Ndugu usijitese bure. Nimeshashuhudia ndoa ikivunjika kisa mwanaume alibeba maneno ya vijiweni/mitandaoni akaenda kuanza kumuhoji mkewe kuhusu aliyemtoa bikra. Ugomvi ukawa mkubwa hadi ndoa ikavunjika. Ukweli ni kwamba wanaume wengi kama sio wote tungependa sisi tuwe ndiyo tuliotoa bikra za wake zetu. Lakini kwa hali ya jamii ilivyo sasa jambo hilo sio rahisi mana vijana wengi wanaanza ngono kwenye umri mdogo. Ningependa ulichukue hivi:
Si kila kitu tunachotamani kuwa nacho kwenye maidha haya tumefanikiwa kukipata. Na kuna vingine tumevikosa na tumekubali kwamba hicho tumekikosa na maisha lazima yaendelee. Inawezekana uliza darasa la saba ulitamani uchaguliwe shule fulani ya sekondari lakini haikuwa hivyo, au ulipokuwa form 4 ulitamani kupata Div One lakini haikuwa hivyo, au ulitamani uzaliwe kwenye familia ya kitajiri lakini haikuwa hivyo ukazaliwa na wazazi wenye kipato cha katu kama sio cha chini au maskinu kabisa. Ukakubali kukosa na maisha yakaendelea. Sasa hata la bikra kubali tu kwamba umeikosa na maisha lazima yaendelee na mke wako. Huwezi kupata kila unachotaka, yaangalie mazuri mengine ambayo mkeo anayo mfanye maisha yenu mzeeke pampoja kwa upendo. Achana na habari za bikra yake. Wala haitakupngezea heshima yoyote mbele ya jamii ya leo. Tena unapoongea hayo mbele ya watu wazima utaonekana akili yako haijakomaa. Kama hukulazimishwa kumchukua awe mkeo basi jitahidi kuyawaza mazuri yake kwanza wala usiyape nafasi kichwani mapungufu yake. Utamfurahia mkeo na mtazeeka wenye amani nyingi. Haya fanya haraka nenda kamnunulie zawadi umpelekee. Mwambie mke wangu leo JF imenifundisha kukomaa kiakili, nisamehe kwa kukuuliza habari za bikra, nimeamua kukupenda kama ulivyo pamoja na mapungufu yako yote. Nitakusitiri wala sitaenda tena kukutangaza JF naomba na mimi unisitiri mapungufu niliyonayo..... nakupenda mke wangu. Halafu mpe busu zito kwenye paji la uso kisha mkabidhi zawadi yake.
Kila la kheri...