Je biashara ya Kondo la uzazi la Mbwa ina ukweli?

Je biashara ya Kondo la uzazi la Mbwa ina ukweli?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Leo asubuhi nikiwa zangu mtaani nanyoosha miguu nikakutana na swahiba yangu mmoja ambaye aliomba kuzungumza na mimi. Tulitafuta sehemu tukakaa na kuanza kuzungumza.
images - 2025-06-14T175454.329.jpeg

Tulijuliana hali na kuelezeana machache kuhusu maisha, na nilipomuuliza kuhusu harakati zake za maisha alidai kuwa anafanya kazi ya kununua Kondo za uzazi za wanyama haswa mbwa. Mwanzoni nilipigwa butwaa kusikia kuwa Kondo la uzazi la Mbwa lina dili kiasi hicho.
images - 2025-06-14T175421.193.jpeg

Yeye alidai kuwa kitu hicho kina matumizi makubwa sana kwenye matibabu, na ukipata makondo yasiyopungua 10 basi muuzaji atakuwa na pesa za kutosha sana. Amekuwa akisafiri kwenda nchi kama Uganda, Burundi kutafuta hizi vitu.
images - 2025-06-14T175412.241.jpeg

Nilishindwa kumhoji zaidi kuhusu jambo hilo ingawa nimewahi kusikia mara kadhaa watu miaka ya 2000 mwanzoni wakitafuta makondo ya uzazi ya wanyama kama Ng'ombe na Mbuzi.
images - 2025-06-14T175454.329.jpeg

Natamani nifahamu ukweli je kuna ukweli wowote kuhusu hili, je Kondo lina matumizi ya kitabibu ama ni biashara ya ujanja?
 
Huu uzi umeuleta kimkakati sana, watakuja pm wengi kutaka uwaunganishe na huyo jamaa, na hapo ndo watapigwa za uso,,,, ukute huyo jamaa ni wewe mwenyewe
 
Sio kwamba anataka kukuingiza king?

Je ulipomdadisi umeonaje ?.
Sikutaka kumtoa kwenye reli ndo maana sikumuuliza zaidi hiyo kitu ipoje!?

Mwamba ana maisha mazuri aisee sio kitoto!
 
Sikutaka kumtoa kwenye reli ndo maana sikumuuliza zaidi hiyo kitu ipoje!?

Mwamba ana maisha mazuri aisee sio kitoto!
Wewe una viashiria vya utapeli ila kijanja sana. Kuna wajinga watakutafuta uwapige.
 
Ushindwe kumuuliza vizuri mtu mnayefahamiana ukimbilie kumuuliza sisi usiotufaham.

Kuna mawili hapa

Kama wewe sio tapeli basi umechanganyikiwa
 
Back
Top Bottom