Je, biashara ya Bar ina laana?

Basi wenye viwanda vya kutengeneza pombe wangekua na laana wote, biasha zipo palepale kinachofanya muone ni laana ni kwamba wamiliki wa hizo biashara wanakua maarufu hivyo kila wanachofanya mnakiangalia kwa makini
 

Vipi biashara ya Guest, haina laana maana kwa kiasi kikubwa ndio nyumba za kunyanduana kuliko kulaza wageni
 
inategemea ntu na ntu biashara nzuri sana hii me naipendaa ukishaimiliki ukaiweza unakuwa maarufu.
 
Laana ni neno ambalo limetungwa ili kutisha watu, hamnaga laana hapa duniani kama mkwanja upo fungua hata danguro cha muhimu upate pesaaa
 
Mtazame Jessica Kikumbi bila shaka utaona uzi wako wa kipumbavu
πŸ˜€ πŸ˜€ Unajuaje kama hana laana au ziko njiani?

Au ukiwa na pesa basi laana zinaisha?

Usiite uzi wa mtu kuwa wa kipumbavu, wakati unaona anafanya kama kukusanya data.

Labda tungemuuliza laana kwake ni nini?

Katika kuchungulia chungulia vitabu kadhaa na kujifunza naweza kusema laana ni matokeo mabaya yanayotokana na mchakato wa awali wa vitendo au shuguli fulani kuelekea uelekeo fulani usioelezeka(undefined), shughuli hizo zinaweza kuwa nzuri au mbaya.

Japo jambo zuri au baya linategemea maadili na tamaduni za watu husika,pia mtazamo na maadili ya mhusika. Kw

Ili isiwe laana, basi inabidi katikati ya shughuli au mchakato kuwe na jitihada za kuusoma huo uelekeo usioelezeka na kuchukua tahadhari.

Kwa mfano Single au single mothers wengi baadae wataleta single mothers au fathers aidha kwa watoto wao au wajukuu, uwezekano wa link kuendelea kwa atleat mtoto au mjukuu mmoja kati ya wengi upo kwa kiasi kikubwa.
Na kuna uwezekano pia ilianzia kwa babu au bibi.

Utakuta babu alisababisha mimba sehemu na hakuwahi kujua, wala hakuweza kupatikana tena.

Kumjibu jamaa naweza kusema hata kazi ya kuwa kiongozi wa dini inaweza kuwa na laana, angalia watoto wa baadhi ya viongozi wa dini wanavyokuwa
 
Hapa duniani hakuna kosa, laana,.........bali tafsiri.
 
Biashara.
1. Iwe imehalarishwa na serikali.
2. Ilifuate taratibu zote za kiserikali.
Ni biashara nzuri na haina laana kwa mmiliki wa hiyo biashara.

Mfano Guest house.
Hii biashara inafanana kabisa na Hoteli ndogo.
Guest house kamili inatakiwa iwe na sehemu ya chakula na vinywaji ili mgeni asisumbuke kutafuta hayo mahitani ya lazima.
Kama Kuna baadhi ya wateja watafanya uovu wao humo haita mhusu mwenye biashara.

Lengo la biashara halari ni kutoa huduma kwa mwananchi, kulipa Kodi serikalini, kuzalisha ajira na kujiongezea kipato kwa mwenye biashara.
Biashara yenye laana ni ile inayofanywa bila ridhaa ya serikali. Eg. Guest Bubu. Bangi, Gongo nk.
 
Jombe kwanza ni wapi.....
 
LAANA ni mambo ya kufikirika yasiyo na uhalisia, labda point ya ulipofafanua ya kuwa mtaji ni mkubwa na faida ni kidogo ina mashiko.
Biashara ya pombe ingekuwa na laana viwanda vya pombe ndiyo vingeanza kufilisika lakini maajabu ni kati ya entities zinazoongoza kwa kupata faida kubwa na kudumu kwa muda mrefu.
 
Umetafuta Information za kuprove jambo unaloogopa kulifanya, Labda nikukumbushe TBL ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza kuingiza pato kubwa la taifa...

Kivipi useme bar hailipi? Such a Coward
Yaah hata mimi hii kitu nimeiona kwa mleta uzi.
Ametafuta data za kuprove uoga wake na zile za kumchallenge kaachana nazo.

Sijui faida ndg zangu wanaipimaje ila ile biashara inalipa aisee bar ikiwa kubwa na faida inakua kubwa vilevile. Bishaa unanunua kwa bei ya chini zaidi tofaut na wenzio kama unachukua mzigo mkubwa.

Hamna laana kwenye hiyo biashara, biashara yoyote ina wakati wa kua juu na kuna muda hushuka, changa karata zako vyema. Ukibweteka na biashara inabweteka
 
Unasema faida ndogo wakati waheshimiwa wanywaji wananunua bia 2500 ambayo sehemu nyingine inauzwa 1800!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…