana ni neno ambalo limetungwa ili kutisha watu, hamnaga laana hapa duniani kama mkwanja upo fungua hata danguro cha muhimu upate pesaaa
 
Mtazame Jessica Kikumbi bila shaka utaona uzi wako wa kipumbavu
😀 😀 Unajuaje kama hana laana au ziko njiani?

Au ukiwa na pesa basi laana zinaisha?

Usiite uzi wa mtu kuwa wa kipumbavu, wakati unaona anafanya kama kukusanya data.

Labda tungemuuliza laana kwake ni nini?

Katika kuchungulia chungulia vitabu kadhaa na kujifunza naweza kusema laana ni matokeo mabaya yanayotokana na mchakato wa awali wa vitendo au shuguli fulani kuelekea uelekeo fulani usioelezeka(undefined), shughuli hizo zinaweza kuwa nzuri au mbaya.

Japo jambo zuri au baya linategemea maadili na tamaduni za watu husika,pia mtazamo na maadili ya mhusika. Kw

Ili isiwe laana, basi inabidi katikati ya shughuli au mchakato kuwe na jitihada za kuusoma huo uelekeo usioelezeka na kuchukua tahadhari.

Kwa mfano Single au single mothers wengi baadae wataleta single mothers au fathers aidha kwa watoto wao au wajukuu, uwezekano wa link kuendelea kwa atleat mtoto au mjukuu mmoja kati ya wengi upo kwa kiasi kikubwa.
Na kuna uwezekano pia ilianzia kwa babu au bibi.

Utakuta babu alisababisha mimba sehemu na hakuwahi kujua, wala hakuweza kupatikana tena.

Kumjibu jamaa naweza kusema hata kazi ya kuwa kiongozi wa dini inaweza kuwa na laana, angalia watoto wa baadhi ya viongozi wa dini wanavyokuwa
 
Biashara.
1. Iwe imehalarishwa na serikali.
2. Ilifuate taratibu zote za kiserikali.
Ni biashara nzuri na haina laana kwa mmiliki wa hiyo biashara.

Mfano Guest house.
Hii biashara inafanana kabisa na Hoteli ndogo.
Guest house kamili inatakiwa iwe na sehemu ya chakula na vinywaji ili mgeni asisumbuke kutafuta hayo mahitani ya lazima.
Kama Kuna baadhi ya wateja watafanya uovu wao humo haita mhusu mwenye biashara.

Lengo la biashara halari ni kutoa huduma kwa mwananchi, kulipa Kodi serikalini, kuzalisha ajira na kujiongezea kipato kwa mwenye biashara.
Biashara yenye laana ni ile inayofanywa bila ridhaa ya serikali. Eg. Guest Bubu. Bangi, Gongo nk.
 
Hivi ni kweli biashara ya bar na kumbi za starehe ina laana? Zamani nilikuwa na rafiki yangu mfanyabiashara aliyekuwa anaishi Chunya, Mbeya. Wakati huo, mimi nilikuwa katika biashara za magari, zote tukiwa tumerithi kutoka kwa wazazi wetu.

Katika mazungumzo yetu kuhusu maisha na biashara, nilimshauri kwamba, kwa kuwa alikuwa na fedha, angeweza kuanzisha sehemu ya starehe Chunya, kwani wakati huo hakukuwa na sehemu nzuri za starehe.

Alinijibu kwa urahisi na kusema, "Mwanangu, biashara ya bar ina laana. Chunguza familia ambazo ama baba, mama, au familia kwa ujumla wanamiliki biashara hiyo – wengi huishia kuharibikiwa, kufilisiwa, kuchoka, kufa na magonjwa ya aibu, au kupata ajali. Hakuna maisha marefu kwenye hiyo biashara, na usijaribu hata kufikiria."

Miaka ilipita, na rafiki yangu huyo aliaga dunia. Siku moja, nilikuwa kwenye sehemu ya starehe mjini Mbeya (City Pub), ambapo nilikutana na mfanyabiashara mwenzangu. Katika mazungumzo yetu, nilieleza kisa hicho kuhusu biashara za starehe. Naye alinipa ushauri mkubwa akisema kuwa biashara hiyo haina baraka, na hata alitoa mifano kutoka kwenye Biblia. Maneno yake yalinishtua na kuanza kujiuliza kama kweli biashara hii ina matatizo.

Nilichogundua ni kwamba:

  1. Biashara hii huvuma kwa muda mfupi na kisha hufa ndani ya miaka michache.
  2. Inahusisha dhuluma nyingi.
  3. Familia nyingi zimepoteana baada ya biashara hii kufilisika.
  4. Wengi huanza biashara hii, lakini wachache sana huweza kudumu.
  5. Ni vigumu kupata muda mwafaka wa kuendelea kuboresha biashara hiyo.
  6. Faida yake ni ndogo sana, na mtaji na faida havilingani.
  7. Matukio ya vifo vya wamiliki wake hufanana sana – iwe ni magonjwa, ajali, nk.
Nilipenda sana siku moja kuwa na sehemu ya starehe hapa Jombe, lakini haya niliyoyaona na kusikia yanazidi kunitia shaka. Siku moja rafiki yangu Mhindi alinishauri kuwa na mawazo tofauti ya biashara na kuepuka bar, akidai kuna matatizo. Aliendelea kusema nifikirie biashara kama mgahawa mzuri lakini sio kuuza vileo.

Nauliza kwenu: Biashara ya bar na kumbi za starehe huko kwenu imekaaje?
Jombe kwanza ni wapi.....
 
LAANA ni mambo ya kufikirika yasiyo na uhalisia, labda point ya ulipofafanua ya kuwa mtaji ni mkubwa na faida ni kidogo ina mashiko.
Biashara ya pombe ingekuwa na laana viwanda vya pombe ndiyo vingeanza kufilisika lakini maajabu ni kati ya entities zinazoongoza kwa kupata faida kubwa na kudumu kwa muda mrefu.
 
Umetafuta Information za kuprove jambo unaloogopa kulifanya, Labda nikukumbushe TBL ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza kuingiza pato kubwa la taifa...

Kivipi useme bar hailipi? Such a Coward
Yaah hata mimi hii kitu nimeiona kwa mleta uzi.
Ametafuta data za kuprove uoga wake na zile za kumchallenge kaachana nazo.

Sijui faida ndg zangu wanaipimaje ila ile biashara inalipa aisee bar ikiwa kubwa na faida inakua kubwa vilevile. Bishaa unanunua kwa bei ya chini zaidi tofaut na wenzio kama unachukua mzigo mkubwa.

Hamna laana kwenye hiyo biashara, biashara yoyote ina wakati wa kua juu na kuna muda hushuka, changa karata zako vyema. Ukibweteka na biashara inabweteka
 
Unasema faida ndogo wakati waheshimiwa wanywaji wananunua bia 2500 ambayo sehemu nyingine inauzwa 1800!
 
Back
Top Bottom